Mama yangu mzazi aliwahi kuniambia bora nife tu apumzike

Hatariiii
 
Mkuu jimama lilikupurusa ada[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
CHAPTER 11

daaah hatari katika lile eneo tulikutana na mauza uza ya ushirikina na uchawi hatari. pale wakati tunachimba kuna mda tunasikia kama sauti za watu hivi wanakuja kwahiyo fast sana tunatoka tunaenda kujificha alafu ukichungulia hakuna watu wala nini.

mukienda tena kinatokea kituko kingine mara musikie kama mwanamke analia hivi yani sauti fulani hivi kama mwanamke kapigwa alafu analia.

yani tulichimba kidogo tu tukaona hapa pazito tuondoke haraka sana.

Tuliondoka lakini mipango yetu tukae siku kadhaa turudi tena kule kijiji kujaribu bahati yetu kwa round ya pili.

Daaah hii round ya pili ndo ilikuwa ngumu zaidi kuliko ile ya kwanza.

INAENDELEAAAA...

Tulifika mpaka mjini hapo mimi nawaza madini tu lakini kiupande mwengine naona kama fix.com hivi.

na vituko vya kule shimoni ndo nikawa sipati majibu kabisa. tukakaa mjini kama week mbili hivi sasa tukaamua kurudi tena mimi ostadh na mjomba. round hii tulisema lazima turudi na madini.


tukatoka zetu Dar es salaam. mpaka mkoa x safar yetu mda ni ule ule kule kwenye shimo mpaka stand ya mjini ni mwendo wa masaa minne kwa miguu.

tofauti ya round hii na round ya kwanza round hii tulianza kusoma dua tukiwa tupo huku huku Dar es salaam. tukapanga tukifika tena tunasoma dua then kazi inaanza fast fast.

lakini pia round hii hatutorudi stand kuna sehemu tutaenda ni kijiji cha pili jirani kuna mtu mjomba anajuana nae tutaenda kulala hapo mpaka asubuhi. ikifika asubuhi tutaanza safari yetu sasa ya kurudi mjini.

lengo la kwenda kulala kijiji jirani na sio porini ni kuwa tusikutwe na raia wa kijiji pale asubuhi. maana lile eneo limepigwa marufuku kuchimbwa.

kwahiyo tukapiga mguu mpaka kijijini pale shimoni tukakata miti kwa ajli ya mipini kama kawaida. dua zikaanza pale ostadh kama kawaida yake dua dua mwisho wa siku akazima ikabidi sasa mimi na mjomba tuiingie shimoni.

jamani kupata utajiri ni kazi ngumu sana na ukisikia kuna utajiri unapatikana kiurahisi rahisi tu basi unatakiwa ujifikilie mara mbili sheria ya pesa siku zote kila inavyozidi kuwa nyingi na maumivi yake pia yanakuwa makubwa.

piga sululu piga jembe piga sululu piga jembe hiyo mida ya saa 5 usiku inakimbilia saa 6 vituko vikaanza mara tusikie sauti za mtoto mchanga mara mwanamke analia kama ana kwikwi hivi.

tunatoka shimoni tunatazama huyo mwanamke na mtoto wako wapi sasa alafu tukitazama kweupe hakuna kitu wala nini.

tunaingia tena shimoni tunafanya kazi kidogo tu.vituko vinaanza upya mara tusikie sauti kama watu wanakuja hivi tukichomoka shimoni hakuna mtu anae kuja wala nini kiufupi usiku ule siwezi kuusahau katika maisha yangu mpaka kifo changu.

inafika mida ya saa 9 usiku tukamuasha ostadh tusepe. akatuuliza mumepata chochote jibu la mjomba " hatujapata kitu kama tulivyokuja ndo tunavyoondoka "

ostadh alitikisa kichwa akasema " hapa pazito sana sijui kama kafara lake haijavuja damu ya binadamu"

mjomba akauliza " kafara la binadamu kivipi"

ostadh akajibu " inawezekana kana hapa haliuliwa binadamu ili kulinda hizi mali zilizopo hapa yani hapa inawezekana munafanya kazi lakini munafumbwa macho nyie mwenyewe hamujui munachokifanya"

mjomba na ostadh waliongea ongea sana dakika ya mwisho ikabidi tusepe tu. sasa njiani wakati tunatembea kuna mda tukamuona ostadh kama kasimama hivi alafu akatuambia tupiteni njia za maporini huku barabarani leo inaonekana pazito sana.

