Hahaah
umenikumbusha rafiki Qnet
Binafsi nimehudhuria kitu kinaitwa TRAINING
zaidi ya mara moja
Huwa wana ya kwanza na ya pili n.k
Salamu yao huwa ni Moja tu
GOOD MORNING
haijalishi ni Asubuhi, Mchana, Jioni ama Usiku.
Siku ya kwanza hahaah yale masharti yao ya salamu, mnazunguka duara, mara ushuhuda kwa watangulizi
Duh
Nikajisemea kimoyo moyo
wallah Leo nimeingia Freemason
nimeingia cha kike!
Hiyo nyumba yenyewe ili uingie humo utadhani unaingia Ikulu mizengwe kibao, huwezi kuingia ingia tu
HATA SIJUI WANACHOHOFIA.
Nikaoneshwa walioacha kazi zao za maana zenye mishahara mikubwa kisa kuingia Qnet
AKILI IKAGOMA
Wana maneno mazuri
utasikia HUYU NI MTU MUHIMU SANA NINAYEJIFUNZA VITU VINGI KWAKE, MTU NINAYEMHESHIMU MNO, ALIYENIONESHA HII FURSA, n.k
Nikaonesha bidhaa mara
saa za mkononi, vifurushi vya holidays, vya Elimu
AKILI IKAGOMA.
Nikaelekezwa kuhusu B-system inavyofanya kazi
AKILI IKAGOMA.
Saa za hadi $2000 kwa mtz wa kawaida?
Eti ni wadhamini wa F1
Hahah
KIFUPI SIKURUDI TENA
WALA SIFIKIRII KURUDI QNET
Hahah AMA
KWELI UKIITWA KUWA NJOO KUNA FURSA
BASI TAMBUA KUWA HAPO
HIYO FURSA NI WEWE MWENYEWE.