Kuna fikra za baadhi ya watu wanaotamani itokee siku moja "makosa" ya kimtazamo na kiutendaji ya Hayati John Magufuli, aliyekuwa Rais wa Tano wa serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania YAREKEBISHWE.
Kiuhalisia makosa hayo hayawezi kurekebishwa kwa kuwa umbali aliotufikisha Magufuli inakuwa ngumu sana kurudi kwenye njia sahihi kiurahisi. Kitu pekee kinachoweza kufanyika ni kusuluhisha mitazamo yetu na uhalisia wa mambo.
Kwa mfano; chuki kati ya wafuasi wake na wale waliokuwa wanaipinga falsafa yake ya undeshaji nchi inarekebishwaje? Jee watu waliodhurika wakati wa utawala wake wanaponaje ama wale waliopotea wanapatikanaje? Leo hii hawa kina Ben Saanane, Simon Kanguye, Azor Gwanda nani anajua walipo na inawezekana wakarudishwa kwa familia zao. Lissu na wengine waliopata ulemavu zama hizo maisha yao yanaweza kurejerezwa?
Nani mwenye akili timamu anayeweza kusimamisha ujenzi wa bwawa la umeme la Nyerere kwa hatua ililofikia. Au SGR inawezaje kuwachwa wakati tayari mabilioni ya shilingi yameteketea kwenye mradi huo tayari. Nani ataruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa wakati CCM amri ya marufuku hiyo haiwahusu?
@Allen Kilewella
Siku zote utambuwe kwamba wanasiasa ni kikundi kidogo sana cha watu katika jamii ya watanzania.
Ambacho kinajinufaisha na jasho la walalahoi bila chenyewe kutoa jasho.
Wakati wananchi wakitoa jasho lao,nyinyi wanasiasa mnadondosha mate,mkiyatamani matokeo ya hilo jasho lao.
Huwezi kutoka na kikundi kidogo kilichozowea uporaji kupitia vyeti feki,mishahara hewa, ubia wa wizi kimfumo na huu upumbavu mwingine unaluongea wewe humu.
Kwanza uelewe kwamba hatuwezi kukaa kila siku chadema mkitulisha habari za mauaji yasiyothibitika kufanywa na mnayemtuhumu.
Halafu ulipaswa kuelewa kwamba wananchi hawali sera za tuhuma za mauaji bali sera zenye kuwaletea unafuu wa maisha bora.
Habari yenu kukaa kila saa Saanane, Azori gwanda,sijui nini na nani hiyo haiwezi kuwapeleka Ikulu.
Watu walikufa kwa uhanga wa kisiasa tangu enzi za mababu zetu.
Pia uelewe kwamba hata hao wajerumani wanaoifadhili chadema kwa sasa,ndio waliwaua mashujaa wetu kina Mirambo,Mkwawa na Songea!
Lakini leo wameipakata chadema mapajani huku wakiwaambia Demokrasia.
Ni ujinga mtupu na ujuha uliopitiliza kama wewe Killewea na walevi wa ufisadi wenzako kuiona miradi hii ya SGR na bwawa la Nyerere ambayo ni ya kimkakati kama ni hasara kwa taifa.
Ila ukamuona huyo mama yenu anayekopa fedha kuhonga wananchi bila mikakati wala miradi endelevu na yenye tija kwa taifa.
Eti ni shujaa.
Chadema hamjitambuwi kikubwa mnachoweza ni kugawana vyeo na mahusiano ndani ya taasisi.
Ukibisha hilo nitakuwekea ushahidi humu.