Mambo 30 usiyoyajua kuhusu utapeli wa Q-Net (Network Marketing)

Haha bro umeanza kwa mbwe mbwe kubwa sana. But hujaweza kuelezea UZI wangu unashida sehemu ipi? Umeshindwa kuendana na mada yangu.. unapopinga kuwa qnet sio ecommerce njoo na mifano iliyo hai..
Je unaelewa hasa ecommerce ni nin?
Kwa nin qnet ikose sifa za kuwa ecommerce?
Lete hoja
Ukaenda kukopy bandiko la watu wa India. Sina hakika hata kama umesoma vyema maandishi ya humo ndani. Sijaona jambo la ajabu kwa kampuni kutuhumiwa.. kila kampuni duniani huoata tuhuma hii na ile.. hivi aribuni tumeshuhudia facebook ikituhumiwa kutumia siru za memmber wake.. ni juzi juzi tu tumemshuhudia Marc Mello akituhumiwa kuhusu JF inavyofanya kazi ..
Si jambo geni kutuhumiwa kwa vile hanzo vha tuhuma huwa pia ni kutoelewa jambo fulani..
Aya ya mwisho ya bandiko lako la wahindi limeelzea hali halisi. Qnet haikushikwa na HATIA..
Kasumba hizi za kutoeleweka kwa hii kampuni haikuwa tu India ni sehemu nyingi duniani na hadi hivi leo hakuna sehemu hata moja ikashikwa na hatia.
Qnet ni Ecommerce.

Wewe unadhania nchi yako haipo makini kwenye idara zake za usalama na mambo ya uchumi na biashara kiasi kwamba mwaka wa tatu huu sasa tangu wimbi kubwa la qnet products kuanza kuuzika hapa nchini alafu hadi leo iwe haija jua nini cha kufanya.?


Mda si mrefu nitakuja kuelezea how you can buy your product from there where you are.
Mada ni Qnet ni Ecommerce.
Baki kwenye mada
 
Mtoa mada, Anashindwa kujibu maswali ya msingi anayoulizwa.
Swali gani mkuu?
Embu ainisha swali lipi linalohusu Qnet ni Ecommerce sijalijibu.
Tatizo wadau wanataka nimalize kila kitu hapa hapa.
Nimejiwekea utaratibu wa kuja na mada 1 kila week. Na nitakuwa najibu hoja juu ya mada husika tu.
Una swali lipi juu ya qnet ni ecommerce?
 
Wewe kijana unaonekana una shida kichwani, si muda mrefu utalizwa utashindwa ukalilie wapi. Umepewa hadi ushahidi wa kimahakama bado kichwa kigumu? hata RIFARO walikuwa vichwa vigumu hivihivi, leo waulize wako wapi, ulizia pia D9 watu waliolizwa wana hali gani sasa hivi. Ondoa hizi takataka zako hapa, usije kuharibu vchwa vya watanzania wengine waache kufikiri kufanya kazi na kujipatia kipato wakaishia kupewa ndoto za abunuasi na kulizwa.
 
Kwamba huo ushahidi wa kimahakama unaelezea hukumu ipi kwa hatia ipi?
Hivi unadhania wenye akili timamu wakisoma unachoandika wewe na mimi yupi anayeonekana mwenye shida kichwani?
Unazungumzia kulizwa kulizwa vipi labda? kwamba wa kutumia ecommerce sytem ya qnet nitalizwa pesa zangu kwa maana sitopewa nilichonunua au?
Lete vitu kama hivi.. baki kwenye mada.

Mimi ni mtalii tuseme, unataka kusema kama nahitaji kununua tripsavr pacage ili nitumie Zanzibar kwenye holiday yangu nisinunue kwa vile sitopewa huduma au naibiwaje labda?

Embu niambie napigwa vipi kwa kutumia Ecommerce platform ya Qnet kununua bidhaa nipendayo? Au twambie wewe uliibiwa vipi hukupewa bidhaa? Ulipewa bidha fake au? Kwamba cheni zao wanazouza ni feki au?
Embu nipe fact kwa mujibu wa mada. Achana na habari za Fulsa za kibishara. Sijazizungumzia kw enye mada.
Subiri ijumaa nitakuja pande hizo. But leo kaa kwenye mada.


Hata wewe waweza tuhumiwa umebaka na kumbe sio.. wangapi wametuhumiwa wameua kumbe sio.. embu tuambie ushahidi wa mahakama umesemaje juu ya jiyo kesi ya kihindi? Hahhaha

Au hujui kusoma wewe umekop tu ukapest.. hujaona kuwa huo ushahidi uliouleta unakuonesha kuwa mahakama haikuishika kampuni kwa hatia yeyote. Na mwisho unaambiwa kuwa upande wa mashtaka wanajipanga kukata rufaa.. si ndio bandiko lako ulilolileta. Kw taarifa yako mabandiko kama hayo yapo lukuki na niliyasoma tangu 2016 We unaleta leo.. hhhaaha
Baki kwenye mada sipo kushawishi mtu hapa.
Kuna watu wanachambua pumba mchele na hawacomment kitu.
Relax.
 
