EPISODE 5: I gained another job connection through honesty and lack of greed (Uaminifu na kutokuwa na tamaa kunalipa always)
Iko hivi ndugu zanguni, maintaining honesty and avoiding the influence of greed can have positive consequences in various aspects of life, including professional opportunities. When someone prioritizes honesty in his actions and interactions, he builds trust with others. This trust forms the foundation of meaningful relationships, and in the professional context, it can lead to valuable connections and job opportunities.
Maisha ya kazi yalienda kasi sana na kiukweli nilikuwa nimeshaizoea sana kazi yangu. Siku zilitembea na miezi ilikatika kuna ups and downs nyingi sana nilipitia lakini pia nilijifunza mengi mno. God was so good to me . Sasa kama nilivodekeza kule kule mwanzo lile jengo ambalo ofisi yetu zilipokuwepo kulikuwa na maofisi mengine mengi tu mara nyingi lilikuwa bize sana.
Nikiwa nimeshakata miezi kama saba hivi pale ofsini kuna kipindi kazi zilikuwa nyingi sana na ili kumeet my deadlines nisigombane na wakubwa nilikuwa sometimes natoka ofsini pala hata saa 4 usiku. Nakumbuka siku moja nilienda job weekend, ilikuwa jumapili. Sasa nilikuwa ofsini mpaka saa mbili usiku kuna kimeo nilikuwa nakimbizana nacho maana kesho yake nilitakiwa kusafiri mkoani na sikutaka kuacha vimeo nikiwa safarini.
Sasa wakati naingia kwenye lift ili nikishuke chini gafla nikaona kuna simu imeangushwa. Mule kwenye lift kuliko hakuna mtu basi nikaiokota. Ilikuwa smart phone aina ya Sumsung matata sana rangi nyeupe lile toleo lilikuwa bado halijaja bongo. 2012 ile nakumbuka huku kwetu simu za kijanja mara nyingi zilikuwa blackberry au nokia zile zenye button na touch. So ile simu ilikuwa ni android na ilikuwa kama imetumika basis i zaidi ya mwezi. Mimi nikaichukua nikakuta ina line na haina paswed. Sasa wakati huo mimi natumia kisimu cha ajabu ajabu tu ukilinganisha na ule mtambo niliouokota pale. Tama ikanishika nikaizima na kuchomoa line. Nikaendelea na safari zangu.
Nilipofika home nikawaza sana vipi niitumie au niiuze. Lakini badae nikakumbuka umuhimu wa line na kipindi kile ilikuwa ni ishu sana kurenew line kwaio ukipoteza simu na line ni kama umepoteza kila kitu. Basi nikaamua kuirudishia line ili nisome meseji nijue mtu aliyepoteza ni mtu wa namna gani, akili yangu ikanituma pengine anaweza akawa demu mkali hahahaa (jokes), kikubwa ilikuwa nione namna gani naweza kumrudishia line yake ila simu nibaki nayo. Lakini moyo wangu ulikuwa baridi mno nikaona ni kama namdhulumu mtu kitu kikubwa sana ile simu. Basi nikaamua tu akijitokeza mwenyewe nitampa simu. Basi nikawasha simu pale na kuiacha on ili mwenyewe akipiga nimwelekeze nilipo aifate au tuone namna ya kuifata. Kwenye kusoma soma meseji nikaja kugundua ile simu ilikuwa ni ya wageni pengine kutoka ulaya au marekani maana niliona jinsi walivyokuwa wanawasiliana na mwenyeji wao kwa emails na text messages (hakukuwa na wasap siku zile), tena mbaya zaidi walikuwa bado hawajaonana na walipanga wangeonana kesho yake, yaani iyo Jumatatu ambayo mimi nilikuwa nasafiri. Basi nikalala zangu.
Asubuhi nikajidamka kuanza safari nilikuwa naenda Morogoro kule turiani kikazi. Basi mpaka naanza safari ile simu haikupigwa. Nilipofika moro town wakati natafuta usafiri wa Turiani simu ile ikapigwa. Ile kupokea tuu naskia sauti ya jamaa wa kizungu ina sema” Oh thanks God he picked up!!”. Jamaa tukasalimiana pale akajitambulisha jina na kusema ile namba ni yakwake anahisi alidondosha simu ila hajui ni wapi, akaniambia mpaka nimeamua kupokea ina maanisha mimi sio mtu mbaya hivyo hana haja ya kujua niliipataje simu au line yake ila anachoomba tuu nifanye iwezekanavyo nimsadie aipate ile simu kwani ina mambo yake mengi sana aliyahifadhi napengine safari yake ya kuja Tz ingekuwa haina maana.
