Malezi magumu ya utotoni ndiyo yaliyonijenga kuwa mtu wa kanuni na utaratibu mpaka leo

Malezi magumu ya utotoni ndiyo yaliyonijenga kuwa mtu wa kanuni na utaratibu mpaka leo

Maisha kama haya nimepitia Mkuu, na ndio maana niko stable sana. Nakumbuka mwaka 1995 nikiwa darasa la kwanza Marehemu babu alikuwa anatuamsha kwenda kulima na jembe la ng'ombe na Nilikuwa na miaka 7 tu tunaamshwa saa 10 alfajiri.

Ukirudi ile saa 5 unakula ugali na mtindi unaenda kuchunga wale ng'ombe hiyo kila weekend lazima. Kazi zingine kujifulia nguo za kawaida na kusaidia kazi zingine.

Hata nilipoanza kukaa na wazazi shule nilikua naenda kwa miguu darasa la nne 4.5 KM asubuhi, mchana narudi kula chakula cha mchana halafu narudi tena shule na jioni narudi tena kwa Mguu nakumbuka home kulikuwa kuna gari lakini hakuna kupelekwa na hupewi hata sh 50 ya kula mihogo au viazi vya kukaangaa.

TV tunaangalia movie za Baby Day Out, Home Alone, Tom & Jerry na taarifa ya habari tu. Marudio ya michezo tunaangalia Jumamosi tu.

Sekondary nayo ilikuwa ni 9KM hupewi hata hela ya kutumia hata kununuliwa baiskeli hakuna.

Kulikuwa na ratiba ya kufunga madirisha saa 12 jioni na ukifunga madirisha hakuna tena kutoka nje. 🤣

Ulikuwa ni msingi imara sana wa maisha ya baadae
Mkuu na wewe umepitia msoto sana
 
Zamani bora ingawa mimi sikukulia eneo la kuwa na shamba.. TV na vikadeti vya muvi etc vilikuwepo na kisatalaiti..

Mashuleni pia kuwa na bustani na tuta la kulima ilikuwa raha sana jijini Dar eneo zuri.. Kumwagilia, kupanda maua unapenda kwa kipande unapewa mbele au nyuma ya darasa..

kuendeleza haswa kazi za nyumbani, kuwafuatilia masomo etc ni muhimu sana

Miaka ya sasa na nyuma kidogo dunia ina mengi.. Wazazi tuwajenge watoto hongera kwa mengi yaani yote ulivyo sasa una ujuzi. Sasa imagine mtoto ambaye hajui lolote.. Hata kutandika kitanda.. Kufagia etc

Watoto bila hayo wakikaa hawasemi inawapa picha ya kukosekana upendo wa kulelewa na wazazi... Kulea ina mengi..

Hii topic nzuri sana na ina mengi...
Natamani kuandika zaidi ila nimeichokaaa.. Sita usiku sasa hivi..

Usiache wanao wakawa na uhuru bila kuwafunza pia kiaina yoyote..
Asante sana, ukipata muda njoo utupe uzoefu wako katika ukuaji wako
 
Kwenye umri wa utoto kati ya miaka 7 hadi 14 ndiyo umri wa kukopi kwa yale mtoto anayoyaona na anayofanyiwa , ndio maana mtoto yeyote akifanyiwa jambo baya au zuri kwa muda huo litakuwa kumbukumbu maisha yake yote au linaweza kumuaffect kisaikolojia. mfano kwa watoto waliofanyiwa ukatili kwa umri huo huwa hawawezi kusahau na inabaki kumbukumbu mbaya maishani mwao.

