Ertugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 14,705
- 30,041
Nakubaliana na wewe huenda ni DNA, binafsi sikuwa mkaidi au mwenye tabia za ajabuSio kweli, kwa mfano vitoto vya kizungu mbona vinakuaga good behave na civilized yaan hii issue itakua ipo kwenye DNA..
Katoto ka ki afrika mpaka bakora ndio kana elewa yaani ni noma ila Mimi tangu udogoni mwangu sikuaga mtundu , ni msikivu sana pia vitu vya ovyo ovyo sijafanyaga kwa kwelii
Nina wanangu sijawahi kuwachapa hata siku moja,na wasikivu sana,unamuelekza jambo fulani mnaenda sawa,na maombi ya kuomba watoto wema yanasaidia sana
Binafsi siamini kuwa mkali ndio kumfundisha mtoto,sana sana unawafanya wasijiamini na hata ukaribu na wewe unakuwa haupo,kuna familia baba akiingilia mlango huu watoto wanachomokea mlango huu,haya ndio malezi gani?
Matokeo yake uzeeni unasema watoto wanampenda mama yao kuliko mimi,kumbe mwenyewe umetengeneza distance toka zamani,mfano mtoa mada kaambiwa akiwa hana jambo la msingi asimpigie baba yake simu,leo hii anampigia zaidi mama,je baba akililalamika kuwa mwanangu hanikumbuki itakuwa sawa? Amesahau hapo awali alishasema usinipigie simu bila sababu ya msingi