Kiukweli kutimuliwa kwa Big kulinichanganya sana. Nilikuja kuambiwa kwamba my colleague is no longer working with us siku nilipoingia ofsini baada ya kutoka training. Big alikuwa ni kampani yangu sana kati ya staff wote pale, labda kwa kuwa tuliingia mjengoni pamoja. Nikamcheki Big kwenye akawa hawezi hata kuongea analia tuu. Wkennd iliyofuata nikaonana nae akasema anapanga kuja ofsini kuomba radhi ili apewe second chance. Kweli wiki iliyofata alikuja ofsini pale kama mara tatu lkn wakubwa wakawa wanamfungia vioo, kimtindo flani Big alikubali kudhalilika mana kuna siku nasikia alipa magoti kwa boss kubwa akimshika miguu ili afikiriwe. Sikuhiyo mimi sikuwepo ila nilipata story. Nikakumbuka kujidhalilisha kwenye shida ni kawaida hata mimi nilishawahi kufanya kwa Dr KJ kama mnakumbuka. Shida inakuja inaumiza sana ujidhalilishe halafu na msaada wenyewe usipewe – aisee!!!
Wakati namiuwazia Big nikasema inawekana BIG aliingizwa kwenye mfumo wa wakubwa bila yeye kujua. Maana na mimi nalumbuka kuna awkward situation moja iliwahi kunikuta pale ofsini nikiwa kama na miezi miwili hivi kipindi ndio tunasubiri subiria tumalizane na probation. Ile situation sikuwa na hakika kama ulikuwa ni mtego ama vipi ila kiukweli ile situation ilinivuruga sana sio kidogo.
Labda niwarudishe nyuma kidogo niliwaambia kwamba ile ofisi ilikuwa na line managers wa idara tofauti tofauti ambao walikuwa ndio sehemeu ya Office Management Team (OMT). Hawa OMT ndio walikuwa ndio wanaomua mustakabali wa ofisi kwenye uendeshaji na mwellekeo wa ofisi. Na niwakumbushe tu niliwaambia kwamba idara yetu ndio ilikuwa ndo inadili na fedha za ruzuku kwenye kuamua nani aapate na asipate, so sisi officers ndio tulikuwa na madaraka ya kupitisha kulingana na mafaili (portifolio) unayofanyia kazi. Kwa hiyo kwenye kupata hizo grants mnoko wa kwanza kukubania usipate fedha ni sisi, au favour ya kwanza ya upendeleo ilikuwa inatoka kwetu. Tulikuwa ndio uti wa mgongo wa NGOs kupata au kokosa ruzuku.
Sasa nakumbuka line meneja wetu pamoja boss kubwa mwenyewe – CEO mara kwa mara walikuwa wanatuweka vikao vya kukumbushana kuhusu maadili ya kazi kwenye idara yetu. Kuna siku boss kubwa mwenyewe alituita mimi na mshikaji wangu Big ofisini kwake na kutuweka licheni ya masaa kama mawii na ushee akiongea na sisi kuhusu maswala ya integrit na being professional katika kazi.
According to Boss kubwa alisisitiza kwamba one strong reason why an employee must be ethical and professional in the workplace is to maintain and enhance the organization's reputation. Ethical and professional behavior contributes to a positive work environment, fosters trust among colleagues, clients, and stakeholders, and reflects positively on the company as a whole. Kwake yeye image ya shirika ilikuwa ni kitu cha msingi sana for organization sustainability. Alisisitiza san asana tujiepushe nay a kipuuzi kwani yeye aliamini kwamba unethical behavior can lead to legal issues; damage the organization's reputation, na kupoteza trust among employees and stakeholders. Yale mamneno binafsi yaliniingia sana nikajiongeza Boss kubwa himself sio mjinga mpaka atumie muda wake wote huo kuongea na sisi kitu ambacho angeweza kufanya HR au line meneja katika idara yetu. Basi kile kikao kikaisha ni kila mtu akabaki na akili kwa kumkichwa.
