Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Mwezi uliopita, aliyekuwa mkuu wa majeshi ya ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, aliongea na waandishi wa habari wa gazeti la serikali, Daily News, kuhusu siku za mwisho za Rais John Magufuli.
Wajuzi na wajuvi wa mambo wakadai kwamba ametumwa na Samia kuyasema hayo aliyoyasema.
Kwamba hakusema tu kwa bahati mbaya. Alipewa baraka zote na Samia, ili kutuma ujumbe kwa watu flani flani.
Sasa leo/ jana huko Arusha, Gavana wa mkoa huo, Paul Bashite Makonda, katishia kuwataja watu wanaowatuma baadhi ya watu kumtukana Rais Samia kwenye mitandao ya kijamii.
Gavana Makonda kasema anawajua watu hao ambao kati yao wapo na mawaziri wa serikali ya Samia.
Gavana Makonda kawapa watu hao mpaka Jumatatu ya wiki ijayo wawe wameacha mambo wanayoyafanya, la sivyo, atawataja kwa majina!
Sasa swali ibuka ni, je, Gavana Paul Makonda naye ametumwa na Rais Samia awafikishie ujumbe watu hao kama vile ambavyo ilidaiwa Jenerali Mabeyo alivyotumwa?
Wajuzi wa mambo tujuzeni basi na sie tusio na huo ujuzi na ujuvi wenu 🙏.