Makonda kupata teuzi wakati wowote kutoka sasa

Makonda kupata teuzi wakati wowote kutoka sasa

Jamaa amewekwa kama tairi ya spea, kuna wakati unaofaa watamtumia tu hilo lipo wazi pia mahaba na mahuba hayaishi bali hupoa tu.
 
Huyo mama sasa hivi amechanganyikiwa, hana hili wala lile, imebaki kutapatapa tu na kuendeshwa kama gari bovu.

Hana lolote la maana analoamua sasa hivi kwa utashi wake kama kiongozi.

Na kwa kweli nisimpe sifa bure, kwa sababu hiyo sifa ya uongozi hana. Hili linajulikana kitambo sasa.
Umeandika kwa jazba bila ku justfy lolote katika hayo uliyoandika,kifupi hujaeleweka ni kama tu umesukumwa na chuki binafsi
 
Tuwekeeni Ile picha Bashite na Maza ya kale wakiwa kwenye pozi IPO humu
 
Ukimtaja Bashite namuona Ben Saanane......Bashite na baba yake walivuka mipaka sana kuondoa Phd holder kwa mambo ya kijinga yaani kuambiwa ukweli tu unapoteza mtu?
 
Makonda namba hazipo upande wake, kinachomuokoa mpaka sasa ni kuwa alibahatika kupata cheo cha made man ndani ya family ila kwa bahati mbaya Ushamba wake ukazidi na akawa mlevi wa madaraka akasahau principle ya Made men ain’t supposed to make statements yakamkuta ya kumkuta akaondolewa kwenye family, kwa maslahi mapana ya familia hakuchukuliwa hatua kali zaidi ya kutengwa na kupewa ulinzi tu ila akanyimwa madaraka na ushirikishwaji wa aina yoyote kwenye masuala ya familia kwenye muundo wa familia ukizingua ndio bye bye. Sababu kuu ya Makonda kutochukuliwa hatua ni alikua made man safi aliye perform vizuri sana tatizo alilemewa na ujana na ushamba wa madaraka kama John Gotti, family ikaona anyway hana ubavu wa kuwa tishio kwetu tumtimue tu ila kwa yale mazuri aliyofanya tumlipe kwa kutokumchukulia hatua kali

Ole sabaya yeye aliyebahatika kuitambua family akahakikisha anatumia namna yoyote ile ili awe made man, akishirikiana na makonda ambaye tayari alikua ameshabatizwa, ili uwe made man ni lazima upate udhamini wa made man au member wa familiy, kwa bahati mbaya ndoto zake hazikutimia kwa sababu made man aliyekua anamtegemea alikanyaga live wire na kutimuliwa, so huyu joker made man (ole sabaya) ndoto zake zikaishia hapo, akakosa access ya taarifa yoyote kutoka kwenye family kwa sababu daraja lake la kuifikia familia lilikatika ikabidi abaki akiishi kwa matumaini na kuwa tayari kwa lolote litakalo tokea mbeleni. Kinachompunguzia credit za kurudishwa katika mfumo ama kuingizwa kwenye family ni unyama wake aliofanya waziwazi.
BTW usiamini sana nilichoandika.
 
CCM hamna mtu msafi,sembuse makonda,sema tu aliikosea familia ya msoga Kwa kuitaja ktk list ya wauza unga ndo maana amesahaulika awamu hii
 
Yaani cha kufanya ni kuachana na huo mkataba wa kilaghai afu kuomba msamaha kwa wananchi. kifupi hali ya hewa ishachafuka kuelekea 2025.

Hata huo wizi kwa kura utaufanyaje sasa kama most of people are against you. Itakuwa kazi kubwa kwa CCM. Bashite hana ushawishi wowote kanda ya Ziwa.
 
Mtoa taarifa wangu amethibitisha , kwanza atateuliwa ccm halafu baadaye serikalini

Mtoa taarifa huyu alinidokeza wiki moja kabla kwamba cheo cha Naibu Waziri Mkuu kinarejeshwa , nikabisha

Ikiwa kama Mnyeti amerejeshwa pamoja na uchafu wake wote , basi huenda Makonda naye akarudi
Kumbe unahisi tu kuwa kwa kuwa mnyeti karudishwa basi na makonda nae atarudishwa.. unachotakiwa ujue katika siasa haramu yako halali ya mwenzio.
 
Mtoa taarifa wangu amethibitisha , kwanza atateuliwa ccm halafu baadaye serikalini

Mtoa taarifa huyu alinidokeza wiki moja kabla kwamba cheo cha Naibu Waziri Mkuu kinarejeshwa , nikabisha

Ikiwa kama Mnyeti amerejeshwa pamoja na uchafu wake wote , basi huenda Makonda naye akarudi
Hata sabaya nayeye amrudishe tu. Hili li chama liondolewe hata kwa kuiga gabon
 
Kama Bashite atarejeshwa na Le general Lengai ole Sabaya naye arudishwe ili utatu mtakatifu wa mnyeti Makonda Sabaya ukamilike. Maana nchi imekuwa nyoro nyoro sana.
Mnataka mkali au mpole???ladha zote zipo ni ninyi tu na chaguo lenu
 
Umeandika kwa jazba bila ku justfy lolote katika hayo uliyoandika,kifupi hujaeleweka ni kama tu umesukumwa na chuki binafsi
Kama wewe ni 'chawa' wake (mnavyojitambulisha wenyewe siku hizi), ni lazima uchukulie hivyo ulivyoandika hapa, kwani huwezi kuona vinginevyo.

Inahitaji 'justification' gani kujua kuwa mama hana karama ya uongozi? Muda aliokaa madarakani hakutoshi kukuonyesha upungufu mkubwa alionao? Unahitaji 'justification' ya namna gani?

Kama itakuwa ni "msukumo wa chuki" ya kutopenda inakoelekzwa nchi hii chini ya uongozi wa huyu mama, sina lolote la kujutia kuhusu chuki hiyo.
 
Swadakta
 
Back
Top Bottom