Makosa makubwa matano ya mwanzo ya kisiasa ya Rais Samia ambayo yanamgharimu sasa

Makosa makubwa matano ya mwanzo ya kisiasa ya Rais Samia ambayo yanamgharimu sasa

Mkuu Zanzibar-ASP, thanks for this!, very objective na hoja zote ni kweli kabisa, ila hoja ya kuwarejesha Nape na January ni baraka kwa Samia kwasababu kiukweli kabisa, hawakutendewa haki na hawakuwa na kosa lolote la kustahili kutumbuliwa!. Psychoanalysis ya Waomba Msamaha Kwa Rais, Makamba Snr is the Next, Membe Will Never for Pride, Kiburi na Jeuri, Kinana Will Never for Integrity

P
Hahahaa nimekuelewa!
Nape, January na Kinana ndio walikuwa mafundi mitambo wakuu wa 2015, waliweza kuchezea mpaka VAR ili goli la mkono lifungwe vizuri ili Edo asiende ikulu eeh!
Na hao jamaa inaonekana waliweza pia kumtingisha Magu vyema kwa ile style ya kuvujisha nyeti huku wakijificha kwenye kuvuli fake cha Pdidy wa kule Twitter.
Safari ijayo hawambebi tena mtu, wanajibeba wenyewe, Samia ajipange.

Samia alikuwa na namna bora na tofauti ya kuwalipa fadhila kuliko kuwarejesha haraka haraka kwenye post zile zile za kisiasa. Samia ameziba tundu kwa kutoboa tundu lingine. Kisiasa naona Samia alikosea.
 
Mh Rais anaendelea kujenga SGR sifa zinaenda kwa Hayati Rais JPM unaona hiyo ni haki na sawa? Wakamtafutia Royal tour anze upya. Nani ana uhakika huo kwamba umeme ukitengamaa sifa zitaachwa ziwe za Mh Rais kama walizuia za awamu ya5 zisimnufaishe inavyo stahiki.

Ikulu chamwino imeisha Raia huku kitaa wanasema JPM asingekufa angeifikisha hii nchi mbali sana katika suala la maendeleo.
Ikulu ya Chamwino ina uhusiano au mchango gani katika maendeleo ya nchi??
 
Sikia mkuu!...

Ni kwamba Samia hana uwezo wowote kiuongozi, hii inayotawala sasa hivi ni ccm ya kikwete.

Hao mawaziri wa Magufuli unaosema Samia amewarithi hakuna hata mmoja wa kumtingisha maana wenye nguvu wote kama kina Lukuvi aliwatoa akabaki na watu dhaifu tu kama kina Doroth Gwjima na kia Bashungwa.
Unamaanisha jiwe alikuwa anateua watu dhaifu ambao wamerithiwa sasa?
Kwa nini alikuwa anafanya hivyo?!
 
Umewahi kufika jimboni kwake ukapaona palivyo choka na umaskini??
Ni Moja ya Viongozi ana heshima na nguvu kubwa kubwa nyanda za juu kusin. Mikoa ya Iringa, njombe,songea ,mbeya ,rukwa na katavi na Bado maeneo mengine unaanzaje kusema mtu huyo Hana nguvu
 
Kwenye siasa kila maamuzi yanazaa matokeo na matokeo yanaweza kuwa chanya au hasi. Hapa chini nitaweka baadhi ya matukio ya kimaamuzi yaliyofanyika kimakosa na Rais Samia mwanzoni mwa utawala wake na yanamgharimu vibaya kwa sasa.

1. Kurithi baraza la mawaziri la Magufuli. Mbali na kuwa lilikuwa ni kosa la kikatiba pia lilikuwa ni kosa la kisiasa. Ule ulikuwa ni udhaifu mkubwa wa Samia kisiasa. Wanasiasa wale wale, leo ndio wanatumika kumzunguka na kunyemelea kiti chake.

2. Kumtengenezea Mbowe kesi ya ugaidi ili kuzima mjadala wa Katiba Mpya. Hilo lilikuwa ni kosa kubwa la kisiasa. Pasipo sababu ya msingi Samia aliamua kujitengenezea uadui na wapinzani wa CCM. Japokuwa Samia alikuja kuifuta ile kesi baadaye sana lakini itachukua muda mrefu sana kuirudisha hiyo imani.

3. Kuanza mapema wazi wazi harakati za urais 2025 kwa mwamvuli wa kijinsia. Siasa za kuukumbatia uanamke ni sumu inayochukiwa vibaya sana na jamii yenye mtizamo wa mfumo dume na wanawake wanaoamini mwanamke hafai kuwaongoza au kuwatawala. Bila kujua, ghafla wanaume na wanawake wengi wanamchukia rais Samia kwa mtizamo huo.

4. Kuwarudisha haraka serikalini na ndani ya CCM watu waliofukuzwa (kwa haki au chuki) na Magufuli au wanasiasa waandamizi waliokuwepo katika serikali au CCM kipindi cha Kikwete. Watu kama Kinana, January Makamba, Nape etc. Watu wengi wenye mtizamo chanya kuhusu Magufuli wanamuoa Samia kama mtu aliyekuja kuzika yote mema ya Magufuli ili kuyafufua yote mabaya ya Kikwete.

5. Kuwapooza au kuwakumbatia baadhi ya watu wasioweza kufaa kabisa katika utawala wake. Kundi kama la Covid 19, Sukuma gang (Bashiru, Pole Pole) lilipaswa liwe ni hadithi iliyosahaulika ndani ya wiki mbili tu toka Samia aingie madarakani. Uwepo wa hao watu bungeni, serikalini au ndani ya CCM ni kujiharibia kisiasa.

