Kuna jambo linanichanganya. Tunashuhudia mama mwenye watoto zaidi ya umri wa miaka 30 anafanyiwa sherehe ya kutolewa mahari, kwa mbwembwe kubwa, akiwa kama binti wa kwanza. Lakini cha kushangaza, anayemposa si baba wa hata mmoja wa hao watoto.
Shughuli ni ya moto! watu mtaa mzima wanajua, watoto wa huyo mama wapowakubwa kwa wadogo..
Je, huu ni uthibitisho wa uhuru wa mwanamke kuanza ukurasa mpya wa maisha? Au ni ishara ya kutafuta kuthibitishwa kijamii bila kujali athari za kisaikolojia kwa watoto?
Tumeingia kwenye enzi ambapo "mradi apate mume" imekuwa kauli maarufu, lakini je, namna tunavyotafuta hiyo ndoa inatoa mfano gani kwa watoto wetu na jamii?
Naomba tujadili kwa heshima:
- Je, ni sahihi kutolewa mahari kama binti wa kwanza ukishakuwa mama wa watoto wengi?
- Watoto wanajifunza nini kupitia haya?
- Hii ni haki ya mwanamke au ni presha ya mitandao?