Angalia revolution ya map ya Palestine alafu ndio utajua nani mkorofi,
Unajua nini kilitokea baada ya UN Kufanya partion 1947? Waisrael walikubali mgao wa UN, Waarabu walikataa na kuamua kupigana 1948.......that was the greatest mistake! Wao Wanaita Nakba....! Huu ndio ulikuwa Mwanzo wa kushindwa! Kumbuka ukiangalia Ramani ya UN 1947, Jerusalem hawakupewa Waarabu wala Wayahudi...Iliacha iwe International City.......asiwe mtu ana mamlaka nayo....Waarabu Waliaamua kuja kwa njia ya Vita na Israel 1948, yalikuwa mataifa matano! Lebanon, Syria, Iraq, na Egpty,Israel iliyashinda hayo mataifa matano na iliwanyang'anya hata kile walichopewa na UN 1947.
Hili ni kosa la kwanza kubwa, Waarabu Wengi waliokuwepo hapa waliondoka kabla ya Vita vya 1948, kwa sababu walijua "obvious" Israel itashindwa......Na Wakatawanyika katika nchi nyingi za Kiarabu na kuwa Wakimbizi na kutambulikana kama Waplestina. Hivyo vita vya 1948 iliwapa Israel more Land, na kuzidi kuingiza Wayahudi wengi waliokuwa Wamesambaa Ulaya, Waarabu wengi waliondoka, na Israel ikatumia mwanya wa vita kuwaondoa baadhi kwa nguvu!
Waarabu hawakuishia hapo, Wakajaribu tena 1967.....Yalikuwa ni kujihami na mashambulizi ya kushtukiza, Katika vita hii Waarabu ( Egypt, Jordan na Syria walishindwa tena! Unajua walipoteza nini, Israel iliichukua Sinai Peninsula, Ukanda wa Gaza, na milima ya Golan! na East Jerusalem Kama Waarabu wasingelianzisha vita 1967 wasingepoteza maeneo hayo. Kuna mambo mengi yametokea 1967 ambayo yamekuwa kama bench mark ya kujaribu kutatua mgogoro huu
Waarabu wakarusha kete nyingine 1973, October 6, Egypt na Syria walifanya mashambulizi ya kushtukiza kwa pamoja, na Mrusi alikuwa amewaanda kikamilifu, na walikuwa na silaha na vifaru zaidi ya Israel, hili lilikuwa shambulizi kubwa la kustukiza, Mashambulizi yalianzia Sinai Peninsula upande wa Egpty na Syria milima ya Golan, waarabu walishindwa vibaya mno, na msaada wa Marekani ndio uliowaokoa.
Kumbuka Mwaka 1967 August 29 Waarabu walikutana Khartom, Sudan wakala yamini kwa pamoja, na kutoka na Azimio la "THREE NO"
1.No peace deal with Israel.
2 No Recognition with Israel.
3 No negations with Israel!
Baada ya kushindwa 1973, na Egypt kutambua kuwa Kijeshi haiwezi kabisa kuishinda Israel, ikaanza kufanya mapatano na Israel, na kurudishiwa Sinai peninsular 1979, katika mkutano wa Camp David, Waarabu wengi hawakufurahi, maana ili kuipata tena Sinai Peninsular ilibidi iitambue kuwepo kwa taifa la Israel! Mapatano hayo yaliwa waumiza mno baadhi Waarabu, na hata wenye misimamo mikali.....na Kufanya Sadat kuuwawa October 6, 1981 na Yatzhak Rabin 1995!
Kama ni kwa njia ya vita Waarabu wamejaribu na wamekuwa wakishindwa, wengi tulitegemea Iran hasa katika vita hii ya Gaza inaweza kufanya attempt ya Vita kama Waarabu walivyofanya huko nyuma, lakini yunaishia kuona Gaza inagawanywa vipande viwili mbele ya Iran! Imeumiza mno kwa Wapelestina,
Mtazamo wangu binafsi, Mwarabu na Myahudi ni kuwa Wote wana historical attachment na hiyo land! Ushahidi wa historia na imani zao za dini unaonyesha hivyo. Ni mitazamo radical ambayo iko pande zote unafanya washindwe kabisa kufikia muafaka.
Na kuangalia historia toka 1947 ni vigumu kwa upande wangu kuita Israel Wavamizi, UN iliwapa wote Waarabu na Wayahudi kila mtu sehemu yake, Israel ikajitangaza kama taifa katika sehemu yake 1948, Waarabu ( Wapelestine) Hawakujitangaza kabisa kama taifa katika sehemu yao, Walitegemea kwa njia ya vita wataweza kuiondoa Israel mahali hapo, mpaka leo hilo halijafanikiwa, na Israel imeshakuwa taifa imara, ni vigumu kuifuta chini ya jua.
Ujio wa Hamas na mitazamo yake ya kidini, umeleta more confusion kuliko solution, na wala hauwezi kabisa kusogeza hata hatua moja ya kusaidia Wapelestina.