Nikamsikiliza pale kisha nikamwelezea mazingira niliyookota ile simu. Akasema nikweli walikuwa pale kwenye lile jengo kupata dinner (kwenye mezzanine floor ya jengo la pale ofsini kulikuwa na restaurant) kwenye mida ya sambili ndio waliondoka kurudi hotelini kwao. Yule jamaa alikuwa ni raia wa Sweeden (Kwenye hii story nitamwita Mswedy) na alinambia kuwa alikuja kikazi na wenzake. Nikamwambia sasa mimi nipo safarini Moro tunafanyaje ili aipate simu yake? Akaniuliza nitageuza lini nikamwambia baada siku tatu, akaniambia tuu basi atasubiri maana hapa Tz wangekaa wiki tatu hivyo baadhi ya program atazisogeza mbele mpaka nitakaporudi. Akaniomba namba yangu pale nikampa akasema tutawasiliana mpaka nitakavyorudi ila tu akasisitiza ile simu yake niizime tuu mpaka nitakapompa.
Basi mimi nikaendelea na mishe zangu baada ya siku tatu nikarudi. Mswedi hakunipigia kabisa kwa siku zote ambazo nilikuwa safarini. Nakumbuka Alhamis ndio niligeuza Dar boss akanambia nipumzike tuu ile Ijumaa ofsini niende Jumatatu. Basi ijumaa jioni kwenye saa kumi Mswedy akanicheki. Tukasalimiana pale akaniuliza kama nsharudi, nikamwambia yes nipo mjini. Akanipanga kama nina nafasi jioni ile niende kuonana nao wao watakuwa coco beach kuanzia saa12. Kwa kuwa nilikuwa sina ratiba yoyote ya maana wala kikwazo chochote cha kunibana nikaona wacha niende tuu na ukizingatia kipindi kile coco ilikuwa inabamba sana hasa usiku.
Basi nikajiandaa pale na nikachukua simu yake nikasepa kumfata Mswedi. Nilipofika coco pale ilikuwa kama saa moja hivi usiku basi nikampigia kwa ile namba aliyonicheki nayo akanielekeza alipo. Nilipofika alipokaa nikawatuka yupo na watu saba hivi, wazungu wanne (mmoja mwanamke) na wabongo watatu. Katika wale wabongo watatu wote walikuwa wanawake. Basi jamaa tukahug pale akafurahi sana. Sasa nikashangaa cha kwanza hata kabla sijakaa jamaa akaniuliza umekuja na simu? Mimi sikumjibu nilichofanya ni kuitoa tu nakumpa. Jamaa akaiwasha huku akicheka sana nikaona na wale wengine wanacheka kwa sauti yaani ile kama walikuwa kuna kitu wanashindana. Nikaona mara Mswedi anawaambia wenzanke haya nipeni sasa hiyo cash maana jamaa ameileta hii simu.
Kumbe wale jamaa bhana wakati wananisubiri walibet mimi sitaenda kuwapa ile simu na ahesabie maumivu. Yeye akabeti kwamba mimi nitaenda na simu yake ataipata hivyo wale wazungu walibeti euro 100 kila mmoja kumpa Mswedi na yeye alibeti angetoa euro 100 kuwapa wagawane. Kwakweli kilikuwa ni kitu cha kufurahisha sana na Mswedy kweli akapewa Euro zake 300 pale mmoja akasema atampa wakifika hotel. Basi Mswedy huku mimi na yeye tukiwa bado tumesimama akachukua zile euro na kuniwekea mfuko wa shati langu huku akisema kwa sauti “I think this money should be given to him” akimaanisha mimi. Kila mmoja akasapoti pale na nilipotaka kukaa akanika kauli kwa kuniambia “my friend this is not a request but an order”. Hata kama ungekuwa wewe ungefanyeje, nikashukuru pale nikakaa na utambulisho ukaendelea.
