KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Niseme kwa ufupi tu mkuu Phillemon Mikael,Dr John Pombe Magufuli hakua wa kufa leo wala kesho ; tatizo kubwa ni ile hali aliyoiweka na washauri wake kushindwa kuhakikisha Daktari wa Rais anakuwa na msimamo...
Tunao madaktari wazuri sana ndani ya nchi hii, tena wengi wao ni waliohitimu hapahapa nyumbani na kuendelea kufanya kazi kwenye mazingira ya ukosefu wa vifaa vya kuionyesha dhahiri umahiri wao.
Wapo wazuri kabisa, kama ilivyo katika nyanja zingine kote hapa nchini.
Tatizo kubwa sana, na kwa bahati mbaya, limekuwa ni siasa kuwa kila kitu.
Ukichunguza vizuri, utaona wakati wote wa uwepo wa Magufuli kwenye utawala, siasa ndiyo ilikuwa sauti ya mwisho kwa kila kitu.
Ukichanganya na kiburi chake, hata hao madaktari waliokuwa wamemzunguka wakawa ni wa kupima upepo wake unavuma kuelekea wapi.
Hebu fikiria haya mambo ya kujifukiza dhidi ya corona - Muhimbili na Mloganzila zikalazimika kuweka Sauna Spa, kila moja yenye gharama siyo chini ya milioni saba!
Ni daktari gani aliyethibitisha kwamba sauna inatibu corona?
Naungana nawe moja kwa moja kusema kwamba Magufuli kwa hali ya kawaida ya ugonjwa wake unaofahamika, hakuwa mtu wa kufa wakati huu.
Lakini unaona jinsi wanavyoendelea kuvungavunga na kuhadaa watu kwa kupindisha ukweli?
Sijui wanaendelea kufanya ujinga huu kwa manufaa ya nani hasa. Mtu aliyeshupalia jambo lenyewe hayupo tena. Wangetumia nfasi hii kuwahimiza wananchi kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa huu.
Badala yake, wao wanaendelea kueneza ujinga.
Nililotaka kuanza nalo katika kujibu bandiko lako ni hili: Tanzania haiko mbali sana na jina la "Banana Republic."
Tunapodharau kutofuata taratibu; tukawa watu wa kujipigia tu bila mpangilio maalum, hali hiyo ni vurugu tupu.
Hili ninalolisema hapa unaweza kuliona hata katika mpangilio mzima wa maombolezi haya tuliyonayo sasa hivi.
Ni hali ya kuogopesha sana inayoweza kulikabili taifa. Omba sana tusikabiliwe na janga kubwa zaidi ya huu msiba tulioupata kabla hatujaanza tena kuwa watu wenye kufuata taratibu maalum katika utendaji wetu.