Licha ya msemo wa huruma sio malezi ibaki kwa wazazi kuwafunza watoto wao misingi ya maisha itakayo msaidia kuishi ukubwani.
Uko sahihi mkuu, matukio yote haya ni kabla sijafika 15 years
Mpigie simu msumulie uliyotuambia, mpe furaha ya malezi na shukurani upokee baraka tele zaidi. Hiyo umeandika hapa naamini unapona zaidi juu ya mawasiliano nae. Mpigie mpige story apate furaha ajivunie

Leta mrejesho, hata akisema umemkumbuka.. Hili na lile or kulalamika ignore maana labda, anaumia unaongea zaidi na Mama yako kuliko yeye.. Mwambie umemumisi sana.. Na unampenda

Mpe furaha, cheka furahia nae..
Mola asimamie
Naweza kusema nimefurahia upendo wa mzee wangu nikiwa tayar mkubwa , sahv tumekua karibu na huwa ananipigia mara kwa mara akitaka kujua maendeleo yangu na huwa ananishauri sana niendelee kusali na kumtanguliza Mungu kwenye kila hatua ya maisha
 
Yanafaa sana Tena sana uhuru umezid Kwa watoto wa kipindi hiki hawana nidham
Nadhan unaona huko mtaan kwako namna wazaz wa kileo wanavolea watoto wao ndo maana watoto wengi wameharibika sababu ni MALEZ mtu atakuja kusema kulea Kwa ukali ni ukatili je Hawa watoto wa Sasa mnawaonaje?

Nimepita humo Kwa mzaz mkoloni na mkali haswaa ila Leo nimeelewa kwanin alifanya vile nataman kizaz changu kiwe chenye malez niliyopitia sio Lele mama na uhuru uliopitiliza tunajionea mengi Kwa hichi kizaz mpaka mtu unaogopa uzao unaokuja utakuaje kma watoto ndo hawa.
Acheni kulea watoto kisasa kusema kwamba mnawapa uhuru watoto hawana adabu,utiifu,nidham watoto hawana uoga Kila kitu kwao ni sawa hayo sio malezi unalea bomu litakalokuja kukulipukia
Hii generation ya sasa imekosa Self discipline, sababu wazazi wame relax mnoo,
 
Mimi niwape pongez wote mliolelewa na baba zenu tena kwa uwajibikaji

Binafs nikir wazaz wangu walinitelekeza kwa bibi tena sio bibi n bibi yake mama sijui mm nimuiteje imagine alikuwa na umri wa miaka 65 wakat huo mm 5yrs je unadhan angeweza kuyasimamia hayo mliyoyasema hapo juu lakn namshukuru nilijitambua toka nikiwa mdogo sina msaada lazma nipambane mwenyewe ili bibi ale na mm nipate mahtaj ya shule

Kiufup mm nilikuwa jeshi la mtu mmoja yaan mm n baba mama na mlez pia

Nimeanza kulima.mahind nikiwa na 9yrs na nikivuna nauza naweka akiba mengne kwa chakula na pesa natunza

Uhuru ulikuwa mkubwa sana kwangu hakuna wa kunizuia nyumban

MUNGU alibless class nilikuwa vizur sana baada ya kumaliza std 7 nilipangiwa bwen mkoa x lakn nilipambana kupata uhamisho kurid shule jiran na home ili kumlea bibi kiukwel alikuwa kikongwe sana
Nikiwa form 3 bibi alifarik na imagine hapo ndio nilimjua baba na mama kwa mara ya kwanza

SINA MENGI YA KUSEMA ILA WAZAZI WANAOTUNZA WATOTO WAO KWA TARATIBU NA KANUNI HONGERENI SANA
leo nipo jiji la chalamila nam na watoto nahakikisha kila hatua nipo nao na namshukuru wananisikiliza sana huwa nawasilimulia nilipotoka
Mkuu hongera sana kwa kuweza kujisimamia mwenyewe mpaka hapo ulipo sasa
 
Wazazi wengi waliishi katika era ya ukoloni na era za siasa za ujamaa , kwakuwa hizo ndio zilikuwa sera za Nchi nyingi za Africa Kwa wakati ule na wao walipitia kwenye kuburuzwa na hizo sera basi waliathirika Kwa kupokea malezi ya ukatili wakiwa wana amini kwamba huo ndio mfumo sahihi wa kumshape mtu katika maisha Kwa upande mwingine walikuwa sahihi lakini Kwa upande mwingine pia hawakuwa sahihi

