Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Hali inazidi kuwa mbaya kwa vijana wetu hasa hawa wa kiume wanahamasishana kila kona na kampeni yao yenye hashtag #KATAA NDOA
Sababu wanazotoa zinachekesha mno na kwakweli hazina mashiko.. Kubwa ikiwa ni kuogopa kusalitiwa lakini pia kuna la uchoyo na kukwepa majukumu ila haya hawayasemi kwa uwazi
Hili jambo ni kama fasheni yenye mass hallucination ndani yake! Itapita lakini inaweza kuacha madhara kwa wengine hivyo hatuwezi kukaa kimya
Haya ndio makundi yao
1. Wasiojiamini
2. Wenye kasoro za kimaumbile
3. Waathirika kisaikolojia
4. Wasela na wakaa geto
5. Wenye kasoro za kijinsia
6. Wapenda kitonga, dezo
Sababu wanazotoa zinachekesha mno na kwakweli hazina mashiko.. Kubwa ikiwa ni kuogopa kusalitiwa lakini pia kuna la uchoyo na kukwepa majukumu ila haya hawayasemi kwa uwazi
Hili jambo ni kama fasheni yenye mass hallucination ndani yake! Itapita lakini inaweza kuacha madhara kwa wengine hivyo hatuwezi kukaa kimya
Haya ndio makundi yao
1. Wasiojiamini
- Hawaamini kama wanaweza kutunza mke kutokana na story za vijiweni
- Hawaajiamini kama wanaweza kumridhisha mwanamke kitandani
- Hawajiamini kama wanaweza kutulia kwenye ndoa bila kuwa na vimada
- Hawajiamini kwamba watapendwa na hawawezi kusalitiwa!
2. Wenye kasoro za kimaumbile
- Wanaojihisi ni vibamia
- Wanaojihisi hawawezi kumpa mwanamke ujauzito
- Wasiotahiriwa
- Wagumba kwa ithibati
3. Waathirika kisaikolojia
- Kutokana na makuzi mabaya
- Kutokana na malezi mabovu
- Waliolelewa na walezi katili
- Walioathirika na punyeto
- Walioumizwa kimapenzi
- Waliosalitiwa
4. Wasela na wakaa geto
- Maisha hayajasimama
- Wanaishi kwa kuungaunga
- Wasiopenda majukumu
5. Wenye kasoro za kijinsia
- Mashoga wa kujificha (mchicha mwiba)
- Madomo zege
- Wenye ulemavu uliojificha
6. Wapenda kitonga, dezo
- Wanaolelewa na wake za watu
- Wanaotunzwa na mashangazi
- Wanaopenda vya bure toka kwa yeyote
- Wapenda shortcut
- Wavivu wasipenda kujishughulisha
- Wapenda starehe
- Wanashadadia tu kwasababu fulani kasema
- Wanafuata mkumbo kwakuwa fulani yumo
- Wanadhani ndio usasa na ndio ujanja
- Walioshindwa kuhimili changamoto za ndoa
- Walioachwa, waliopigwa kibuti
- Walioharibu kwenye ndoa zao
- Wapotoshaji