Doubleg Malafyale
JF-Expert Member
- Feb 17, 2017
- 2,733
- 3,561
Ukiona mpaka kaongea jua kafanyiwa hilo jaribioHizi Siasa za Kurogana na Kuwekeana Sumu niliamini ziko Vyama vya Upinzani sasa Kauli ya Mwenezi wa CCM imenishtua Sana
Imenikumbusha enzi zile Wabunge wa Chadema walikuwa na dada zao Viti Maalum kwa ajili ya kuwapikia chakula kuepuka kulishwa Sumu Mitaani
Hata Dr Slaa alilalamika Chumba chake kurushiwa ungaunga kama ule wa Joka la makengeza bungeni
Yaani tunarudi kule kule dadeki 🐼
hivi huyu si aliletwa na msoga? naona amekataa kuwa kwenye msoga gangSasa Shujaa Magufuli apumzike kwa Amani
Ahsante Sana kwa Zawadi uliyotuachia ya Huyu Bwana mdogo Paul Makonda 😄
Navalonge swela 😂
Mtumishi wa Mungu ni yule atendaye na kuhubiri KWELI iletayo wokovu. Aweza kuwa mkulima, mfugaji, seremala, ...., kiongozi na siyo lazima awe kanisani, msikitini au nyumba yoyote ya ibada.Ndio maana huwa sielewi kwa nini mtumishi wa Mungu anakuwa mwanasiasa
Ilikuwa ni tahadhari tu, kwamba mtatokea....sasa...Mmetokea.Makonda anaiongelea CCM, wewe unadakia CHADEMA. Be serious
Tuliwaambia mkishamaliza kuwaua wapinzani mtaanza kuuana wenyewe ndiyo haya sasa juzi tu wamemuua Thadei Ole Mushi sasa wamehamia kwa Makonda.Katibu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Paul Makonda akiwa katika ziara yake Tunduma Mkoani Songwe amesema
"Si nimepewa usemaji? nitasema kweli bila kumung'unya maneno na kwa taarifa yenu sifi na Mungu hana mpango wa kuniondoa kwanza. Mtege sumu kwenye vyumba mnapoteza muda tu, mtafute waganga mnapoteza muda tu. Nataka kila kiongozi awajibike kwenye nafasi yake.
Waliopo serikalini wote wana magari, nyumba na wanaheshimika kwa kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan Kwanini hatumsaidii kazi? Tabia ya kusubiri Rais ana ziara ndiyo mnajitokeza na mkifika pale ooh Mama unaupiga mwingi hapa ni wewe tu!... Ngojeni dawa yenu inachemka."
Ndugu zangu Watanzania,
Hiyo ni kauli ya kijasiri kabisa iliyotolewa na Mheshimiwa Makonda Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa.kauli hiyo imetolewa akiwa anahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Tunduma.Ni kauli iliyotikisa na kutetemesha hadi mpakani mwa zambia huko kutokana na namna ilivyotolewa kijasiri na kijana jasiri.
Amesema amekuwa akiambiwa na kupewa masharti mengi mengi sana kutoka kwa watu ya kuwa mara asisalimiane hivyo na watu,mara awe makini na vyumbani ,mara yeye ni kijana bado mdogo kwa hiyo awe makini sana mara hivi mara vile. Kwa ujasiri na ukali akasema ya kuwa yeye haogopi kurogwa wala kuwekewa sumu.akasema ya kuwa yeye analindwa na Mungu tu.
Huku akishangiliwa na maelfu ya watu alisema ya kuwa Mungu akimtaka basi atammchukia tu .katika hotuba hiyo alisema kwa ukali na ujasiri kuwa tusitishaneeee hii ni wakati akieleza kuwa unakuta mwingine anasema anaongea jambo hili la kisheria kama nani? Naye akasema huyo anayeongea hivyo naye anaongea kama nani? Akasema kwanza wamesomeshwa kwa kodi za watanzania na wanalipwa kwa kodi za watanzania hivyo wasilete za kuleta.
Akasema watumishi wazembe atakula nao sahani moja na kwamba dawa yao inachemka moyoni,maana wengine wamekuwa wanalindana na kukumbatiana katika maovu,halafu wakipanda jukwaani wanasema mama anaupiga mwingi. wakati wanajuwa kuwa wala hawafanyi kazi zaidi ya uzembe na uvuvi halafu wanatoa sifa za uongo kwa Mheshimiwa Rais. amesema Ole wao wakiendelea na tabia hizo,maana hawatavumiliwa wala kuachwa salama.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
View attachment 2896605View attachment 2896606View attachment 2896607Lucas mwashambwa weka namba.
JPM tangu waziri wa Ujenzi alikua na wapinzani.Sasa mkuu, kipindi yupo benchi alikuwa na madhara gani kwao. Think hata JPM kwanini alikuja kupata maadui baada ya kuingia uwanjani wakati yupo benchi kama waziri hawakumuona?
Amegusa maslahi yao?Hivi kwa nini maccm wanataka kumuua makonda?
Katibu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Paul Makonda akiwa katika ziara yake Tunduma Mkoani Songwe amesema
"Si nimepewa usemaji? nitasema kweli bila kumung'unya maneno na kwa taarifa yenu sifi na Mungu hana mpango wa kuniondoa kwanza. Mtege sumu kwenye vyumba mnapoteza muda tu, mtafute waganga mnapoteza muda tu. Nataka kila kiongozi awajibike kwenye nafasi yake.
Waliopo serikalini wote wana magari, nyumba na wanaheshimika kwa kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan Kwanini hatumsaidii kazi? Tabia ya kusubiri Rais ana ziara ndiyo mnajitokeza na mkifika pale ooh Mama unaupiga mwingi hapa ni wewe tu!... Ngojeni dawa yenu inachemka."
Uko sawa kabisa,Ndio maana huwa sielewi kwa nini mtumishi wa Mungu anakuwa mwanasiasa
Nikipewa akili zako najinyonga!Nae anaweza mfuata shujaa mapema,kumbuka huyu hana executive power kama yule