aaah sisi hatukuweza kumpinga. tembea tembea ostadh akasema " munajua kwanini tumewaambia tupite njia za porini"

tukamjibu " tujui kwanini"

hakasema hamuwezi kuamini nimemuona mtu analoga yupo uchi wa mnyama". ostadh mda uo anaongea maneno hayo lakini anatetemeka yani hayupo katika hali ya kawaida kabisa.

yani anatetemeka kama mtu ambae kakamatwa na baridi kweli kweli. anatetemeka mpaka meno ya juu na ya chini yanagong'ana.

"mjomba akasema " sikia ali wewe beba begi la vifaa , mimi nambeba ostadh nadhani hayuko sawa hapa bado hatua kidogo tufike kijiji tunachoenda "

nikamwambia mjomba " sawa lakini si bora tujikaze twende na ostadh mjini maana huko tunapoenda kijiji cha pili hakuna hospital wala nini "

jibu halonipa mjomba " aya mambo mengine hayaitaji hospital ukimchoma mgonjwa sindano tu ndo ushamuua mazima mambo ya Kiswahili yanamalizwa kiswahili swahili tu"...

ostadh hali yake ilikuwa haieleweki kabisa kuna mda anakuwa sawa kuna mda anaanza kutetemeka mpaka tunafika iko kijiji tukichokuwa tunaenda. imeshafika saa 10 usiku.

kuna nyumba flani hivi ya udongo mjomba akaenda kupiga hodi mda uo mimi nimekaa pembeni nasoma mchezo tu.

baada ya kupiga hodi kama tatu hivi akatoka jamaa na kibukita kashika tochi mkononi na panga alivyomuona tu mjomba aaakacheka sana nadhani yule mtu alikuwa anajuana na mjomba baada ya yule jamaa kucheka mjomba nae akacheka waliongea ongea sana dakika ya mwisho akamueleza kuwa tupo na mgonjwa mwenzetu hayupo sawa tunahitaji msaada wake.

yule mtu akaja akamtazama ostadh akasema huyu kwa hali ilivyo tumpeleke KWA KOMBO ( sio jina halisi la muhusika ). huyo kombo ni mganga wa kienyeji mda huu sasa ikawa jamaa ndo kambeba ostadh hiyo safari sasa tunamuwaisha ostadh kwa mganga.

huku tunampeleka mgonjwa lakini pia story za hapa na pale zinaendelea.

nikamuuliza " mjomba ushawahi kusikia story ya yule mganga aliyejinyonga baada ya kutapeliwa "

mjomba alicheka sana akasema " acha hizo mada sasa hivi sio mda wa kuongea hizo mada zako"

mguu kwa mguu mpaka kwa mganga tukamkuta mganga yupo macho anafanya tiba tiba zake kuna moto unawaka pale nje kwake lakini pia tulimkuta mwanamke nadhani yule ni mkewe nilimjua kama mkewe baada ya story story hapo mbele lakini pia tulimkuta mwanamke jimama la nguvu jeupe limekaa pale pembeni ya moto hivi.

kichwani nywele zipo wazi ana kitambaa cheusi kajifunga kama taulo kiunoni hivi lakini kifuani yupo wazi kabisa. yani kifua kinaonekana kabisa mitindi unaiona ile pale.

siku hiyo baada ya kuliona lile tukio ndo nikaamini kama uchawi upo na wanawake wanapenda ushirikina kuliko hata wanaume....


Gusa hapa kupata muendelezo 👇👇👇👇
Post in thread 'Mama yangu mzazi aliwahi kuniambia bora nife tu apumzike' Mama yangu mzazi aliwahi kuniambia bora nife tu apumzike
 
Nasikia migodini kuna mauzauzaa balaaa....!!
Ngoja niendelee kusoma!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…