Mambo 30 usiyoyajua kuhusu utapeli wa Q-Net (Network Marketing)

Sijui kwanini SIRIKALI haifungii hili dubwasha
Bora iendelee kuwepo na wengine waendelee kuwatapeli watu. Maana jamii yetu inawajinga wengi, kila wakielimishwa wao hawasikii.

Kuna wengine wanaitwa Wozur, kampuni inajidai imesajiliwa UK lakini kumbe hamna kitu. Wacha watu wapigwe. Ujinga wa huyu ni utajiri wa yule.
 
sjasoma ilo gazeti lako ( tena la Rai ), nachojua hao jamaa ni wapigaji
 
Kipigo Chake Ni Cha Mbwa Ko Ko
[emoji3][emoji16][emoji23][emoji28][emoji1][emoji2][emoji1787][emoji23][emoji16][emoji3][emoji28][emoji1][emoji2][emoji1787]
Ni mshenzi tu[emoji23][emoji23]
 
Kabisa!
 
Hongera sana chief umechambua vizuri sana
 
Hongera sana chief umechambua vizuri sana
Nimeona nitoe dukuduku langu hawa Qnet watu wengi waliojiunga hawakupata muda wa kujiridhisha kuhusu hii kampuni, mana wale jamaa wakikushika huwa hawakuachi mpaka aidha utauza chako au utakopa au namna nyengine lakini baada ya mawasilisho yale ya mwisho hawakupi ata wiki watataka wakusajili ulipe zile milioni 5
 
Umechelewa sana ndugu kupata hii fursa yaani kifupi ni utajiri nje nje usipoteze nafasi hiyo adhimu wenzio wanaililia,JIUNGE HARAKA KISHA JIPIGE KIFUANI MARA TATU KISHA SEMA "Mimi ni mpumbavu"
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]hili jibu huwezi kusoma bil kucheka
 
ukiitwa kwenye fursa tambua weye ndo fursaa ,achana na uduanzi namna eyo wa kukimbilia haya makampuni mageni haswa hiii QNET.Hakuna hata haja ya kuchimba sana hzi details za huu utopolo, evi sijuhi akili zenu huwa mnaburuzaga kwenye mitalo alfu ndo mnatumia au ndo mpaka mshikiwe safe place ndo zione?.
Hii ni karne ya 21 unataka kufanya bishara kama kansa mansa mussa ,unashindwa kujisimamia mwenyew alfu unataka kujiungwa Qnet saa si utopolooo mtupu.....lisemwalo lipoo

kazana kulilia utopolo wakutopole
 
Nilivunja urafiki wa kifamili just because mke wa jamaa yangu alimshawishi wife ajiunge Q Net alafu anamwambia iwe siri yao.

Shubhaaamit
 
Mmi nimekutana nao jana, mshikaji wangu kanipeleka. Ilikuwa saa Saba mchana nikashangaa nilipofika nikashangaa wanasalimiana GOOD MORNING nilishituka Nikawaza labda nipo Dunia Nyingine, lakni haikuwa hivyo nikajisemea moyoni kiingereza kimevamiwa na wahuni. Si nikapewa wasilisho na simulizi zote kuhusu Qnet sikuwa najua hili wala lile. Ukafika mda wa maswali na majibu, unajuwa ilikuwaje? Niliwabana kwenye kodi, nikawabana Faida ya Kampuni iko wapi, pia nikawabana mfumo mzima wa uendeshaji wa biashara ili kampuni iweze kupata faida . Majibu yalotolewa hata sikuyaelewa ikabaki siri yangu
Nikakubaliana nao ili yaishe isijeonekana mimi mkorofi, kitu kingine ambacho sikukielewa na sikutaka kukiuliza ni kwanini wanafanya kama siri hii biashara? Niliwaza na kutafakari nikajisemea hapa hakuna kitu; kusema kweli hawa jamaa wamejipanga kushawishi watu.
Baada ya yote waliniomba nirudi tena siku nyingine kwa ajili ya kupata somo awamu ya pili.
Hapa nawaza Je, nirudi tena nikawasikilize au niwapotezee?
Naomba ushauri wana JamiiForums
 
Wako kwenye radar ya TAKUKURU hao achana nao mkuu,ni pyramid scheme.Halafu wamepigwa marufuku katika nchi zifuatazo:-

  • Afghanistan (2008)
  • Rwanda (2009)
  • Iran (2005)
  • Sri Lanka (2004)
  • USA & Canada (2008)
  • Syria (2009)
  • India (2010)
 
Yaan wew yamekukuta kama ya kwangu.. walinipa intro wao wanasema ni 20% ya intro 80% ntaipata siku ya pili.. sikurudi hadi leo [emoji38][emoji38] maana naisikia imeliza wengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…