Ujue nakusubiri uje tena na picha za kuonesha umekwama wapi kwenye kununua na wapi ukaambiwa ujiunge?
Njoo bandugu.
Au bando limekata?
Qnet ni ecommerce.
 
Yaani we jamaa unadhani kote sikupita huko.

Sehemu ya shop inaleta log in inayohitaji ir id of my referral ambayo ni lazima ijazwe.

Unaijua hata web yenu kweli?
 
Yaani we jamaa unadhani kote sikupita huko.

Sehemu ya shop inaleta log in inayohitaji ir id of my referral ambayo ni lazima ijazwe.

Unaijua hata web yenu kweli?
Haha nilkutumia njia sahihi ya kuingia dukani kwa Ecommerce system a qnet. It is very simple
1. Ingia _ www.qnet.net
2. Ingia _ shop
Utaletewa ujumbe wa tahadhari unakukumbusha kuwa unainhia duka la retail na unakuambia kama wewe ni IR then log in au kama sio endelea.
3. Kwnye huo ujumbe chagua _continue to shop
Kuna ukurasa utakuja ikiwa ni hatua ya mwanzo ya manunuzi unatakiwa kujaza namba ya referer wako na nchi uliyopo. Hapo chagua option ya kiwa huna refere number. Ipo chini ya kibox ulichopaswa kujaza namba ya referer.
4. Jaza nchi yako na click kwenye I DONT HAVE REFERER NUMBER
5. then utakuwa umeingia dukani na endelea na hatua zingine za manunuzi kama kawaida.

Go now. Then be back here.

Any body can do this.
Lets do it then tuje na mrejesho hapa je Qnet sio Ecommerce?
Je umeungwa mahali ulivyokuwa ukinunua?
Here we go

QNET is ECOMMERCE
 
Nikirejea kauli ya mtoa mada amezungumzia E-commerce pekee, huku akijaribu kutolea mifano ya jinsi hiyo e-commerce inavyofanya kazi basi. Na sio ishu za kujiunga kupitia hizo products ambazo hupatikana kwenye duka lililopo katika website yao.
Na hapo ndipo alipoharibu na kutaka kupotosha watu while inajulikana kua hyo ni network marketing kama zingine tu
 
Habari wandugu. Nimerudi tena kama nilivyoahidi kuwepo hapa kila Ijumaa kwa new thread.

My last topic ilienda vizuri na kulikuwa a maswali mengi nje ya topic ambapo mengi yao yataweza jibika kwenye hii topic ya leo.

Ingawa katika hatua za mwisho ikatokea tu nikawa siioni tena topic yangu na kupelekea kushindwa kushiriki tena kwenye mjadala but sio mbaya leo naendelea.

Tujikumbushe last week.. topic ilikua QNET ni ECOMMERCE ambapo tuliona kuwa yeyote aliyepo popote duniani anaweza nunua bidhaa yoyote aipendayo kutoka QNET system na akapatiwa bila kujiunga mahali wala bila kufika mahali ( kwa kifupi ukiwa hapo ulipo unaweza jinunulia utakacho kutoka qnet system the same kama ufanyavyo kwa alibaba.com, ebay au Amazon.

Hatua zake ni simple
1. ingia www.qnet.net
2. then ingia shop
3. then maelezo yoyote yatakayokuja wewe ingia continue to shop.
4. Utajaza nchi yako na chagua I DONT HAVE REFERER
5 shop ya qnet itakuwa open na utanunua utakacho bila bugdha yeyote.

MADA YA LEO NI MOJA TU, naamini kuna mengi yahusuyo QNET but mimi nitakua nakuja na MOJA, MOJA kila week.

Okay. So today mada mpya ni:

QNET ni DIRECT SELLING

Direct Selling ni mtindo wa uuzaji bidhaa moja kwa moja kwa mlaji bila kupitia kwenye mazingira ya reja reja / retail, badala yake mauzo hufanywa maofisini, makazini, majumbani, online au popote pale pasi na store wala physical shop.
Mfumo huu huondoa watu wengi wa kati katika chain of distribution hivyo product hutoka kwa mzalishaji kisha hupitia kwa direct selling company to rep (wawakilishi/ wasambazaji) hadi kwa mlaji.

Bidhaa zote zinazouzwa kwa mtindo huu huwa hazipo kwenye maduka ya kawaida hivyo ukitaka kununua bidhaa hizo njia pekee ni kwa kutumia wawakilishi hao (rep).

Direct selling inahusha mitindo mbali mbali
(a) Single level marketing ambapo msambaji hufanya kazi peke yake na hutengeneza pesa kwa commision kutokana na mauzo afanyayo yeye kama yeye pekee.

