Mama amshauri mwanaye kuacha kazi kisa ndoa

kwani Huko alikoenda amekwambia hatafanya kazi yoyote? Maisha Sio kukariri. Fursa ziko.nyingi ukichangamsha fuvu.
 
Kiinglish logical or logically?
 
Mbona unaumia hivyo mke kumfuata mme wake? Ulikua unafukuzia?

Mama na mtoto wake wote wako sahihi asilimia zote.
 
Mkuu maisha na uchumi wa Norway huwezi kuyafananisha na maisha ya mchongo ya bongo. Huyu mama kampoteza mwanaye kwa kumshawishi kuacha kazi kwa ajili ya kutumikia m.boo. Hii ni mbaya sana.
Mafunzo ya ndoa yanasema, mume na mke ni mwili mmoja, njaa zetu zisitufanye kuwa watumwa tukavunja ndoa zetu. Bora uridhike na shilingi 10 kukiwa na utulivu ndani ya ndoa, kuliko kuwa na mamilioni na migogoro ya ndoa pamoja na maradhi.
Pia kuajiriwa wote ni utovu wa nidhamu kwa nini wasijiajiri? Pia hakuna tajiri aliyeajiriwa.​
 
Mtoa mada huyo mwanamke ni nani kwako mbona unaonekana umekwazika sana katika jambo lisilokuhusu? Ndoa ni ya wawili na wanamakubaliano iweje wewe uumie kiasi hicho??
 
Mtoa mada alitegemea supports,ila amejikuta kabanwa mbavu!halafu kumbe mleta mada ni kataa ndoa na age bado ya kitoto
 

Hofu ya vitu kama hivi kutokea

 
Kama familia yote inajiweza kwanini asiache kazi na kumfuata mumewe?.

Umasikini ndio chanzo wanawake kuwa watafutaji.
Muwe mnafikiria na mambo menginè. Maisha huwa yanabadilika, kuna kuachishwa kazi, biashara kuyumba, magonjwa,kifo, mke kuachwa ataenda wapi.
Muache ubinafsi wakati mwingine.
 
Mchawi ni wewe unaefuatilia maisha ya watu kwa kiwango cha lami na kuja kuwabeza JF
 
Kuacha kazi kunaweza kuwa chachu ya maendeleo na afya njema. Yumkini kazini kuna madhila mengi ambayo hayavumiliki. Utumwa uliofundishwa katika vitabu vya historia unafanywa makazini na viongozi wasio na utu na wanaojivisha ufedhuli na wasiojali utaalam na umuhim wa mtu. Kumfuata mume/mke ni kigezo cha uhamisho kwani uhai wa taifa lolote huanzia kwenye familia imara.
Pili, hii ni kwa wafanyakazi wote ikiwa alifanya kazi kwa ujuzi, anaweza kuibadili akili ileile na kufanya makubwa katika sehemu aliyopo. Fursa inatembea na mtu. Asiogope watu wanamuonaje.
 
We jamaa unaona kazi ndio kila kitu kwenye maisha yako

Pole sana
Sasa wewe mkuu unaona ndoa ni kitu cha kuchukulia umuhimu kiasi hicho? Ndo si ni utapeli tu?
 
Mkuu umemaliza kila kitu. Naomba nikutunuku PhD ya heshima Dokta Nifah .
 
Kumtunza mwanamke ni wajibu wa mwanamme.

Ni umasikini tu kwa mwanamke kufanya kazi kama mwanaume,yeye ni pambo la nyumba wakati wote anatakiwa awepo nyumbani.

Hana haja ya kufanya kazi.

Mama yupo sahihi.
 
Hapo ilitakiwa maamuzi ya busara sana kwa sababu mama ameona ndoa ni bora kuliko kazi, lkn swali je mume akifa ?

Je wakitalikiana?

, bint baada ya kushauliwa vile angeomba ushauli kwa ndugu wengine hasa kaka zake na angemshiliksha mumewe,

Hapo jamaa walitaka pesa,

Ndio maana huwa ninaambia vija wangu sio kila ushauli wa mzazi wa kuusikiliza unatakiwa utumie akili zako
 
Kama wanaishi vizur we unaumia nini? Au ndo ulikuwa mchepuko wake. A ndo ulikwamisha uhamisho?

Kazi zipo na yalianza Maisha kabla ya kazi

Familia ni bora kuliko mali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…