Makosa ya Hayati Magufuli hayasahihishiki

Makosa ya Hayati Magufuli hayasahihishiki

Usipaniki ndugu malaika! Hakuna aliyesema utakufa. In fact nakuombea maisha marefu mpaka Jalali atakapoamua vinginevyo. Nakuasa tabia yako ya kujifanya katibu Mukhtasi wa Mungu ndugu malaika. Ujue tu Mungu hana katibu muhtasi. Na ujue wewe ni mwanadamu kama Rais Magufuli alivyokuwa. Na utasimama mbele ya Mungu kujibu kuhusu mambo yako. Jikite kuandaa utakapoishia. Magufuli amekwisha kuondoka kati ya walio hai na Mungu hahitaji ushauri wa awaye yeyote kujua amuweke wapi na kama amtunuku au amuadhibu.

Jifunze kujua mipaka yako mbele ya Mungu ndugu malaika!
Sawa dada angu
 
Unaweza kusoma tena nilichokiandika. Kama utakielewa basi sawa. Ila kama hutakielewa basi sina namna nyingine ya kuandika.

Nikutakie jioni ya baraka!
Nimesoma na kuelewa na ndiyo maana nimekunukuu.

Mungu yu mwema kwa kila mtu.
 
Kuna fikra za baadhi ya watu wanaotamani itokee siku moja "makosa" ya kimtazamo na kiutendaji ya Hayati John Magufuli, aliyekuwa Rais wa Tano wa serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania YAREKEBISHWE.

Kiuhalisia makosa hayo hayawezi kurekebishwa kwa kuwa umbali aliotufikisha Magufuli inakuwa ngumu sana kurudi kwenye njia sahihi kiurahisi. Kitu pekee kinachoweza kufanyika ni kusuluhisha mitazamo yetu na uhalisia wa mambo.

Kwa mfano; chuki kati ya wafuasi wake na wale waliokuwa wanaipinga falsafa yake ya undeshaji nchi inarekebishwaje? Jee watu waliodhurika wakati wa utawala wake wanaponaje ama wale waliopotea wanapatikanaje? Leo hii hawa kina Ben Saanane, Simon Kanguye, Azor Gwanda nani anajua walipo na inawezekana wakarudishwa kwa familia zao. Lissu na wengine waliopata ulemavu zama hizo maisha yao yanaweza kurejerezwa?

Nani mwenye akili timamu anayeweza kusimamisha ujenzi wa bwawa la umeme la Nyerere kwa hatua ililofikia. Au SGR inawezaje kuwachwa wakati tayari mabilioni ya shilingi yameteketea kwenye mradi huo tayari. Nani ataruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa wakati CCM amri ya marufuku hiyo haiwahusu?​

Tunataka tujue mchango wako kwenye hii nchi kabla ya kujadili….. ushangae ulikutwa na cheti feki!?
au ulikua unaptisha mizigo bandarini bila kodi??

Au ulitumbuliwa!!
karibu
 
Nyerere alifanya makosa na mwenyewe anakiri kabisa kuwa alikosea.

Mwinyi alifanya makosa.

Mkapa alikosea.

Kikwete kakosea pia.

Wewe una makosa mengi tu ila kwa unafiki wako unayaona ya wengine zaidi kuliko hata yako.

Hulka ya binadamu ni kukosea.

Na huwa tunajifunza kutokana na makosa.

Sasa kama kuna makosa ya Magifuli yanakukera ni vyema tuliopo tukayatumia kama njia ya kuboresha utendaji serikalini kwa manufaa ya Taifa.

Ukiachana na Makosa yake ambayo lazima awe nayo kama binadamu, ana mazuri yake pia, ni jukumu letu sisi kuyaenzi.
 
Kuna fikra za baadhi ya watu wanaotamani itokee siku moja "makosa" ya kimtazamo na kiutendaji ya Hayati John Magufuli, aliyekuwa Rais wa Tano wa serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania YAREKEBISHWE.

Kiuhalisia makosa hayo hayawezi kurekebishwa kwa kuwa umbali aliotufikisha Magufuli inakuwa ngumu sana kurudi kwenye njia sahihi kiurahisi. Kitu pekee kinachoweza kufanyika ni kusuluhisha mitazamo yetu na uhalisia wa mambo.

