Malengo yako ya mwaka huu yametimia?

Binafsi ya kwangu hayakutimia kwa asilimia kadhaa, nilikuwa na mradi wa doda bodo
ambapo nilikuwa na kijana kusema ukweli alikuwa mwaminifu kwa kuleta rejesho.
Nikajishauri mwenyewe kwamba mwaka huu nibadilishe hiyo biashara ninunue ngómbe wa maziwa badala
ya piki piki sababu ni kwamba nilipopiga mahesabu niliona.mwisho wa mkataba pikipiki inaondoka.
lakini kwa wafugaji,unauza maziwa unarudisha fedha yako na bado unabaki na mifugo na faida nyingine kama vile mbolea shambani.

Basi bwana nikanunua mmoja mtamba nikampandisha na kuendelea kumuudumia.
mimba ikiwa na miezi mitatu,akafa ghafla na hivyo pesa yote ikapotea.
hivyo lengo langu halikutimia,sijui kama nilikosea kuchanga karata.
Nami naamini kama wewe kuteleza siyo kuanguka.
 
Simba akijeruhiwa hakimbii uwanja wa vita bali anabadili mbinu za kummaliza adui,,, kamwe usivunjike moyo, ingia vitani pambana
 
Kwa kweli Mungu ni mwema kuna malengo madogo mawili nimetatimiza na kufanikisha kwa asilimia themamini

Haya malengo madogo ndio yatanirahisishia kukamilisha malengo makuu kwa urahisi

Kazi na sala

Katika umri huu nimegundua maombi yana nguvu sana
 
Mwaka haujawa mzuri sana hasa kiuchumi, plan za kuwekeza zimefanikiwa, kisimamia uwekezaji ni jukumu lingine la 2023, mikopo ipo kama yote na tutazidi kukopa coz kama taifa(!) tunakopesheka[emoji16]
 
Vizuri kwa kujitambua mapema
 
Mwaka haujawa mzuri sana hasa kiuchumi, plan za kuwekeza zimefanikiwa, kisimamia uwekezaji ni jukumu lingine la 2023, mikopo ipo kama yote na tutazidi kukopa coz kama taifa(!) tunakopesheka[emoji16]
Madeni Ni htr mkuu, unaweza kupita road unaongea peke yako
 
Kuishi kwa malengo Ni Namna Bora ya kujipangilia, pia inasaidia kile unachokipata (income) kuelekezwa kule ambako umekusudia !
Sahihi kabisa kiongozi... Kama huwezi kuishi kwa malengo kiukweli ni sawa na Msafiri ambaye hajui anaelekea wapi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…