Mambo 30 usiyoyajua kuhusu utapeli wa Q-Net (Network Marketing)


Ndio wanavyoanza hivyo, wanaanza na kukushawishi kuwa utakuwa Tajiri, Qnet inafadhili timu ya Manchester United, usiwe na wasiwasi, yeye amenunua bidhaa ya milioni nne, nk..

Utapeli, Utapeli Utapeli..
 
Reactions: Ctr
Vipi na wale forever living product!!? Huwa nahisi nao Ni sawa na hawa QNet
 
Nilichogundua kwamba wajinga duniani hawaishi na hawatokuja kuisha ,watu wanaingizwa mkenge sana hiyo qnet,,,Oriflame nao wanafunga virago , Forever nao wanapumulia mashine now wanauza hadi dawa za nguvu za kiume,ma tycoon wa forever wanapiga mishe nyingine za kuwatapeli wajinga(KEKUNDU KEKUNDU).
 
Kuna mfanyakazi mwenzangu alikopa 5m kujiunga jamani tumejuta aseehh!usumbufu kila kona anatushawishi na hakupata hata supporters mwisho kaja kuishia kua tapeli maana anakatwa pesa nyingi hela hana qnet wamekula mkopo wote
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daah, wapenda shortcut lazima walie tu

House girl(dada wa kazi) Ni binadamu aheshimiwe, apumzike, apewe Uhuru wa kuabudu pia
 
Hao Qnets nadhani wana watogaga..mana kuna jamaa alikua chuo..kapigwa upofu wa hilo kampuni..kamdanganya mzazi wake..6m kawapatia Qnet..sahv hana mbele wala nyuma.
Hivi watanzania tunakwama wapi?
Yaani mtu hajawahi kufanya hata biashara ya mtaji wa laki moja, anaenda QNET anaimbishwa maneno kibao halafu anakwenda kuzisaka popote zaidi ya 4milioni halafu anawapa QNET.
Tumerogwa na nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeeleza kwa ufasaha sana hongèra sana
 
Qnet Ni utapeli
 
Hawa majamaa wameniita wamenipiga msasa wa hatari et Nina Bahat sana, Mara good morning hata jioni....nimewauliza kiingilio sh ngap...wakanificha wanadai kesho nirud ndo watanijuza...alaf hawatak nimwambie mtu.... Kesho hawanioni....
Jamiiforums is a school of aweareness.!
Bear it in your mind

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafaidi matunda ya Qnet kupitia mteja wangu aliyejaribu kunirubuni akashindwa, huwa akija kwangu nikitaja bei wala haliilii kupunguziwa sijui ndo ananiringishia utajiri.... huwa nafurahi sana anavyonikomoa kwa kuniachia vichenji ili nimwone maisha bora.

Good morning.
 
Hahahaha dah, sawa mkuu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…