Basi tukafahamiana pale kifupi Mswedy na wenzake walikuwa wanatoka wizara ya mambo ya nje ya Sweeden na walikuwa kitengo cha international cooperation ambacho ndio kinahusika na kutoa misaada ya kifedha kwa nchi za dunia ya mabondeni huku. Waliniambia kwamba kilichowaleta hapa bongo kipindi kile ni kuja kufanyia tathmini mashirika flani ambayo alinitajia yenye reputation kubwa tuu hapa nchini. Hayo mashirika ni kati yay ale yaliyopata funding kubwa sana za kutekeleza program zao hapa Tz. So wao kama technical team ndio walikuwa zone ya East and Southern Africa. Hivyo akaniambia kwenye ile simu alihifadhi baadhi ya docs zake muhimu sana zitakazomsaidia kufanya kazi zake. Nikaja kufahamu pia wale wadada watatu wa kibongo wawili ni wenyeji wa wale wageni na mmoja ni kampani tuu.
Basi na mimi nikajieleza pale taaluma na shughuli yangu pale na maisha mengine yakaendelea. Basi kwa kuwa ilikuwa weekend tulikula bata pale kimtindo na mimi nikaclear bill moja niliyoona haina maumizu sana ili nisiwe mnyonge na hapo ukicheki nilikuwa na kama Euro 300 kwenye mfuko wa shati. Basi mazungumzo yakaendelea pale mmoja wa wale madada wakibongo akamuuliza Mswedy vipi kama nikimconnect Taidume kwenye program yetu pale ofsini maana nimemwona ni kijana mdogo lakini anauaminifu sana? Asee kwanza kiroho kilipiga paap! Mswedi akamwambia ‘I had the same thought but hesitated to intervene. However, I completely agree with you. I'm not sure about how Taidume will react to it! Now the ball was at my side, yaani kazi hii hapa mikononi mwangu eti ni mimi tu niseme nataka au sitaki dadeki. Can you guess what was my reply was?????????
Tukutane next time?
Au ngoja nimalizie tuu.
Kiukweli I was speech less. Ila nikajitutumua kumuuliza yule nikamwambia I would love to join, but I'm not sure if I can manage since I don't have any clue about the program you are talking about". Yule dada mbongo akaniambia based on what you have shared with us on what you are doing, I am quite sure you will manage. Basi akanipa abcd za hiyo program nikaona mbona haina kwere, after all kubadilisha mazingira ya kazi for other ni muhimu wakati mwingine. Basi tukaagana pale kwenye saa tatu hivi usiku. Wakati naondoka yule dada mbongo akanipa namba yake ili tuwasiliane ikiwezekana Jumatatu tuwasiliane. Mswedy naye akanisisitiza kesho ile team yote watajutana mahali kupata lunch so akanisisitiza sana na mimi niwepo.
Basi kesho yake baada ya maswala ya church service na kupumzika kidogo Mswedi akanicheki na kunielekeza eneo la tukio. Nilipofika pale nikawakuta watu wengi wengi ni dizaini kama ndio walikuwa wanaaga hivi wanaelekea Zambia kuendelea na kazi zao. Basi nikajumuika nao lunch pale na yule dada mbongo alikuwepo. Badae nikapa muda wa kuongea nae vizuri na akanipa mchongo wote wa ile ofisi ambayo nilitakiwa kwenda. Kifupi yule dada mbongo alikuwa ni consultant ambae kampuni yake ndiyo ilipewa kazi ya kusaidia mchakato wa kupata wafanyakazi kwa ajili ya hiyo program mpya, sasa wale wazungu pamoja na kufanya tathmini kwenye yale mashirika yatakayopewa fedha walitakiwa pia kumfanyia tathmini mtu ambay alipewa tender hiyo ya kutafuta wafanyakazi. Kigezo kikubwa pamoja na mambo mengine cha kupata wafanyakazi wa hiyo program ilikuwa ni pamoja na uaminifu maana ile kazi ilikuwa inahusika na mambo ya kugawa na kusimamia ruzuku/fedha kwa NGOs nyingine ndogondogo za hapa Tz. Kiufupi pale nilikuwa nimepata kazi bila hata kufanyiwa interview.
