Makonda: Kuna UJINGA unaendelea wa kumtofautisha Hayati Magufuli na Rais Samia

Makonda: Kuna UJINGA unaendelea wa kumtofautisha Hayati Magufuli na Rais Samia

Jibu swali langu,kama Iko hivyo Kwa nini haiitwi hivyo?
Haiitwi hivyo kwa sababu kuna watu au kikundi kimeamua(take advantage of...) na kupotosha kwa maslahi yao binafsi.
Hila hizo zimefanikiwa kwa sababu; wananchi walio wengi hawafuatilii mambo ya siasa sana na hivyo kutoa uhuru kwa wanasiasa kusema au kufanya lolote wakiamini kuwa hakuna anayefuatilia.....
Naamini nimejibu swali lako japo kwa kifupi!.
 
Maslahi binafsi kama yapi? Ulitaka wafanye Kwa maslahi ya nani?
 
Maslahi binafsi kama yapi? Ulitaka wafanye Kwa maslahi ya nani?
Unapokuwa kiongozi, unakuwa na dhamana ya kutumika kwa maslahi ya wananchi waliokuchagua....katu hupaswi kutanguliza utatuzi wa mambo yako ya kibinafsi, kifamilia, kidini au kisiasa kupitia nafasi au mamlaka uliyopewa.

Vyama vya siasa, ofisi za umma na taasisi kupitia viongozi na watendaji walioaminiwa wanapaswa kuhakikisha kuwa hawavuki msitari unaotenganisha maslahi ya umma na yale yaliyo binafsi.
 
Kwani viongozi wa awamu ya 6 wanatumikia maslahi ya nani tofauti na ya Wananchi?
 
Kwani viongozi wa awamu ya 6 wanatumikia maslahi ya nani tofauti na ya Wananchi?
Kwanza hakuna viongozi wa awamu ya sita, na huu ndio ushahidi wa kile nilichoandika hapo juu kuwa hupaswi kuingiza maslahi binafsi. Hii ni awamu ya tano kikatiba na kisheria, Sasa inapolazimishwa kuwa hii ni awamu ya sita, wakati awamu tajwa itaanza baada ya uchaguzi ujao 2025....lengo la kiongozi au chama kufanya hivyo ni nini?
 
Makonda katika sherehe za kuipokea ndege mpya ya ATCL (BOEING 737-9 MAX) jijini Dar; amekemea tabia inayoonekana kuanza kukua na kukomaa kwa baadhi ya viongozi wa Serikali kwa ngazi mbalimbali ya kujaribu kutenganisha mafanikio yanayoendelea kutokea chini ya Rais Samia na kipindi cha awamu ya tano chini ya JPM.

Wakijaribu kuchafua huku na kusifia huku. Kitendo kicho makonda amekemea na kutaka tabia hiyo ife kuanzia leo.

Kwani hata kipindi cha kuomba kura wawili hao walizunguka kila mahali pamoja akiwemo waziri mkuu kasimu majaliwa.

Awataka waache UNAFIKI na KUJIKOMBAKOMBA.

Yeye makonda ndiye mpumbavu kutaka kutuletea habari za marehemu wake hapa. Magufuli alishafanya aliyoweza kwa wakati wake na kwa mazuri aliyofanya tunamshukuru,kwa sasa hayupo kutaka kumlinganisha na mtu aliyepo hai ni uduwanzi mtupu.
 
Kwanza hakuna viongozi wa awamu ya sita, na huu ndio ushahidi wa kile nilichoandika hapo juu kuwa hupaswi kuingiza maslahi binafsi. Hii ni awamu ya tano kikatiba na kisheria, Sasa inapolazimishwa kuwa hii ni awamu ya sita, wakati awamu tajwa itaanza baada ya uchaguzi ujao 2025....lengo la kiongozi au chama kufanya hivyo ni nini?
Wapo wa awamu ya ngapi?
 
