Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Kwenye siasa kila maamuzi yanazaa matokeo na matokeo yanaweza kuwa chanya au hasi. Hapa chini nitaweka baadhi ya matukio ya kimaamuzi yaliyofanyika kimakosa na Rais Samia mwanzoni mwa utawala wake na yanamgharimu vibaya kwa sasa.
1. Kurithi baraza la mawaziri la Magufuli. Mbali na kuwa lilikuwa ni kosa la kikatiba pia lilikuwa ni kosa la kisiasa. Ule ulikuwa ni udhaifu mkubwa wa Samia kisiasa. Wanasiasa wale wale, leo ndio wanatumika kumzunguka na kunyemelea kiti chake.
2. Kumtengenezea Mbowe kesi ya ugaidi ili kuzima mjadala wa Katiba Mpya. Hilo lilikuwa ni kosa kubwa la kisiasa. Pasipo sababu ya msingi Samia aliamua kujitengenezea uadui na wapinzani wa CCM. Japokuwa Samia alikuja kuifuta ile kesi baadaye sana lakini itachukua muda mrefu sana kuirudisha hiyo imani.
3. Kuanza mapema wazi wazi harakati za urais 2025 kwa mwamvuli wa kijinsia. Siasa za kuukumbatia uanamke ni sumu inayochukiwa vibaya sana na jamii yenye mtizamo wa mfumo dume na wanawake wanaoamini mwanamke hafai kuwaongoza au kuwatawala. Bila kujua, ghafla wanaume na wanawake wengi wanamchukia rais Samia kwa mtizamo huo.
4. Kuwarudisha haraka serikalini na ndani ya CCM watu waliofukuzwa (kwa haki au chuki) na Magufuli au wanasiasa waandamizi waliokuwepo katika serikali au CCM kipindi cha Kikwete. Watu kama Kinana, January Makamba, Nape etc. Watu wengi wenye mtizamo chanya kuhusu Magufuli wanamuoa Samia kama mtu aliyekuja kuzika yote mema ya Magufuli ili kuyafufua yote mabaya ya Kikwete.
5. Kuwapooza au kuwakumbatia baadhi ya watu wasioweza kufaa kabisa katika utawala wake. Kundi kama la Covid 19, Sukuma gang (Bashiru, Pole Pole) lilipaswa liwe ni hadithi iliyosahaulika ndani ya wiki mbili tu toka Samia aingie madarakani. Uwepo wa hao watu bungeni, serikalini au ndani ya CCM ni kujiharibia kisiasa.
Bado Rais Samia hajachelewa sana, anaweza kurekebisha baadhi ya mambo sasa na baadhi ya mambo kwenda sawia kwa sehemu.