Mama Samia ameingia kwenye mtego wa wafanyabiashara kubembelezwa kulipa kodi, tumekwisha!

Mtoa mada anzisha biashara ili nawe ubembelezwe
Sekta binafsi ndio mlipa kodi namba moja kwa serikali yetu , handle it with care ,
 
Maendeleo gani unayosemea ya wazi wazi ? Hiyo Atcl yenye kutupa hasara ya 60 bil kila mwaka? Au chato airport?
 
Mlichofanikiwa kuuaminisha imma ni kuwa , kila mtu anayeilalamikia serikali ni mhujumu uchumi au mpiga dili
Bei ya mbaazi ilifika 2300 kwa kilo mwaka 2016 mmemsumbua manji , sasa mbaazi hazina tena soko. ukiuza 300 kwa kilo una bahati.
Halafu kukwepa kodi kwa tech ya sasa ni ngumu sana, efd zina record karibu kila kitu na ni ngumu kutotoa receipt na ukasurvive . Mtu akizungunzia mambo ya kukwepa kodi au kupiga Tax deals kwa sasa naona kama sio mfanyabiashara wa kweli.
 
Kodi sio sababu ya kwanza ya kukimbiza wafanyabiashara. Hii ni hoja ya watu wajinga ambao hawakwenda shule.

Huko ulaya kuna very strict laws za kodi, umeona kama wafanyabiashara wanakimbia ulaya?
Mkuu
Unalinganisha mazingira ya kodi za ulaya na nchi zinazoendelea ?
Unafahamu kwa nini tunatumia mitumba huku kuanzia nguo magari hadi mitambo? Ni kwamba hii mitumba inakuwa subjected kwenye makodi makubwa huko ndo maan a wao huamua kutupia afrika,
Sasa tunatumia products za mitumba katika uzalishaji wako halafu unataja utumie sheria za kodi za ulaya , lazima ufeli
Vat threshold Tanzania ni mil 100, uk vat threshold ni pound 85000 , karibu milioni 273 , maana rahisi ni kuwa TRA inasajili wafanya biashara Vat wakiwa bado wachanga kabisa ndo maana kila siku ni kukimbizana na kesi za Vat.
 
Tunamuomba Mama apunguze VAT ili ilipike kwa urahisi aifanye hata 6% au even lower

Tunamuomba Mama apunguze Utitiri wa Kodi na matozo ya mateso
Mkuu
Vat yenyewe watu wanaingizwa kibabe , kwetu unasajiliwa vat ukifika turnover ya milioni 100 , uk ni milioni 273 approximately, south africa ni wastani wa 159 milion
 
Hii njemba inaonekana ni kwepa kodi iliyopewa mbinyo.....
Hata biashara sidhani kama anafanya , hawa ni praise team wa the late , na waliamini kila kitu alichosema.

Hawa hata wangemkuta shambani anapanda mahindi yaliyokaangwa , bado wangeamini yangeota!
 
Uongo wa mchana.
Mliozoea kulipwa vihela kutokana na dhuluma sasa mnaona vyanzo vitakauka.
Anzisha na wewe biashara yako ili ulipe kodi kuokoa nchi.
 
Mtu ana Tax clearance , unawezaje kumkadiria upya kwa miaka mitano au kumi nyuma ,? Ulikuwa wapi na kuwa nini ulimpa Tax clearance ?
mahakama zingekuwa huru haya mambo yasingetokea
 
Mapato yakishuka, yameshuka. Tuna miradi kibao ya kimkakati tunayoifanya kwa pesa zetu za ndani ambazo ni kodi. Sasa badala ya kukaza hapo hapo, huku tukibuni vyanzo vipya sie twatepeta. Mpango alisema anataka TRA wakusanye trillion 2,itashuka mpaka 800Bil maana hiyo 1 trillion tulipo tra walijitahidi kwa mateke na magumi. Hatua kumi mbele, hatua thelathini nyuma.
 
Binafsi naona mama angepunguza speed, wafanyabiashara siyo watu wamchezomchezo mbele ya pesa. Pia kuagiza kesi zisizo na ushahidi au ushahidi hafifu zifutwe, watu watazifuta kweli na zisizo stahili kufutwa.
 
Atavuna mabua kweli kweli.Lakini tangu lini watu wa pwani walio wengi wakawa serious on serious issues?Hapa tumeliwa.CCM mpo?Mtatuuza tena kwa mabeberu kama mlivyo tuuza enzi za akina Mkapa na Kikwete?
 
Huyu mama ni dhaifu sana, na ameshajikaanga kwa mafuta yake mwenyewe, ngoja acheke na nyani alafu aje avune mabua, lakini muda utasema ngoja tumzoom.
 
Binafsi naona mama angepunguza speed, wafanyabiashara siyo watu wamchezomchezo mbele ya pesa. Pia kuagiza kesi zisizo na ushahidi au ushahidi hafifu zifutwe, watu watazifuta kweli na zisizo stahili kufutwa.
TRA waje nyumbani kwako kukusanya kodi.
Wakunyang'ang'anye kama wanavyofanya kwa wafanyabiasara.
 
Binafsi naona mama angepunguza speed, wafanyabiashara siyo watu wamchezomchezo mbele ya pesa. Pia kuagiza kesi zisizo na ushahidi au ushahidi hafifu zifutwe, watu watazifuta kweli na zisizo stahili kufutwa.
Yaani huyu mama aisee,sijui hajui athari za anayoyafanya?Yaani inafikirisha sana.Huyu ndiye tuliyeaminishwa kwamba amekaa chini ya Magufuli kwa hiyo kaiva.CCM do something and fast vinginevyo we are sliding towards Kikwete era.Utawachekeaje mabeberu,wafanyabiashara na mafisadi?
 
1.) Unaonaje na wewe ukaanzisha biashara, dumu nayo hata kwa miaka miwili 2, halafu rudi usome tena huu uzi wako.

2.) Leo mnakiri kuwa idadi ya watu ni rasilimali, sasa kwanini mnabeza wanaopinga uzaziwa mpango?
 
TRA wamefanya makosa makubwa kuanzia 2015 kuelekea 2020 lazima tuwe wakweli. Lengo la kumpa mambo ya nje Mama Mulamula ni kujenga picha ya kimataifa kwamba tupo na nyinyi, na sisi ni sehemu ya dunia yenye mahitaji yanayobadilika.

Huwezi kuwa na mabadiliko ya kimtazamo kimataifa halafu usiwe na mabadiliko ya kimtazamo katika masuala ya kodi ambayo yanao uhusiano na nchi kutazamwa kidunia.

Naamini mabadiliko yanayokwenda kufanyika katika muelekeo ya masuala ya kodi hautaumiza pande mbili kwa maana ya serikali na jamii ya wafanyabiashara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…