Makundi ya wanaopinga ndoa na maisha ya ndoa

Nafkiri umelenga kuwaumiza kihisia ama naweza sema umeamua "kujibu mapigo" maana hoja zao ni kama haujazijibu kabisa.
Ni kawaida sana kwa Binti kuonywa kuwaepuka wanaume kwamba wanaweza haribu maisha yake na hii imefanywa na jinsia zote kwa Miaka mingi lakini kwa Vijana wa kiume hali hua ni tofauti.
Hii kampeni ya Vijana kukataa ndoa haimaanishi wanaogopa mwanamke au majukumu.. wanahofia madhara yanayotokana na "Ndoa rasmi". Sheria za Ndoa zinambana Mwanamume na kumpendelea Mwanamke bila sababu za kueleweka. Na hii inafanya wanawake kutumia mwanya huu kuwafanyia ukatili Wanaume.. huenda Sheria na taratibu zikiwa updated Kampeni kama hizi hazitosikika.. Vijana wa kiume wana haki ya kujilinda kama wenzao.. usiwe ambassador wa Harmful masculinity Amigo. Change is inevitable
 
Kuna mshkaji wangu mmoja tulikuwa tunakaa naye vikao mara kwa mara, sasa majuzikati kajichanganya akaoa! Hivi sasa kila weekend lazima aje kwangu anipe sim niongee na mke wake nimuombee ruhusa!!!
Nimemwambia weekend hii ndo mwisho atafute njia nyingine ya kutoka kwake au atulie na familia yake aenjoy (kama mnavyodanganyana) maana ndo maisha aliyochagua.
 
wanaume wa kisasa wametoka kwenye nafasi zao kimwili na kinafsi,wababa wa leo mnamchango mkubwa kwa watoto/wadogo zenu wa kiume ksma kila changamoyo inayoletwa humu ingepewa uzito na ushauri positive basi hizi kampeni za kijinga zisingekuwepo,vijana wengi wamebaki kuwa wa kiume na si wanaume ndomana hawawezi kumudu familia ..........over
 
Wanaume kama huyo rafiki yako ndo wanafanya ndoa zidharaulike mwanaume unaanzaje kuomba ruhusa kwa mwanamke pumbavu kabisa huyo rafiki yako.
Mwanaume anatakiwa aondoke na kurudi nyumbani muda wowote anao utaka
 
Huyo kaolewa mkuu, acha mazoea na mke wa mtu
 
Una uhakika gani na unacho kisema?
Nina marafiki wengi waliooa, naona na kusikia majuto yao. Nimesuluhisha sana migogoro ya ndoa na kujifunza mengi kupitia migogoro hiyo. Pamoja na yote ninekuwekea mifano michache ya watu maarufu wanaohangaika na ndoa zao kipindi hiki (Dr. Mwaka, Manara) na wewe nipe mifano ya watu wanaojuta kutooa.
Nje ya ndoa kuna uhuru, Sex (ngono) pia inapatikana kama kawaida, watoto unapata bila ndoa na zaidi unaepuka stress zisizo na ulazima.
Ndoa ni kichaka cha wanawake kuwanyonya na kuwavuruga wanaume.
#KATAANDOA
 
Wanaume kama huyo rafiki yako ndo wanafanya ndoa zidharaulike mwanaume unaanzaje kuomba ruhusa kwa mwanamke pumbavu kabisa huyo rafiki yako.
Mwanaume anatakiwa aondoke na kurudi nyumbani muda wowote anao utaka
Huo uhuru wa kurudi muda unaotaka haupo ndani ya ndoa vinginevyo mwanamke atakuvuruga mpaka ujute. Kifupi unapooa unakuwa umekubali kukabidhi nusu ya uhuru wako kwa mkeo! Ukitaka kuforce basi jiandae kulea watoto wa mwanaume mwenzako.
 
Huo uhuru wa kurudi muda unaotaka haupo ndani ya ndoa vinginevyo mwanamke atakuvuruga mpaka ujute. Kifupi unapooa unakuwa umekubali kukabidhi nusu ya uhuru wako kwa mkeo! Ukitaka kuforce basi jiandae kulea watoto wa mwanaume mwenzako.
Mkuu mwanaume huwa anaaga na sio kuomba ruhusa.

Mwanaume kabla ya kuondoka nyumbani unamuaga mkeo kuwa unaenda sehemu fulani kwenda kufanya jambo fulani ili ukipata tatizo iwe rahisi kujua na namna ya kukusaidia na sio kuomba ruhusa.
 
Kama wanatamani kutoka mbona sasa hawatoki ?
Subiri na ww uje uzae binti ili tuone kama utafurahi yy kuwa single mother.
 
Unapuyanga yote haya wakati kila kukicha unalizwa na mkeo ndani hadi unajuta kumuoa na unaogopa kusema. Ndo nyie tunawakuta mmejinyonga. #KATAANDOA
 
Ndoa imekuja kuvurugwa na wanawake wenyewe kutaka hamsini kwa hamsini(fifty fifty) kwenye kila jambo..

Halafu hapo hapo sheria zinawapendelea sana wao na kuwapa favouritism.

Sheria za Ndoa ziko kumsapoti Mwanamke zaidi kuliko mwanaume, Mwanaume yeye anabanwa na hizi sheria.

Mambo ya feminism, women empowerment, Haki sawa kwa wote..Yanawapa Ujasiri wanawake na kuwajengea imani kwamba sasa wana uwezo wa kuwa control wanaume na sheria zika wa favour wao..

Wazee na Mababu zetu walimudu ndoa kwa vile walitumia Mfumo Dume..

Sasa kwa hiki Kizazi cha sasa cha wanawake wenye kutaka "Fifty Fifty" watasubiri sana......

Ili vijana wakubali ndoa lazima "mfumo dume" uendelee kama kwa wazee wetu na sheria za ndoa zisi mnufaishe sana Mwanamke....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…