Siku moja wakati zoezi la kureview proposals za wadau ili kutoa au kutotoa ruzuku likiendelea nikapokea kimemo kutoka kwa one of my colligues wa pale idarani. Labda niseme hivi kuna wale ambao wenye wadau wao ambao wanapenda iwe isiwe lazima wapate ruzuku. Sasa unaweza kuta kwamba labda uyo mdau wako faili lake lipo kwa mtu mwingine, kwahiyo unaweza kufatwa na mwenye interest zake ili uangalie namna ya kumuwezesha huyo mdau. Hiyo ishu ilikuwa inafanyika kulingana na watu jinsi walivyoshibana huwezi tu tumfata kila mtu maana ni risks sana unaweza ukachomwa au ukajichomesha ikala kwako. Yule dada colleague wangu alinpatia kile kimemo na kuniambie kwa kunong’ona kwamba kimetoka kwa kibosile mmoja (line meneja wa department ingine). Kwamaana ya kwamba kuna meneja ameona wadau wake wapo kwangu kwa hiyo niwafanyie mipango wapate.
Wakati bado nafikiria nifanye nini mara yule kibosile akaingia kwenye pool yetu ambapo officers wa idara tunakaa akanicheki kisha akanikonyeza ile kwa kuniambia bila shaka ujumbe umeupata kisha akaendelea na mambo yake. Asee nilikuwa kwenye wakati mgumu sana ukifikiria ilikuwa ni 1st attempt halafu inatoka kwa kibosile. Gafla risala tuliyosomewa na Boss kubwa kwenye ile kicheni ya party ya mimi na Big ikajirudia kichwani mwangu. Nikajiuliza huu ni mtego au kweli yule kibosile ana maanisha. Nilichoamua kufanya sikuifungua kwanza ile memo nikaendelea na kazi maana nikasema nikiifungua yale majina niliyotakiwa kuyafanyia kazi yanaweza yakatibua kazi zangu pengi mengine ndo nimeshayanyima kwa kukosa vigezo. Basi nikauchuna nikaendelea kupiga mzigo.
Baada ya kama siku mbili hivi yule kibosile akamtuma mtu aniite niende ofsini kwake. Kiroho kikapiga paap nikaenda. Kufika kwake akaanza kujichekesha chekesha pale ili kujenga urafiki then akanichomekea kuhusu ile ishu. Akanilobby sana kwamba wale wadau ni muhimu sana sio kwamba yeye anainterest zake ila hata menejiment inajua kwamba wale ni watekelezaji wazuri wa miradi. Kwamba wameshafanya mitradi mingi tuu na ofisi kwahiyo sio vizuri wakakosa. Basi akapiga blabla zake pale na akaniuliza what is the status ya hao wadau wake kama wamekidhi au hawajakidhi?
Nikavuta pumzi pale kisha nikamwambia kiukweli sijui status yao maana kile kimemo mimi sikukifungua. Akaniambia eti hakuna shida maana muda bado tunao kama wiki hivi so nikifungue ni nihakikishe wote wana pata. Nikamuuliza wapo wangapi akaniambia wapo 11, si mchezo mwanawane. Basi nikawaza nikasema huyu kama ni mtego imekula kwake kama yuko real anataka niwabebe hao wadu wake basi leo ataniona mimi ni bonge la mkono. Unajua ipo hivi always trust your gut feelings (machale yako) iwe unconditionally au kwa kujiongeza. Mimi kikubwa kilichonifanya kwanza nione ule ni mtego ilikuwa ni approach ya yule dada mfanyakazi aliyeniapproach. Lazima very strategic katika kuwasoma watu unapoanza kazi mpya, huu uzoefu niliupata kule kwa Dr KJ. Wakati mshikaji wangu Big yuko bize kufatilia watoto wazuri wa kula nao bata and the likes mimi nilikuwa bize kufatilia nani anamichongo gani pale ofsini. Nikaja kubaini pale ndani kuna manyoka kibao sana wanaotumiwa na wakubwa kusoma tabia za watu hususani wageni, huyo dada nae alikuwa ni chawa pro max wa bosskubwa mwenyewe.
Then kingine nikajionea kwamba hoja anazotoa kibosile kwamba wale wadau wake ni wanafanya vizuri hata menejiment inawajua haina mashiko kwa sababu kama ni wazoefu na wabobevu basi kuandika proposal za pale isingekuwa shida. Maana pale pesa zilikuwa zinatolewa nyingi kulingana na uzoefu wako katka ufanyaji kazi na lile shirika so hawa wazoefu wanahaja gani ya kubebwa kama ni wazoefu na hata menejiment inatambua kazi yao.
