Makonda: Marufuku kudai nyongeza ya mshahara! Nashangaa watu wanapita na mabango, mie ningewachapa

Makonda: Marufuku kudai nyongeza ya mshahara! Nashangaa watu wanapita na mabango, mie ningewachapa

Si mlisema kuwa hamtaandika habari zake Paul Makonda?? Sasa imekuwaje hadi mnaanza kumtafuta kijana wa watu? Au zilikuwa hasira tu. Makonda noma, mtake msitake, mtamuandika tu!
Hapo kuna mic ngapi???

Si ya tbccm pekee !
 
Mkuu,hiyo ni roboti na sio mtu huyo.

Ninawashangaa sana WATEULE wa RAIS wakati wao wakijipatia mishahara minono na magri makubwa ya kifahari ya kutembelea,kujiwekeza pesa za wizi ambazo hao wanaotukanwa wanalazimishwa kuzisighn/kuzitayarisha.

Hawa ndiyo walaji wakubwa wa zile 10% za ujenzi wa miundo mbinu,hawa ndiyo wale watafunaji wa mishahara hewa,hawa ndiyo wale wa kivuko hewa na barabara mbovu.Hawa ndiyo wale wa Ndege ya mwaka 1940??

Wakati anatukana wafanyakazi hawa yeye amejilimbikizia magari yaliyotaifishwa kwa wafanyabiashara wakubwa,ana majumba,anakwenda SA kwa kutumia pesa za drug lords,huyu ndiye aliyeteuliwa na mwenye Kebbys Building pale Mwenge.

Hawa ndiyo wanaona walimu waliotumia vyeti vya wenzao ni wezi kupita wao waliopiga Bilioni nane na kivuko hewa.
 
Bora awaambie ukweli, wanadai mishahara huku kazi hawafanyi.

Ni mwendo wa hapa kazi tu, kuna lipi la kushangaza kwa alichoongea!?

Na akitoa mfano, nyie lazima muukuze.

Mtajiju na muache kulalamika juu ya kuzungushwa kwenye ofisi za mji huo, huku akifata njia kuwanyoosha mnamsema.

Makonda oyeeeeeeeeeee
hivi kwa nini sometimes huwa unaniangusha hivo mam?
 
atajuaje machungu kudai nyongeza ya mshahara wakati hajawai kuajiriwa.hapo alipo ameteuliwa to, nauakika hajawai itwa kwenye interview huyu bashite sijui Makonda.
 
Wendawazimu ndivyo walivyo! Hakuna sheria yoyote ile nchini ambayo inawazuia wafanyakazi kudai nyongeza ya mishahara. Huyu jamaa ni mpuuzi sana.
Yaani mambo mengine hadi aibu....
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Bila kupepesa Macho wala kutikisa Masikio, Watumishi mjiandae kupigwa deshi kwa mara nyingine katika mwaka mpya wa fedha.

Hapo ametumwa afikishe ujumbe.
Kweli mkuu.

Maana anasema jambo ambalo halimuhusu.


Hii serikali ina vituko sana,
 
Sisi tukuwaambia ccm ni adui wa nchi hii wengine mnatuona punguani ? Nan punguani kati ya fisi na kapuku? Fisi ndio punguani
 
Kabisa BT inasikitisha na kushangaza sana kusikia kauli za kipumbavu kama hizi.


img-20170322-wa0000-jpg.511442



Yaani mambo mengine hadi aibu....
 
Kuna watu DAB anawalipa kumpigania na kurusha habari zake na kumtetea kwenye mitandao ya kijamii hata ukiangalia hizo post hapo chini utawagundua tu!
 
Back
Top Bottom