Nitafafanua Kwa Nini walikuwa sahihi === walikuwa sahihi katika nyakati zile kwasababu Sehemu kubwa ya jamii zetu hazikuwa zimestaarabika miaka ya 80 na late 90 ilikuwa ni miaka ambayo Kuna Uvunjifu mwingi sana wa sheria mifumo mingi sana ya kiserikali haikuwa Committed nakumbuka ilikuwa ni kawaida sana kuona makundi ya wahuni wakipigana hovyo mitaani kuporana wanawake kupigana mpaka na visu mapanga etc Uhuni ulikuwa Kwa kiwango kikubwa sana vijana wengi wa wakati huo story zao zilikuwa ni kuzamia meli tu kwenda Kwa Madiba etc so kwa Aina hiyo ya jamii iliyopo kama una watoto ukiwalea kilele mama nilazima watageuka kuwa Chakula ya watu wengine 😄😄 haswaa wakiwa ni wanaume , Watoto wa kizazi kile ili waweze kusurvive walipaswa kuwa though Tena ile ngangari kisawa sawa haukupaswa kuwa lelemama kabisa

Na kama wangeweza kulegezewa kimalezi ingekuwa ni rahisi Kwa wao kuweza kuingia kwenye makundi ya hovyo na kuwa vibaka Malaya sugu wezi etc mwisho wa siku unajikuta unampoteza mtoto , so Kwa wakati ule malezi ya namna ile yalikuwa ni sahihi Kwa kiwango Cha Asilimia Fulani

Na kwanini hayakuwa sahihi == Kwa sababu Kwa baadhi ya watu ambao walikuwa ni watoto Kwa nyakati zile baadhi Yao (wengi) wameathirika kisaikolojia na kupoteza bond na wazazi wao Kwa kuwaona wazazi wao ni wakatili sio wazazi marafiki hii Inaweza kuchangia Kwa mtoto kuweza kupoteza mapenzi na wazazi wake tufahamu kwamba mtoto nayeye pia Huwa anafikiria licha ya kuwa katika utoto wake , kwa mtoto inaweza kutokea akapatwa na janga zito like kubakwa lakini akaogopa kuja kusema Kwa wazazi wake kwakuwa tu ataogopa kwamba ataashibiwa adhabu Kali mwisho wa siku anaamua kubaki na Siri yake alidhania kwamba anafanya jambo sahihi kumbe ndio anazidi kuharibikiwa Kwasababu anakuwa anakaribisha uadui kwake Pasipo kujua kwamba endapo ange wataarifu wazazi mapema angeweza kupata msaada wa haraka,

Hivyo hivyo mtoto anaweza kupatwa na balaa zito la namna yoyote lile lakini akaona ni Bora kukaa kimya kwasababu anajua akienda kureport nyumbani ataishia kupata kipigo kikali Cha mbwa Koko badala ya kusikilizwa na kutafutiwa ufumbuzi wa tatizo lake na ukweli ni kwamba wazazi wa type hizo wapo , .


So mzazi unaweza kujikuta unapoteza bond na mtoto + mapenzi Kwa sababu tu ya Ukali uliopitiliza katika nyumba Yako ,


Wazazi tunapaswa kuwa neutral 🙏🥰
 
Kiufupi mwanetu umelelewa kijeshi sana,

Ukilelewa kijeshi mara nyingi watu wa aina hiyo wnaakuwa na nidhamu ya hali ya juu sana lakini linapokuja swala la kuvunjiwa heshima basi hapo ndipo utaona vita ya watu hao.

Naweza kusema hongera kwa baba yako maana hatuwezi wote kulelewa kwa malezi ya aina moja.

Aina ya malezi ambayo umepata,ndiyo yamekufanya kuwa mtu wa sasa,je unahisi umepata maana ya maisha kwa malezi yale amekupa baba yako???
 
Pongezi kubwa ziende kwa mzee wangu, hivi sasa ndo naona matunda yake, just imagine nimebalehe ila mzee anakwambia saa12 jioni uwe ndani .