Kwa mfano; chuki kati ya wafuasi wake na wale waliokuwa wanaipinga falsafa yake ya undeshaji nchi inarekebishwaje? Jee watu waliodhurika wakati wa utawala wake wanaponaje ama wale waliopotea wanapatikanaje? Leo hii hawa kina Ben Saanane, Simon Kanguye, Azor Gwanda nani anajua walipo na inawezekana wakarudishwa kwa familia zao. Lissu na wengine waliopata ulemavu zama hizo maisha yao yanaweza kurejerezwa?

Nani mwenye akili timamu anayeweza kusimamisha ujenzi wa bwawa la umeme la Nyerere kwa hatua ililofikia. Au SGR inawezaje kuwachwa wakati tayari mabilioni ya shilingi yameteketea kwenye mradi huo tayari. Nani ataruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa wakati CCM amri ya marufuku hiyo haiwahusu?​
@Allen Kilewella

Siku zote utambuwe kwamba wanasiasa ni kikundi kidogo sana cha watu katika jamii ya watanzania.

Ambacho kinajinufaisha na jasho la walalahoi bila chenyewe kutoa jasho.

Wakati wananchi wakitoa jasho lao,nyinyi wanasiasa mnadondosha mate,mkiyatamani matokeo ya hilo jasho lao.

Huwezi kutoka na kikundi kidogo kilichozowea uporaji kupitia vyeti feki,mishahara hewa, ubia wa wizi kimfumo na huu upumbavu mwingine unaluongea wewe humu.

Kwanza uelewe kwamba hatuwezi kukaa kila siku chadema mkitulisha habari za mauaji yasiyothibitika kufanywa na mnayemtuhumu.

Halafu ulipaswa kuelewa kwamba wananchi hawali sera za tuhuma za mauaji bali sera zenye kuwaletea unafuu wa maisha bora.

Habari yenu kukaa kila saa Saanane, Azori gwanda,sijui nini na nani hiyo haiwezi kuwapeleka Ikulu.

Watu walikufa kwa uhanga wa kisiasa tangu enzi za mababu zetu.
Pia uelewe kwamba hata hao wajerumani wanaoifadhili chadema kwa sasa,ndio waliwaua mashujaa wetu kina Mirambo,Mkwawa na Songea!

Lakini leo wameipakata chadema mapajani huku wakiwaambia Demokrasia.

Ni ujinga mtupu na ujuha uliopitiliza kama wewe Killewea na walevi wa ufisadi wenzako kuiona miradi hii ya SGR na bwawa la Nyerere ambayo ni ya kimkakati kama ni hasara kwa taifa.

Ila ukamuona huyo mama yenu anayekopa fedha kuhonga wananchi bila mikakati wala miradi endelevu na yenye tija kwa taifa.
Eti ni shujaa.

Chadema hamjitambuwi kikubwa mnachoweza ni kugawana vyeo na mahusiano ndani ya taasisi.

Ukibisha hilo nitakuwekea ushahidi humu.
 
Kumbe?

Ilikuwa halali yake kuuawa! Mtu tayari ni rais, ila wewe na mavi yako umekazana kuhoji phd yake kwanini usile chuma?

Wapumbavu kama hao ndio dawa yao hiyo japo inawezekana kifo chake ni kma kile cha wangwe tu
Nisalimie immortal na muuaji Magufuli
 
SGR Itakuwa na faida kiasi gani na kwa muda upi?
umeme wa gas ni ghali ukilinganisha na huu wa maji, hii ndio sababu iliyofanya Magufuri a opt kwenye rufiji dam, lakini vilevile mikataba ya gas aliyoifanya kikwete unaijua?

kuhusu SGR, ni option nzuri sana kwasababu itaongeza idadi ya mizigo mara dufu kuliko hii inayopita kwenye MGR.
 
Bongo kuna watu wengi wenye ubungo mdogo sana wa kuelewa na kuchambua mambo mepesi sana. Inasikitisha sana.
SGR kwanza siyo teknolojia bali ni upana wa Reli. Treni za umeme zilikuwapo hata kabla ya kuja kwa reli za SGR. Na hoja ya kuongezeka kwa ufanisi kwa kuwa reli imekuwa ni SGR siyo kweli. Ufanisi hauletwi kwa kuwa na reli pana bali ubora wa menejimenti.

Haya ya bei ya umeme kuwa rahisi kwa kuwa unazalishwa kwa maji (Hydroelectricity) ni ya uongo. Gharama za umeme zinakokotolewa kutokana na mambo mengi sana.
 
Back
Top Bottom