Narudia tena, endapo Viongozi wa Tanzania wangekuwa na nidhamu kwenye matumizi ya kodi za wananchi, inawezekana kabisa Tanzania ingekuwa nchi ya uchumi wa juu pekee katika bara hili la Afrika.
Viongozi wa nchi hii wanachukulia kama pesa za Serikali ambazo ni kodi za wananchi ni pesa zao binafsi ambapo wanaweza kuzifanyia chochote wanachowaza wakati wowote ule.
Ndo mana leo tunaona kodi za wananchi zikitumia hovyo bila huruma ilihali nchi yetu ikiendelea kukopa kila siku na kuwa na huduma zisizoridhisha karibu kila sekta.
Jana Mkuu wa Mkoa wa Arusha ametangaza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itagharamia harusi zitakazofungwa Arusha. Ikumbukwe pesa zinazosemwa ni kodi za wananchi, fedha ambazo zinatakiwa kuhakikisha barabara zote za mitaani Mkoani Arusha kuwa za lami, shule zote kuwa na miondombinu sahihi pamoja na vitabu.
Fedha hizo ndizo zinatakiwa kuhakikisha kila hospitali na zahanati Arusha zina dawa za uhakika na wananchi wanapata huduma zote za msingi.
Narudia tena kuwakumbusha wana CCM wenzangu. Ulaya tunayoiona leo haikutokea kwa bahati mbaya ila kwa nidhamu katika matumizi ya kodi za wananchi. Mnaposafiri kwenda China, Ulaya na Marekani na kupiga picha kwenye barabara nzuri, miundombinu mizuri na hata kwenda kutibiwa kwenye hospitali nzuri vile vyote havijatokea kwa bahati mbaya ila ni kutokana na wenzetu wale kuwa na nidhamu kubwa kwenye matumizi ya kodi za wananchi.
Tusitamani ifike mahala Watanzania wagome kulipa kodi au waandamane kutaka Viongozi muondoke kwenye nafasi zenu ndo mjifunze kuwa kodi za wananchi sio za kutumiwa hovyo hovyo kama mnavyojiskia
Akili ni nywele, kila mtu ana zake!
Lord Denning
Qatar