Makonda: Kesho kama huna gari aina ya Land Rover, baki tu nyumbani!

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema kuwa siku ya kesho ambayo kutakuwa na tukio kubwa la Land Rover Festival ambalo linafanyika huko jijini Arusha kama huna gari aina ya Land Rover paki tu gari lako nyumbani.

Makonda amesema kuwa kwa kuwa kesho kutakuwa na msafara wa gari zaidi ya 1000 aina ya Land Rover na kwamba kama unaishi Arusha na huna Land Rover baki tu nyumbani.

Soma pia: Godbless Lema: Land Rover Festival ni mkakati wa watu wasijiandikishe

"Kama huna jukumu lolote la muhimu la kutoka na gari basi kesho kama huna Land Rover baki tu nyumbani. Ningewaomba sana wananchi wa mkoa wa Arusha kama huna shughuli yoyote ile ya ulazima wa kutoka basi ningekuomba uvumilie siku ya kesho"

Mambo ni mengi muda ni mchache!
 
Huyu pimbi kwa kutoa boko hajambo
 
Kwa Sheria ipi... Kama ni kweli amesema au kutoa agizo hilo amekuwa misguided. Hakuna kitu kama hicho kama kubaki nyumbani
 
Ninayo Hammer je inaruhusiwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…