(b) Multi level markteng (MLM) ambapo msambajazi hufanya kazi kwa kushirikiana na wasambazaji wenzake na hutengeneza pesa kwa commision kutokana na mauzo afanyayo yeye pamoja na yale ya wenzake kwenye team yake.

QNET ikiwa kama ecommerce platform pia inatoa mwanya kwa yeyote apendaye kuwa msamazaji wa bidhaa zake ajisajiri kwenye mfumo wao wa directselling na kuwa rep /muwakilishi wacompany.

Atakuwa akipata commision kwa kadri atakavyokuwa akisababisha mauzo. Anakuwa na ihari ya kuchagua mtindo aupendao kusambaza iwe ni MLM au hata SLM ni juu yake.

Utaratibu wa mtu kuwa msambazaji wa kampuni ya QNET upo wazi kwenye website yao. (hakuna ulazima wa kuitwa mahali ili uwe rep wa kampuni ya qnet).
Maelezo zaidi juu ya hili pia unaweza yapata kwa rep (IR) yeyote wa kampuni hiyo.

Kutokana na uhiari wa kuchagua mtindo wa kusambaza bidhaa ndio maana utakuta ndani ya qnet kumekuwa na network groups mbali mbali katika miji na mataifa mbali mbali zenye kutofautiana style ya utendaji kazi ikiwemo pia utofauti wa perfomance.

Kwa wale walioamua kuwa rep wa qnet na wanatumia MLM style wanaweza amua ni vigezo gani anavyohitaji mshiriki mwenza awe navyo ili afanye naye kazi ili mradi tu ziendane na Policy & Procedures za kampuni.

kutokana na MLM procedure kuwa na changamoto mbali mbali katika jamii kutokana na kutoeleweka kwa sababu ya ugeni na upekee (uniqueness) wa tasinia hii kwenye jamii. Wasambazaji wa qent products wamekuwa wakipatiwa training kutoka kwenye special company iliyotengwa kwa kazi hiyo tu na hivyo kuwafanya wawe imara na wataalamu kwenye tasnia.

Locations mbali mbali zenye vikundi au teams za IR wa qnet wakifanya shughuli zao. Hizo ni sehemu zao wao na sio OFFICE za kampuni za QNET.

Kampuni ya Qnet kama ilivyo kwa makampuni mengine yatumiayo mifumu ya MLM imeweka Kanuni na Sheria zinanowaongoza IR wake kuepukana na tabia ya IRs wasio waaminifu kwa kutoa ahadi za uongo kwa watu ili kuvutia washiriki na kusababisha taharuki na uchafuzi wa sura ya tasnia na kampuni. Hivyo kuna Code of ethics pamoja na Policy and procedures zinazowaongoza rep wa kampuni kwenye shughuli zao.
Mfumo wa MLM sio mfumo wa kupata utajiri kwa haraka wala kiurahisi kama ambavyo jamii inavyodhania.

Mafanikio ya mtu binafsi Au hata team (kikundi) katika mfumo huu wa usambazaji yanatokana na Shauku, Ari ya mafanikio, juhudi, ubunifu, ustahimilivu dhidi ya vikwazo na changamoto, ukweli na uwazi (honest) na pia kutokana na uwezo wa kiuongozi alionao mtu binafsi.

Kufeli kibiashara kwa rep (IR) yeyote hakumaanishi kuwa bidhaa za Qnet zinakasoro au Fulsa ya kibiashara ya Qnet inakasoro bali ni kutokana na mtu binafsi alivyokosa umakini kwenye utendaji wa shughuli zake kwani hadi leo sijawahi sikia kuwepo kwa aliyewahi nyimwa commision na kampuni.

Makosa na utovu wa adabu au hali kutokuwa na uaminifu kwa IR au rep wa kampuni hakumaanishi kuwa QNET ndio imefanya makosa hayo. Bali nayo ni makosa ya watu au rep na si QNET.

Mafanikio ya any Rep hayamaanishi ni uzuri wa kampuni ya Qnet bali ni ubora wa mtu binafsi kama rep wa kampuni akiwa kama mjasiriamali makini.

Maelezo zaidi juu ya kanuni, sheria na code of ethics kuhusu kuwa IR wa qnet yapo kwenye website yao www.qnet.net


Hivyo basi Qnet unaweza itumia kununua bidhaa uipendayo na kubaki kuwa mteja au unaweza amua kuwa rep wa kusambaza bidhaa zao kwa mfumo wa direct selling.

Kwa leo niishie hapa. Hadi week ijayo.

Leo nitajibu maswali na hoja zote zinazohusu MLM, SLM na Direct selling kuhusu QNET.

Thanks
 
Haya ulosema ndo yalinitokea jana Zanzibar-ASP
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…