Na alikuwa ana vitu viwili tu kama hauna usingizi soma na kama umechoka kusoma lala kingine mzee wangu alikuwa anapiga viboko mpaka akili inakaa sawa yani ni wale wazee wajeshi jeshi ila leo hii mzee wangu ndo mshkaji wangu mkubwa na niikiwa busy huwa ananitafuta kujua naendeleaje
 
Alikuwa sahihi kwa baadhi ya mambo na mengine hakuwa sahihi,haikuwa sawa kuwatembeza usiku kucha kutafuta kitoto cha mbuzi kisha aje awapige tena,lazima ajue kuna umri ambao bado utoto ni mwingi.

Haikuwa sahihi mtoto wa miaka 7 kumpa shamba kubwa alime,hapo alipita mipaka

Kwa mambo mengine alikuwa sahihi kuwajenga kinidhamu

Wazazi wapya kabla hamjapata watoto muombeni Mungu awape watoto wema,msaada wa Mungu ni muhimu sana,atakupa watoto wasikivu na wema
 
Kwa mawazo yangu malezi ya aina hiyo bado yanahitajika sana. Ukichunguza vizuri ndiyo aina ya malezi ambayo yalijenga vizazi imara na bora kabisa. Ni vizazi ambavyo muundo wa maisha ulikua programmed kwenye muelekeo mzuri wa maadili, tabia hata uchapakazi. Ila naona ulikua na changamoto chache kama ilikua marufuku kuhoji hata mkubwa akikosea. Tofauti na sasahivi malezi yamebadilika sana
 
Mimi niwape pongez wote mliolelewa na baba zenu tena kwa uwajibikaji

Binafs nikir wazaz wangu walinitelekeza kwa bibi tena sio bibi n bibi yake mama sijui mm nimuiteje imagine alikuwa na umri wa miaka 65 wakat huo mm 5yrs je unadhan angeweza kuyasimamia hayo mliyoyasema hapo juu lakn namshukuru nilijitambua toka nikiwa mdogo sina msaada lazma nipambane mwenyewe ili bibi ale na mm nipate mahtaj ya shule

Kiufup mm nilikuwa jeshi la mtu mmoja yaan mm n baba mama na mlez pia

Nimeanza kulima.mahind nikiwa na 9yrs na nikivuna nauza naweka akiba mengne kwa chakula na pesa natunza

Uhuru ulikuwa mkubwa sana kwangu hakuna wa kunizuia nyumban

MUNGU alibless class nilikuwa vizur sana baada ya kumaliza std 7 nilipangiwa bwen mkoa x lakn nilipambana kupata uhamisho kurid shule jiran na home ili kumlea bibi kiukwel alikuwa kikongwe sana
Nikiwa form 3 bibi alifarik na imagine hapo ndio nilimjua baba na mama kwa mara ya kwanza

SINA MENGI YA KUSEMA ILA WAZAZI WANAOTUNZA WATOTO WAO KWA TARATIBU NA KANUNI HONGERENI SANA
leo nipo jiji la chalamila nam na watoto nahakikisha kila hatua nipo nao na namshukuru wananisikiliza sana huwa nawasilimulia nilipotoka
Pole sana comrade
 
Mimi nimekulia kota mzee alikuaga engineer mambo ya electricity.... almost maisha yote primary school tuli ishi kota baadae mzee akajenga ndipo tuka hama...ntatoa SIMULIZI za kusisimua na kushangaza sanaa...

Kuna wazazi walikua wanataka watoto wao wafuate nyayo zao wanasahau Kila binadamu ana FREE WILL mtoto ana passion ya kitu Fulani mzazi analazimisha mtoto awe scientist

Kuna watu walikua wanachungwa yaani ratiba ngumu ngumuu sanaa WAZAE WAKOLONI KINOMA NOMA... Ndio ivoo na wali alibikiwa

Na mengi ya kusisimua na kusimulia..

Juzi nilikumbuka mambo mengi SANA SANA ya udogoni mwangu na malezi yangu ntasimulia yoteee ngoja nipate nafasi

Kuna mengi ya kujifunza abadanii
 
Back
Top Bottom