Bado Rais Samia hajachelewa sana, anaweza kurekebisha baadhi ya mambo sasa na baadhi ya mambo kwenda sawia kwa sehemu.
Umeandika yote ila namba tano bado hujaandika.
 
Mwambieni huyo mamaenu hii nguvu aitumie kuleta umeme, maji na kupunguza makali ya maisha kuliko huu utaahira wenu!

Kuwaondoa kina Bashiru na Polepole aliwaondoa labda useme awafukuze nchini sasa!

Unaweza kuwaondoa serikalini lakini huwezi kuwaondoa kwenye mioyo ya wale wanaoona wao wanao ukweli.

Kuuweka Utawala mpya wa kifisadi ndani ya CCM ndilo kosa kubwa linalomgharimu Samia wenu.
 
Ikulu ya Chamwino ina uhusiano au mchago gani katika maendeleo ya nchi??

Kukopea fedha ya pembejeo za kilimo inaweza tumiwa. Kumbe yale magari ya kuchimba visima yanachangia kwenye 350B za kilimo umwagiliaji kwa maana ya kuchimba na mabawa.
 
Why suala la umeme alaumiwe Mh Rais? Msaada tafadhali. Kama mambo ndivyo yanaenda hivyo basi kumhujumu Rais kumerahisishwa sana. Umeme ukame una nafasi na kule kusema mitambo ilizalisha umeme ikimuhofia mtu flani lakini haikuwahi kukarabatiwa inavyo takikana kwa miaka 5. Matokeo yake ndio haya sasa umeme umekuwa ni wa mgao wakati mitambo inafanyiwa ukarabati stahiki na kwa wakati.

Walio muumiza Mh Rais SSH na wanoo na watakao endelea ni wale waliomshauri kwamba anaweza akajitenga na Utawala awamu ya 5 wa JPM wakati yeye alikuwa Makamu wake. Kwenye kampeni wakipiga na baadaye kuongoza kwa kushirikishana.

Kimsingi mambo yote mazuri ya JPM yamebaki kuwa ya JPM wakati kiuhalisia Mh Rais SSH ana shares hapo. Na hizi shares zingekuwa mtaji mzuri mno kwake wa kisiasa kuliko kutafuta wapambe njaa kali wanao mvisha vilemba vya ukoka kulinda maslahi yao wakati kiuhalisia huku mitaani mambo sivyo yalivyo.
We maku, mitambo gani haikufanyiwa ukarabati? Ilizalishaje umeme?

Sababu ya kipumbavu kabisa hii. Huo ukarabati unafanywa mwaka mzima?

Na yale mabilioni ya kununua mfumo wakuuzia umeme mliyatoa wapi kama siyo mliyakuta mkayafuja?

Nchi mnailamba hadi imekauka halafu eti Magufuli alitumia mitambo bila kukarabati.

Ninyi, dhahama inakuja. Mnatufanya watanzania poyoyo. Mungu atatulipia 2025
 
Unamaanisha jiwe alikuwa anateua watu dhaifu ambao wamerithiwa sasa?
Kwa nini alikuwa anafanya hivyo?!
Mwambie dadako hapo kwa shemeji yako unapokaa akupikia chai unywe kwanza ndio uje kubishana na sisi wakubwa zako!
 
Umeandika yote ila namba tano bado hujaandika.
Jaribu kuwaza vyema na kutafakari. Kuna watu Samia bado anawalea ndani ya utawala wake, hawahitaji, hawana faida kwake, hakuwatengeneza yeye, wanachafua tu utawala wake, wanamuumiza tu akili nk. Kwanini hakuachana nao mapema tu, ili mambo mengine yaendelee?

Covid 19 wanamsaidia nini mama?
Bashiru anamsaidia nini mama?
Pole Pole anamsaidia nini mama?
 
Kumfanya kingai kuwa kachero mkuu wa upelelezi wkt alishatoa boko kwenye kesi ya kubumba ya mbowe.

That was a grave mistake [emoji3061]
 
We maku, mitambo gani haikufanyiwa ukarabati? Ilizalishaje umeme?

Sababu ya kipumbavu kabisa hii. Huo ukarabati unafanywa mwaka mzima?

Na yale mabilioni ya kununua mfumo wakuuzia umeme mliyatoa wapi kama siyo mliyakuta mkayafuja?

Nchi mnailamba hadi imekauka halafu eti Magufuli alitumia mitambo bila kukarabati.

Ninyi, dhahama inakuja. Mnatufanya watanzania poyoyo. Mungu atatulipia 2025

Imekuzaa.
 
Mh Rais anaendelea kujenga SGR sifa zinaenda kwa Hayati Rais JPM unaona hiyo ni haki na sawa? Wakamtafutia Royal tour anze upya. Nani ana uhakika huo kwamba umeme ukitengamaa sifa zitaachwa ziwe za Mh Rais kama walizuia za awamu ya5 zisimnufaishe inavyo stahiki.

Ikulu chamwino imeisha Raia huku kitaa wanasema JPM asingekufa angeifikisha hii nchi mbali sana katika suala la maendeleo.

Kwahiyo unasema wanaomlaumu SSH hawana uelewa wa mambo?
 
Kilichomtia doa ni maji na umeme
Hizo siasa zingine watajuana siasani humo umo
 
Back
Top Bottom