Mambo 30 usiyoyajua kuhusu utapeli wa Q-Net (Network Marketing)

Mnajua sana kupamba kitu na kushawishi hii nguvu mnayotumia kumpata mtu mmoja ajiunge na qnet ungechukua matikiti ukapeleka pale kirumba sokoni ukatumia nusu ya hiyo nguvu tu kushawishi na uhakika ndani ya miaka miwili ungekuwa milionea ila kwa qnet utakoma miaka ata 40,, utakuwa masikini hivyo hivyo
 
Mantiki ya uzi wako ni nini aswa?
 
Asante kwa ushauri. But nimejitahidi sana kufupisha ingawa bado kwako ni marefu. Kujua jambo linaanza taratibu. Kama ulikua hujui kwa qnet ni ecommerce kama ebay basi leo umejua. Na si kweli kiwa unapaswa kungunishana kama mnyororo ili kununua bidhaa. Leo nitakupa kazi moja tu uifanye sasa hivi ili uelewe zaidi.


Hiyo link otakupeleka moja kwa moja alibaba. Na utakutana na muuzaji akiuza saa ya qnet. Jaribu kufanya kama unanunua then uniambie unajikuta ukiwa kwwnye mnyororo upi uliounganishwa.
Qnet hukuwa unaijua vyema leo nimekusaidia. Uje kutoa mrejesho baada ya kuinhia kwenye hiyo link.
 
Mleta mada umeshindwa kuwa mkweli na muwazi hapa.

Sote tunajua zaidi ya 99% ya watu waliojiunga Qnet hawakuwa na lengo la kununua au kuuza bidhaa za Qnet(Maana ni ghali sana, luxurious na hazina jipya) bali wanawaza na kuota ndoto za kuwa mabilionea kwa muda mfupi na njia rahisi rahisi.

Sasa unaposema Qnet ni biashara ya mtu kumiliki duka mtandao lake, unakuwa hauna mantiki kabisa.
 
Naona upo nje ya mada. Sielewi unazungumzia eneo lipi kwenye Uzi wangu kaka.
Samahani lakini.
 
Naamini hujaingia kwenye link niliyokupatia pale juu.. Punguza mwendo kidogo.. twende taratibu kaka mkubwa nia ni kueleweshana. Pia punguza kushambulia.. hoji kwa hoja.


Lete mrejesho juu ya hii link.

Nikupe na nyingine?
 
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] sipati picha hayo majibu ulowapa
 
Niwe mkweli kabisa, sijaingia kwenye hiyo link kwa sababu maelezo yako ya kunishawishi kuifuata hiyo link hayana mantiki. Hujajibu hoja zangu.

Fupisha maelezo yako na jikite kwenye mantiki tukuelewe.

Mimi nimesema haya...
1/Qnet kimsingi ni pyramide scheme
2/Sio sahihi kimantiki kuifananisha Qnet na platform zingine za kuuza na kununua bidhaa mtandaoni kama ebay, alibaba.
3/Mantiki ya kiujumla ya watu kujiunga Qnet ni ili kuvuna mabilioni kirahisi na wala sio kufanya biashara ya bidhaa za Qnet
 
Sasa ndugu yangu huna nia ya kuifunza utakuwa. Wewe unapewa utirio ujisomee unachana si utafeli? Hahahahaha
Any way kaka yangu leo sikuwa na nia ya kugusa huko kote ubao usingetosha. Ila nakuahidi next time nitakuja na mada zinazogusa hayo maeneo.
Kwa sasa emdelea kubaki na hiyo fikra hadi huo wakati utakapo fika nitaweka mada husika kwa Uzi.
Ila pitia zile link upate kuelewa kwa nini nakwambia Qnet ni Ecommerce. Next time nitagusa qnet kwenye angle nyingine
 
Hoja yako namba moja na namba tatu hazipo kwenye mada. Nitazizungumzia ziaidi siku zijazo. Vuta subra
Hoja yako namba mbili ipo kwenye mada.. nakushauri ingia kwenye link ya alibaba ili uahuhudie ukweli wa maelezo yangu. Fanya kama unanua ile bidhaa uone.
Nakushauri uwe mpole na uwe ready kupata elimu juu ya jambo jipya kabla ya kupinga. Au pinga kwa facts na sio kwa maoni yako tu kaka yangu.
 
Huku hakunifai kuna qnet hii net ina kiu ya kunasa matondoo ili wafunge mwaka uzuri
 
Sina hakika kama umesoma vyema Uzi wangu au umeon tu neno Qnet ukaaamua utirililike na wewe.. hahha
Sijaelewa upo eneo lipi kwenye Mada yangu. But
Kwa maelezo yako kuna kitu unapaswa kujifunza zaidi kinachohusu WAJASIRIAMALI ndani ya mfumo wa QNET. Hii ni mada nyingine ambayo itasaidia kwa kiasi fulani kutibu aina ya UGONJWA ulionao. But hii itakuwa next time.
Ila nikushauri tu Soma vyema UZI wangu na dadisi zaidi taarifa yangu then njoo ukiwa kwenye mstari wa mada husika. Ama la subiri next time twende sawa kwenye hayo maeneo.
Thanks
 
Unaweza kujificha kwenye kichaka cha kutoa elimu, alafu ukakuta umeharibu zaidi katika kupendezesha mada. Ukiwa na muda, naamini unao wakutosha tafakari juu ya uwezekano wako binafsi wa kumiliki hilo duka la viatu vya 100m Tshs ili utuuzie watanzania.
haya mawazo ya ajabu sijui mnapata wapi. Bahati mbaya unakutana na jamaa waliobahatika kwenda shule, mpaka unapata hasira kuona ujinga unavyokua katika taifa kila siku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…