Mambo tofauti tunayokutana nayo Madereva wa malori toka enzi

Mambo tofauti tunayokutana nayo Madereva wa malori toka enzi

Unachokileta wewe sasa ndiyo UBISHI wa kipuuzi. Hauna fact yoyte, siyo local wala official.
Nikufundishe tu eneo la Mpembampazi ni eneo ndani ya hifadhi ya Ipole, na palikuwa na kambi ya walina asali pale. Hilo eneo enzi za Mkapa kama sikosei ndiyo maajambazi waliwahi kuteka basi na kuwaimbisha abiria wimbo 'Mtaji wa Masikini ni nguvu zake mwenyewe'.
Ninaongea kitu ninacho kifahamu, ssiyo wewe na huko kujitia ujuaji wakati haufahammu kitu kuhusiana na unachojaribu kubisha.
Sasa ulikuwa unakataa nini mwanzoni?.
 
Tatizo huwa huwa mna story nyingi zenye chumvi mpaka haziliki. Mfano hapa pekee, story ya kweli hapa ni uwepo wa Pori na hao wanyama (Simba na Twiga), lakini Simba wakubwa kuliko uliowahi kuwaona (nalo nisibishe) pia hakuna pori linaloitwa Mpembampazi. Nimelina sana asali pande hizo hadi kule Inyonga


Wewe ni muha au unavinasaba vya watu wa kule.
 
Wewe unaleta ubishi kuwa hakuna twiga mweupe wala msitu wa mpembapazi kisa tu hujawahi kumuona huyo twiga na hujawahi kufika kwenye huo msitu, sasa huu kama sio ubishi wa darasa la 2 B ni nini, umechemka acha kupoteza muda kujustify maneno yako unazidi kuharibu.
Wewe kama ulikuwa chooni basi umekurupuka bila hata ya kujiswafi wakti ulikuwa unaharisha.
Unaweza kunionyesha niliposema hakuna Twiga mweupe?
Tafuta comment yangu humu, nimeielezea hiyo Pembampazi ilipo.
Usipende kuwalisha watu maneno
 
Tatizo huwa huwa mna story nyingi zenye chumvi mpaka haziliki. Mfano hapa pekee, story ya kweli hapa ni uwepo wa Pori na hao wanyama (Simba na Twiga), lakini Simba wakubwa kuliko uliowahi kuwaona (nalo nisibishe) pia hakuna pori linaloitwa Mpembampazi. Nimelina sana asali pande hizo hadi kule Inyonga
PakiJinja Hapa ulikuwa unasema hakuna pori gani na kule umethibitisha nini? au umekunywa chai na unga wa dona mkuu.
 
PakiJinja Hapa ulikuwa unasema hakuna pori gani na kule umethibitisha nini? au umekunywa chai na unga wa dona mkuu.
Umesoma ukaelewa? Tatizo lenu mnaacha sana detail muhimu ambazo ndiyo zinatoa sura ya kitu au tukio. Ningeweza kupandika uwepo wa 'Pori', labda ungenielewa.
Hoja yangu ni kwamba, hilo eneo'Mpembampazi' lipo ndani ya hifadhi ya Ipole
 
Hii ni kwa ufupi juu ya mambo mbali mbali tunayokutana nayo toka enzi mpaka leo hii.....Mengine hudhaniwa ni ya kutunga mengine yanahusishwa na uchawi na ushirikina hasa kwenye makampuni ......
Basi hapa nitakuwa nampeni stori tofauti tofauti juu ya vituko na mambo ambayo si ya kawaida sana katika ulimwengu huuu.

Miaka mingi imepita tulikuwa tunasafiri kuelekea Mpanda tuna lori limekula nundu ya kutosha mixer vipeto ..unajua njaa tena.....sasa njia tuliyopita ni ya Manyoni halafu unakata kushoto kuelekea Rungwa kisha unakata kulia kuitafuta KItunda....hapa tulipishana na basi la SABENA linatoka Tabora kueleke Mbeya hii njia kwa miaka hiyo ni njia dume kwelikweli na tulikuwa tunapita nyakati za kiangazi...aidha tulikuwa tunatembea na kila kitu muhimu kwa dharura ya aina yoyote ile.....

Kwa kifupi kuna pori linaitwa Mpembampazi hapo kuna Simba wakubwa kuliko simba wote niliokwisha kuwaona pia kuna Twiga weupe....anyway .......ilikuwa majira ya kama saa kumi na mbili jioni hivi machine inaunguruma mdogo mdogo taa nilikuwa nimewasha ingawa giza lilikuwa sio zito bado kulikuwa na mwanga.....zingatia ni ndani ya msitu(pori ) nene.....mara taa za gari zikawa zinajiwasha na kujizima zenyewe kama vile zimechanganyikiwa...halafu gari likazima ghafla....kwenye gari tulikuwa watu sita..mmoja kwenye kiti kushoto..... wawili kitanda cha chini...... na wawili kitanda cha juu.....wote tukawa kimya tunatafakari....kujaribu kupiga starter hata switch on haionyeshi.....tukawa kimya kama dk. moja hivi.....mara ukapita upepo wa baridiii upepo mkali kiasi halafu kimyaaa......mara tukasikia mlia shwaa shwaaa shwaa shwaaa kama vile kuna kitu kinaji buruza....

Kuangalia mbele tulishuhudia nyoka mweupe kama maziwa hana madoa doa ni mweupe tuu unene wake ni kama sadolin yaani diameter yake.....halafu kakatiza barabara kwa mbele....wote tuko kimya tunamuangalia tu....kichwa kikapotelea chakani lakini kiwiliwili bado kinakatiza barabarani....,,na mlio shwaa shwaa shwaaa.....duuuh...sasa cha ajabu zaidi mkiani alikuwa anawaka taa...taa ya rangi ya blue..na ina mwanga wa kutosha.....yaani mkia wake ulisimama juu kama mkia wa ng'e..halafu kwa juu kuna kama kakikombe ndio kuna kama jiwe hivi ndio linalotoa huo mwanga........bahati mbaya zamani hizo tulikuwa hatutembei na kamera.....
kwa kifupi baada ya joka kupotelea kichakani gari lilikubali kuwaka na tukaendelea na safari...sasa baada ya kufika Mpanda tukawahadithia jambo tulilolishuhudia......wakafurahi sana wakatukaribisha sehemu fulani kuna wazee wanakunywa pombe za kienyeji...walituhoji na kupata uhakika kabisa kwamba huyo nyoka wanamfahamu na kumuona ni bahati kubwa sana na huonekana mara moja baada muda mrefu sana na lile jiwe linalowaka taa ni jamii ya LULU....
.....ITAENDELEA>>>>>>>>
Mmeanza...
 
Maisha yamenifanya nitembee Sana hasa mapori ya Tanzania na yameniachia kumbu kumbu nzuri Sana.
20241219_070345.jpg
Huku milima ya rubeho umewahi kufika mkuu.
 
Back
Top Bottom