Mambo ambayo sikuwa nayafahamu kuhusu Israel kabla ya "Gaza war"!

Hamas imeitwa kundi la kigaidi baada ya oct 7,kabla ya hapo mbona haikuwa hivyo?Inamaana hiyo article West hawakuiona?kuclaim ardhi yako sio ugaidi
 
Uko brainwashed na unapelekwa tu!Hao Hamas wako occupied West bank?Hamas wako Gaza,sasa hayo niliyoandika yanawakumba wapalestina wote,wa Gaza na West bank!
Yaani mtu anakalia ardhi yako kimabavu,unatakiwa utulie tu!Upangiwe muda wa kutoka ndani na muda wa kurudi,uishi kama mnyama anayefugwa!Halafu eti unaleta story za watoto kufundishwa kurusha mawe,so what?Ndio akimpiga jiwe Askari,ndio apelekwe military court na kuhukumiwa miaka mpaka 20 jela?Uko serious?
 
Israel is last remaining apartheid country in the world.
 
Hapa Mimi nimeleta kile nilichokuwa sijui Kama kipo!Wewe ulichojibu no kuwa kinachofanyika ni sahihi maana Israel anajilinda Kama nimekuelewa!
Ndio nahoji,Kuna uhalali wa collective punishment?

Mkuu unataka twende kwenye rules of War engagements..... Huwa ni za kwenye makaratasi tu! Second World War unafahamu scale of destruction iliyofanyika Ujerumani? Hakuna proportion war, yaani wewe ukiuwa watano, na mimi niuwe upande wako watu watano...Vita siku zote ni destruction of your enemy.PERIOD

Hamas waliopoenda kufanya Mashambulizi October 7 Hawakuwa na guideline yoyote ya rules of engagement! Ilikuwa ni destruction yoyote ile kwa adui yao Myahudi, Sasa kwa nini Israel ipigane kwa different standard!
Vita sio kitu kizuri, naamini Hamas anajua hilo ndio maana alifanya investment kubwa kwenye Mahandaki....alikuwa anajua adui yake ana uwezo gani.....Collective punishment is part of War, achana na makaratasi ya Geneva convention ambayo huwa yanatengenezwa wakati wa amani...
 
Wewe umeongelea baada ya oct 7 na vita vya Gaza,Mimi nasema wapalestina wamekuwa wakiyaishi maisha hayo kabla ya oct 7!Yaani niliyotaja hapo juu,yote yamekuwa yakifanyika ila Mimi nimeyajua baada ya hii vita!
So,jielekeze hapo!
 

Mkuu Borne -e :

Ondoa swala kuwa brainwashed mkuu, kila mtu humu ndani ameamua kufuata narrative yake! Mimi naweza kukuona uko brainwashed.....na wewe kwangu pia! Hata ukileta facts zako hata zangu zitapata interpretation tofauti!

Unaposema amekalia ardhi kimabavu...ni ardhi ipi hiyo? Ni ule mgawanyo uliko katika UN Resolution 181 ya 1947? Au ambao Israel imechukua katika vita vya 1948, 1967, 1973?

Hivyo ni vigumu wote humu kuwa na lense moja....Halafu kuna factor ya dini pia...usisahau yote hayo unapozungumzia mgogoro huu!.
 
Wewe umeongelea baada ya oct 7 na vita vya Gaza,Mimi nasema wapalestina wamekuwa wakiyaishi maisha hayo kabla ya oct 7!Yaani niliyotaja hapo juu,yote yamekuwa yakifanyika ila Mimi nimeyajua baada ya hii vita!
So,jielekeze hapo!

Mkuu mbona husemi pia Israel imekuwa ikiishi maisha gani toka wakati wowote utakao chagua wewe...Iwe 1948....1967...1973...mpaka leo! Ni roketi ngapi zinarushwa mkuu....Kuna narratives ya kulewa kwa kila upande.
 
Mkuu mbona husemi pia Israel imekuwa ikiishi maisha gani toka wakati wowote utakao chagua wewe...Iwe 1948....1967...1973...mpaka leo! Ni roketi ngapi zinarushwa mkuu....Kuna narratives ya kulewa kwa kila upande.
Mkuu Mimi nimeongelea upande wa Palestine na kinachowakuta raia wakubwa kwa watoto!So mbaya nawe ukaandika ambayo wananchi wa Israel wanakumbana nayo kutoka kwa wapalestina!
 
Baby killers mwaka jana kuna wanajeshi wa israel waliwauwa watoto wa wanne wa palestina watoto walikuwa tu wanacheza ufukwen wao wakawapa shaba

Balance your information mkuu....Hamas alichofanya October 7 ni nini mkuu? Kama sio Baby Killers.....Unajua idadi ya suicide kwenye mabasi, mikahawa West bank....? Hao suicidal bombers walikuwa wanaua panya?
 
Hivi umewahi kufuatilia Israel wanachowafanyia wapalestina wa ukingo wa magharibi?

Ukitaka kuuelewa huu mgogoro usichague upande kwanza. Fuatilia kwa kina utajua nani anafanya nini.

Halafu jaribu kuvaa viatu vya kila mmoja wao uone ungechukua hatua gani.
 
Tz chadema akiguswa tu na risasi marekani hao wanalaani. Lkn sasa hivi hatuwasikilizi tena
 
Sheria za ugaidi ndizo zinazofanya kazi hiyo hata Tanzania mlilazimishwa kutunga sheria zinazoendana na mdundo huo baada ya kimbembe cha kujilipua kilipotokea mwaka 1998 Dar Es Salaam kwenye ubalozi wa Marekani.

Kwa hiyo hapa wala usisingizie Israel ambayo imezungukwa na nchi zenye jamii ya kijicho, chuki na uchokozi karibu asilimia 80% ya pande zote ikimaanisha Lebanoni, Syria, Jordan, Gaza strip, West bank zikihanikizwa viburi na Iran, Iraq, Yemen na Uturuki.

Nchi za kiarabu zenye watu wenye roho isyo na visasi dhidi ya Israel ni Qatar, Saudi Arabia, UAE na kwa mbali Egypty
 


Mathewa:

Ukivaa viatu vya Israel toka 1947 ...na Vita vya 1948, 1967, 1973 na Mambo tunayoona Gaza lazima uchukue hatua ambayo Israel inachukua....Na Ukivaa viatu vya Wapelestine.....Kabla ya 1948 walikuwa wanajitambulisha kama Waarabu tu...ingawa eneo lilikuwa linaitwa Palestine...na Baada ya kuwa wanashindwa kila Vita, yaani 1948, 1967, 1973....na lazima wafanye walichokifanya October 7! Hawana option, kila option imeshindwa kufanya kazi, na inaonekana hakuna itakayofanya kazi! Hivyo Mkuu ni wewe kuamua ni narrative gani umeamua kuifuata.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…