Basi nikajilipua nikamjibu kibosile kile kimemo mimi nimeshakitupa tena nilikitupa makusudi kwa sababu sikuona umuhimu wa kujua majina ya mahirika ya hao wadau. Nilimwambia wazi kwamba anisamehee sana na kwakuwa ile ilikuwa ni assignment yangu ya kwanza basi nilikuwa nataka niifanye kwa weledi na fea ili niweze kujifunza kuimudu kazi yangu. Niliamua kujilipua kumjibu vile kwa sababu niijua risk yake ambayo kubwa ni uwezekano wa kuingia kwenye bifu kubwa na kibosile kisha kuanza kuwindana kama chui na paka pale ofisini. Maana nilijua kama sio mtego basi kibosile asingekubali mimi kumwangusha kwenye madili yake na yeye ili kujinasua lazima angeweka mikakati ya kuniwahi. Lakini nikaona potelea mbali ila niliingia na mbinu ya kujihami kama plan b. mazungumzo yetu yote niliyarrekodi dadeki kwa maana kama backup plan endapo ishu ingeniback fire.
Yule kibosile ni kama hakuamini vile nilivomtolea nje kavukavu ila akazuga zuga pale kwamba basi nisiwe na wasi wasi anaaamini hao wadau wake wapo vizuri na bila shaka wangekidhi vigezo. Basi tukaachana kila mmoja akiendelea na majukumu yake. Jioni wakati najiandaa kuondoka yule dada informer akaja kwenye desk yangu akanikuliza vipi mmemalizana vipi na kibosile? Kwanza nikashangaa amejuaje kama kulikuwa na kamkutano kasikokuwa na minutes hahaaa lkn nikaishia tu kumzingua pale nikasepa zangu. Basi ile ishu ikapita kama ivyo lkn kile kimemo nilikuwa nacho na baada ya kumaliza mafaili yote baada ya kama wiki nikacheki status za wale wadau wa kibosile. Walikuwa wadau kama 13 hivi na wengi wao karibia 9 walikuwa hawana vigezo kabisa yaani hawabebeki hata kwa mbeleko la chuma ila wnne ndio walikidhi walau vigezo. Na wakidhi tuu kwa sababu mimi sikuwa strikct sana kwenye kufatiia vigezo kama pesa za babaangu yani angekuwa mwingine strictly wale wote walikuwa wanapigwa chini. Basi nilicgofanya niliwarecommend wafanyiwe training ili sikunyingine wakidhi vigezo.
Sasa kumbuka hayo yote yaliyopita nilikuwa nayakumbuka wiki ile Big ametimuliwa ofsini nikasema inawezekana Big naye aliingizwa kwenye mfumo wa wakubwa. Kama vile Mungu siku moja wiki ile ile ambayo Big ametimuliwa line meneja wangu alitukuta na baadhi ya wafanyakazi tunagonga tea kicheni. Sasa sijui aliropoka au vipi akaniambia tena mbele za watu yaani Taidume sijui ulilaie ubavu gani maana ulivonusurika kila mtu ameshangaa. Hii ikanipa maswali sana nilipomuuliza ana maana ganiakazuga zuga tuu lkn wenye akili walielewa. Wafanyakazi wengine wakaniuliza kwani mzee uliponyokaje mimi nikawa nawazingua tu. Ndio kunijia akilini kwamba ile attempt ya kibosile na yule dada ulikuwa ni mtego mmoja mkali sana lakini nikashukuru Mungu nilisimamia weledi. Tena nakumbuka yule dada aliniambia wakati analitea kile kimemo kama na mimi nina wadau wangu wapo kwenye portifolio za wengine basi nimtajie majina yeye atanisaidie kuwafikishia ujumbe, Dah kuna watu wauwaji jamani lakini ndio hivo akili kumkichwa.
Badae sana nikaja kuthibitisha kwamba ule ulikuwa ni mtego na ambao nilivyopona ni kutokana kusimamia weledi kweny kazi nothing more.
Muendelezo soma Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa