Makonda: Kuna UJINGA unaendelea wa kumtofautisha Hayati Magufuli na Rais Samia

Makonda: Kuna UJINGA unaendelea wa kumtofautisha Hayati Magufuli na Rais Samia

Eti huwezi kumtenganisha Magufuli na Samia,hivi kala maharage ya wapi huyu mshamba? Kifo kilishawatenganisha. Akapimwe akili huyu bashite
 
Awamu ya tano kipindi cha pili cha miaka mitano mitano.
Awamu ya tano ilianza baada ya Kikwete: 2015.
Miaka mitano ya kwanza ya awamu ya tano ilihitimishwa na uchaguzi wa 2020.
Kipindi cha pili cha awamu ya tano kinaisha mwaka 2025.
Rais atakayechaguliwa ataongoza awamu ya sita. Kama Samia atagombea na kushinda atabaki kuwa Rais wa sita awamu ya sita muhura wa kwanza.
Kama atachaguliwa Rais mwingine, huyo atakuja Rais wa saba muhura wa sita. ...Nadhani nimeeleweka.
Unatumia nguvu kubwa kumuelewesha chawa ambaye hajui miaka yake 5 atakuwa wapi
 
Hizo "marufuku na onyo kali" zingefuatwa na hatua mahsusi zozote zitakazochukuliwa kwa yeyote atakayekiuka. Vinginevyo tutafsiri kuwa kauli yake ni "empty threat" aka mkwara.
 
Upuuuzi huna akili kma ulega eti BBT imeleta faida Mil 100+ umeweka bill 66 kwa miaka mingapi unaleta vi hoja vya ujinga ujinga hapa ngoja CAG REPORT HALAFU TUJUE
We punguani,Toka Magufuli amekuwa Rais umewahi sikia CAG akisema Rushwa imepungua? Sana sana iliongezeka ndio maana alimtimua CAG Assad baada ya kumuumbua.

Samia ni level zingine,amewaongezea Bajeti CAG,ameajiri Watumishi wengine wa CAG zaidi ya 2000 na Amewapa vote Yao ya hela Ili akakague na taasisi ambazo Magufuli alizuia ikiwemo TanRoads na ATCL.

Usifananishe Samia na wajinga walioshindwa.👇👇

View: https://www.instagram.com/p/C4sfzEHtFU1/?igsh=MXY1OTRxY3Fmb2t2MQ==
 
Unatumia nguvu kubwa kumuelewesha chawa ambaye hajui miaka yake 5 atakuwa wapi
Inaonekana hawa watu wengi ni bendera fuata upepo, anachosema kiongozi hata kama ni uongo wanapokea tu kwa ule utamaduni wao wa huyu ni mwenzetu... Wanalindana sana na wanahitaji kuelimishwa.
 
Bila shaka huelewi hoja ya Mheshimiwa Makonda.
Nimeelewa sana ila wewe unajitia hamnazo kwa vile ni mmoja wa waliolengwa na kombora hilo. Mnapomsifia Samia bila kumtaja yule dhalim mwenzenu anakereka,kila unapomsifia Samia lazima useme anayoyafanya ni maono ya Magufuli. Sasa jitie wazimu umsifie Samia tena tu bila kumtaja Magufuli uone atakachokufanya.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mimi leo wala sina maneno mengi ila nataka tu kuwaambia kuwa katika siku ya leo ambapo ni siku ya mapokezi ya ndege mpya iliyonunuliwa na serikali yetu ya CCM. Mheshimiwa Paul Makonda Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa .

Kwa hasira kali na kuonyesha moyo wake kujaa jazba na uchungu moyoni ametumia muda wa dakika mbili aliopewa kusalimia kuwashambulia wanasiasa aliowaita wanafiki,wajinga na wanasiasa uchwara wanaojipendekeza na kutaka kuonyesha kuwa mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia kuwa Hayati Dkt Magufuli hahusiki nayo.

Amesema huo ni unafiki mkubwa sana na ujinga kwa sababu Rais Samia anatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025.ambayo Rais Samia na Hayati Dkt Magufuli waliinadi kwa pamoja kwa kuzunguka katika Taifa zima.hivyo anachokifanya Rais Samia ndicho alichofanya Hayati Dkt Magufuli na huwezi kuwatenganisha au kuwatofautisha ,hivyo Rais Samia anaendelea na kazi hiyo ya utekelezaji wa ilani ya CCM.