Ilipofika Jumatatu nikatengeneza excuse pale ofsini ili niende kuonana na yule dada mbongo ofsini kwake. Nikaanda CV yangu na kwenda nayo. Nilipofika yule dada japo alishaona nafit kufanya ile kazi lakini alischedule interview ili wiki inayofata nikafanye. Basi nikaendelea kudeal na majukumu yangu ya kazi pale ofsini kwa boss KJ kama kawaida. Baada ya kama wiki mbili tangu nifanyiwe interview na yule mdada mbongo nikapokea simu kutoka sasa kwenye ofisi mpya ambayo nitahitajika kwenda kufanyia kazi kwamba ninatakiwa nikafanye interview ya awamu ya mwisho. Kumbe utaratibu wao ni kwamba yule dada mbongo yeye akishafanyia watu interview anapendekeza top 3 yake na wale wenye kuhitaji wafanyakazi wanawaita kwa ajili ya kujiridhisha tu. Les say kwenye ile kazi walikuwa wanatakiwa wafanyakazi watatu basi yeye anapeleka top four then wale watachagua watatu. Badae nikaja kugundua sisi tulitakiwa wawili ila kule yalienda majina matatu ili wachuje wenyewe.
Basi muda ulipofika wa kupiga ile interview niliipiga fresh tuu. Uzuri kazi ni kama zile tu nilizokuwa nafanya kule kwa boss KJ ila vitu vitu vichache tu vilikuwa vinaongezeka hivyo interview ile haikuwa ngumu kwangu. Mpaka natoka pale interview room niliona kabisa hapa nimewapoteza hawa panelists. Baada ya wiki nikapokea rasmi offer letter ikinitaka kujoin the new office as soon as possible. Basi nikawaomba walau wanipe mwezi mmoja ili walau niweze kumalizia kazi zangu kule KJ ili nikiondoka niondoke kwa amani na nido uproffesional wenyewe. Wakanikubalia japo waliona ni kama nachelewa.
Nakumbuka soon nilipoconfirm ile kazi mpya nikaenda ofisini kwa boss kumuaga kumwambia kuwa nategemea kuresign. Boss alishtuka sana akaniuliza kama kuna tatizo nikamwambia hakuna akanibana sana labda kama ni ishu ya mshahara. Boss alisikitika sana na kiukweli hata mimi nilisikitika sana. Nikakumbuka jinsi alinivonitoa jalalani, nimefikia pale kwake sijui aa wala bee, pamoja na changamoto za hapa na pale ikiwemo ukali wake usiotabirika lkn alinisaidia sana Dr KJ kiunipa exposure na uzoefu kwenye career yangu. Kingine kama nilivosema Mr KJ hali yake kiafya haikuwa nzuri kabisa kila siku ilikuwa inatetereka. Hii ilipelekea majukumu yake mwngi mimi nndio nilikuwa nayafanya ilifika hatua nilimwakilisha mpaka kuingia kwenye vikao vya bodi. Ila ndio hivyo ilibidi tu akubaliane na ukweli kwamba naondoka. Pia boss KJ nasikia tangu awe Mkurugenzi pale hakuna mtu aliyewahi kuondoka mwenyewe ila wote waliondoka kwa kutimuliwa so nadhani hii ilimpa funzo funzo kwamba kuna siku nay eye anaweza akawa anamuhitaji mtu na akamkosa. Hata niliowaambia wafanyakazi wengine kwa kweli walisikitika sana. PS alipendekeza nifanyiwe sherehe ya kuagwa pale na kutafutiwa zawadi kitu kilikubaliwa nawote.
During the 9-month period in which I served as a Program Officer for Advocacy and Capacity Building under Dr. KJ, I acquired the following key skills:
- Training organization and facilitation skills
- Community mobilization and engagement skills
- Field supervision skills
- Project planning, implement and report writing skills
- Problem solving skills
- Project Monitoring and evaluation skills
Ndugu wajumbe tukutane katika season nyinginezo tuongelee uzoefu mpya kwani mazingira ya kazi yamebadilika. Wenye connection za kazi nitakuwa pia natoa summary ya key skills nilizogain kwenye kila kazi niliyopita hivo mkiona nafit feel free to PM me. Asanteni