Wapo wa awamu ya ngapi?
Awamu ya tano kipindi cha pili cha miaka mitano mitano.
Awamu ya tano ilianza baada ya Kikwete: 2015.
Miaka mitano ya kwanza ya awamu ya tano ilihitimishwa na uchaguzi wa 2020.
Kipindi cha pili cha awamu ya tano kinaisha mwaka 2025.
Rais atakayechaguliwa ataongoza awamu ya sita. Kama Samia atagombea na kushinda atabaki kuwa Rais wa sita awamu ya sita muhura wa kwanza.
Kama atachaguliwa Rais mwingine, huyo atakuja Rais wa saba muhura wa sita. ...Nadhani nimeeleweka.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mimi leo wala sina maneno mengi ila nataka tu kuwaambia kuwa katika siku ya leo ambapo ni siku ya mapokezi ya ndege mpya iliyonunuliwa na serikali yetu ya CCM. Mheshimiwa Paul Makonda Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa .

Kwa hasira kali na kuonyesha moyo wake kujaa jazba na uchungu moyoni ametumia muda wa dakika mbili aliopewa kusalimia kuwashambulia wanasiasa aliowaita wanafiki,wajinga na wanasiasa uchwara wanaojipendekeza na kutaka kuonyesha kuwa mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia kuwa Hayati Dkt Magufuli hahusiki nayo.

Amesema huo ni unafiki mkubwa sana na ujinga kwa sababu Rais Samia anatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025.ambayo Rais Samia na Hayati Dkt Magufuli waliinadi kwa pamoja kwa kuzunguka katika Taifa zima.hivyo anachokifanya Rais Samia ndicho alichofanya Hayati Dkt Magufuli na huwezi kuwatenganisha au kuwatofautisha ,hivyo Rais Samia anaendelea na kazi hiyo ya utekelezaji wa ilani ya CCM.

Ametoa marufuku na onyo kali kwa wanasiasa kuwa leo iwe ndio mwisho wa tabia hiyo ya unafiki na ujinga huo wa kumuweka kando au kuwatenganisha Hayati Dkt Magufuli na Rais Samia katika mafanikio ya Rais Samia. amesema kuwa Waziri Mkuu Mh kasimu Majaliwa ndiye yule yule waziri mkuu wao wote wawili yaani Hayati Dkt Magufuli pamoja na Rais Samia na Serikali ni moja na chama ni kile kile kimoja yaani CCM.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
Kijana anahangaika sana.

Subiri uchaguzi upite ndo atajua hajui
 
Kuna miradi kedekede ambayo Magufuli hahusiki.

Sasa huyo Makonda anajua hii ni awamu ya ngapi? Anatumikia mabwana wangapi?

Samia fukuza huyu Makonda
Hii awamu ya ngapi kwani uliichagua wewe??

Tunamalizia awamu ya 6 ambayo ni ya Magufuli
 
Basi wangeacha iitwe awamu ya 5 na siyo kutenganisha awamu na kuiita awamu ya 6 wakati wote walinadi sera za awamu ya Tano sasa iweje ikawa awamu ya Sita waje watwambie!! Ila Makonda muda utaongea nakukumbusha Humprey Polepole aliwahi kusema CCM wakitaka kukumaliza kuna vitu vitatu watakutengenezea sasa sitaki kuvitaja.........Tusubiri muda hiindiyo CCM
 
Kuna miradi kedekede ambayo Magufuli hahusiki.

Sasa huyo Makonda anajua hii ni awamu ya ngapi? Anatumikia mabwana wangapi?

Samia fukuza huyu Makonda
Kede kede ndio miradi gani ww chawa wa LUMUMBA ORODHESHA NDIO WATAKUELEWA WATU
 
Kede kede ndio miradi gani ww chawa wa LUMUMBA ORODHESHA NDIO WATAKUELEWA WATU
Siwezi kuweka orodha hapa maana ni Mingi across all sectors.Sekta Moja ya uvuvi na mifugo 👇👇
20240326_154435.jpg
20240326_154430.jpg
 
Back
Top Bottom