Ametoa marufuku na onyo kali kwa wanasiasa kuwa leo iwe ndio mwisho wa tabia hiyo ya unafiki na ujinga huo wa kumuweka kando au kuwatenganisha Hayati Dkt Magufuli na Rais Samia katika mafanikio ya Rais Samia. amesema kuwa Waziri Mkuu Mh kasimu Majaliwa ndiye yule yule waziri mkuu wao wote wawili yaani Hayati Dkt Magufuli pamoja na Rais Samia na Serikali ni moja na chama ni kile kile kimoja yaani CCM.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
Ameanza kuwa mkosefu wa adabu . Hakuna mfanano wowote wa kimawazo, kifikra, kimatendo na kimaamuzi kati JPM (Simba) na SSH (Chui)
 
Ameanza kuwa mkosefu wa adabu . Hakuna mfanano wowote wa kimawazo, kifikra, kimatendo na kimaamuzi kati JPM (Simba) na SSH (Chui)
Rais anajuta kumrudisha Makonda kwenye mfumo. Magufuli ambaye alimuamini na kumtumia makonda kwenye kazi zake chafu ifika wakati akamchoka akamuacha kimtindo kwani alikuwa habebeki. Asipodhibitiwa atawavuruga sana CCM kwani ni mtu wa visasi na ubabe wa kishamba.
 
Unahangaika sana na Makonda na kutunga vi uzushi vyako
 
Daktari Magufuli aliwaachia madaktari waamue kuhusu chanjo ya Corona lakini Dkt. Samia alihamasisha tena kwa kuchoma hadharani.

Dkt. Magufuli hakusafiri sana nje ya nchi na kuwaachia mabalozi wa wakilishe Watanzania, lakini Rais Samia hawaamini mabalozi na anaenda mwenyewe nje ya nchi.

Magufuli alipinga mikataba ya bandari kupewa wageni Rais Samia kawapa wageni.

*Makonda ajieheshimu kwa kusema ukweli, aache unafiki. Sisi watanzania wa leo tunasikia ukweli na uongo, tunaona mazuri na mabaya, tunatembea Kusini na Kaskazini hata Mashariki na Magharibi.

Watanzania tunapendana kuliko viongozi wanavyofikiri. Watanzania sasa wanajiongoza kuliko uongozi unavyowaongoza wananchi.* Kifupi sasa hivi viongozi wakiwa katika kofia ya uongozi wanafanya sanaa, wakiwa maisha ya kawaida (wakiwa nje ya kofia ya uongozi) ndipo wanapoongoza watanzania.

Hatuwezi kusema uongo, kama Rais Dr. SSH atenganishwi na Rais Dr. JPM basi ni kwa maneno tu.
Kwa matendo Samia anaenda kinyume na Magufuli.
 
Daktari Magufuli aliwaachia madaktari waamue kuhusu chanjo ya Corona lakini Dr. Samia alihamasisha tena kwa kuchoma hadharani.

Dr. Magufuli hakusafiri sana nje ya nchi na kuwaachia mabalozi wa wakilishe watanzania, lakini Rais Samia hawaamini mabalozi na anaenda mwenyewe nje ya nchi.

Magufuli alipinga mikataba ya bandari kupewa wageni Samia kawapa wageni.

*Makonda ajieheshimu kwa kusema ukweli, aache unafiki. Sisi watanzania wa leo tunasikia ukweli na uongo, tunaona mazuri na mabaya, tunatembea Kusini na Kaskazini hata Mashariki na Magharibi.

Watanzania tunapendana kuliko viongozi wanavyofikiri. Watanzania sasa wanajiongoza kuliko uongozi unavyowaongoza wananchi.* Kifupi sasa hivi viongozi wakiwa katika kofia ya uongozi wanafanya sanaa, wakiwa maisha ya kawaida (wakiwa nje ya kofia ya uongozi) ndipo wanapoongoza watanzania.

Hatuwezi kusema uongo, kama Rais Dr. SSH atenganishwi na Rais Dr. JPM basi ni kwa maneno tu.
Kwa matendo Samia anaenda kinyume na Magufuli.
japo si muhimu, ila itoshe tu kusema,
kila zama na kitabu chake 🐒

popote duniani, mitindo ya uongozi baina ya kiongozi moja na mwingine hutofautiana kulingana na falsafa na vipaumbele vya kiongozi husika. Na kwahivyo hayupo kiongozi wa kurithi kila kitu kutoka kwa mwingine alietangulia 🐒

by the way God Bless Tanzania
 
Back
Top Bottom