Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Maombi yangu siku zote ilikua mama asiingie mkenge wa wafanya biashara maana tunajua kitakachotokea.
Bahati mbaya mama ameuvaa mkenge wa wafanya biashara. Tusitegemee chochote cha maana kufanyika kwa miaka 4 ijayo. Mama mwenyewe amekiri kua kwa kauli yake makusanyo yatashuka, unajiuliza kwa nini yashuke?
Mama ana matumaini kua makusanyo yakishuka baada ya muda yatapanda, yatapandaje? Nini kitayapandisha?
Ukiona kiongozi hayuko firm and strong kwenye kodi, basi ujue hiyo nchi iko doomed to fail. Nashukuru hayati alikua wazi kwenye hilo, alikua wazi na firm kwenye hilo
Kodi ni jambo ambalo halihitaji kubembelezana, hakuna mfanyabiashara anaetaka kulipa kodi, awe tajiri mkubwa awe mdogo hakuna. Kipindi kile Magufuli anaingia kina Azam walikutwa wanakwepa kodi ya kutosha,itakuaje kwa wafanya biashara wadogo na wa kati? Hilo liko wazi kodi ni jambo ambalo hakuna mfanya biashara anataka kulisikia.
Hakuna mfanyabiashara atakaelalamika ikiwa mfumo wa kukusanya kodi ni dhaifu, hayupo. Maana mifumo dhaifu ya kukusanya kodi ni faida kwa wafanya biashara.
Siku zote wafanya biashara hawako tayari kulipa kodi kwani itawapunguzia mapato yao.
Hizo nchi za ulaya hawabembelezani kwenye kodi na kila mwananchi anajaza tax returns awe na kazi awe hana kazi. Nchi zote zilizoendelea hawana cha msalia mtume kwenye kodi.
Sisi tunabembelezana kuhusu kulipa kodi halafu tunaenda kuomba msaada na mikopo kwa watu ambao hawabembelezani kwenye kodi, hizi ni akili ama matope?
Tanzania nchi yenye watu 60m inaenda kuomba msaada Finland nchi yenye watu 5m wakazi wa Dar tu wanazidi wananchi wa Finland, ama Norway 5m ama Sweden 10m, hii ni akili kweli? Na sababu no moja tu, Finland kila mtu analipa kodi na hakuna kubembelezana na ukikwepa kulipa kodi unafilisiwa kabisa.
Mama ameanza kupenda cheap popularity, ameanza kucheka na nyani atavuna tu mabua.
Acha upotoshaji wa kijinga, usidhani hatujasikia alichosema huyo mama. Mama kasema hataki kodi ya dhuluma bali anataka kodi halali. Kinachokufanya upoteshe ni ili ufiche ukweli aliosema kuwa watu walikuwa wanabambikiwa kodi, na hilo limefanyika sana, na kasema kabisa kubambikia kodi kuna faida ya muda mfupi, lakini hiyo inaua biashara za watu. Kama ni kushuka kwa muda ni hayo mapato ya kubambikia na sio mapato halali. Na kwa approach yake kodi ya halali itapanda kwani biashara nyingi zitaamka na kuanza tena.