min -me
JF-Expert Member
- Jul 20, 2022
- 23,322
- 64,738
Napenda sana mapori na ukijaniView attachment 3182357Huku milima ya rubeho umewahi kufika mkuu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Napenda sana mapori na ukijaniView attachment 3182357Huku milima ya rubeho umewahi kufika mkuu.
Niliwahi kuwa na imani kama yako ila kuna vitu viliwahi kunikuta ndipo nikaamini akili zangu zilikuwa hazijakomaa bado japo nikijiona mjuaji mnoStory za kufikirika za uchawi, vibwengo, majini n.k ni tamu sana.
Binti stress za maisha zitakuua kila siku huwa nakueleza sanakuna Mahala nimesema halipo au halitambuliki? Nilichokikataa ni hadhi yake, haikuwa hiy iliyopewa
Mimi nimezunguka sana mkuu na hizo picha nilizopiga mwenyewe ninazo za kutosha.Napenda sana mapori na ukijani
Msaidieni huyo dogo maisha yamemchapa sana hofu yangu asije kuvuliwa ubingwa na mafirauniPakiJinja Hapa ulikuwa unasema hakuna pori gani na kule umethibitisha nini? au umekunywa chai na unga wa dona mkuu.
Kwa hiyo ukisha comment hivi ndiyo unajiona umekua labda mtu fulani hivi of your own dreams?Binti stress za maisha zitakuua kila siku huwa nakueleza sana
PimbiMkuu, wala sina shida na ukongwe wake, nisome vizuri nilichokielezea. Hivi mzazi wako sababu tu yeye ni mkongwe inawezekana akikwambia wewe ni wa kike na wewe ukakubali , halafu ukaanza kuwa wa kike kweli sababu mzazi ndiye amesema hivyo.
Sifurahii hali unayopitia nataka nikusaidieKwa hiyo ukisha comment hivi ndiyo unajiona umekua labda mtu fulani hivi of your own dreams?
KabisaUjuaji ukizidi mwishowe huwa ni kuf***a.
Hii ni kwa ufupi juu ya mambo mbali mbali tunayokutana nayo toka enzi mpaka leo hii.....Mengine hudhaniwa ni ya kutunga mengine yanahusishwa na uchawi na ushirikina hasa kwenye makampuni ......
Basi hapa nitakuwa nampeni stori tofauti tofauti juu ya vituko na mambo ambayo si ya kawaida sana katika ulimwengu huuu.
Miaka mingi imepita tulikuwa tunasafiri kuelekea Mpanda tuna lori limekula nundu ya kutosha mixer vipeto ..unajua njaa tena.....sasa njia tuliyopita ni ya Manyoni halafu unakata kushoto kuelekea Rungwa kisha unakata kulia kuitafuta KItunda....hapa tulipishana na basi la SABENA linatoka Tabora kueleke Mbeya hii njia kwa miaka hiyo ni njia dume kwelikweli na tulikuwa tunapita nyakati za kiangazi...aidha tulikuwa tunatembea na kila kitu muhimu kwa dharura ya aina yoyote ile.....
Kwa kifupi kuna pori linaitwa Mpembampazi hapo kuna Simba wakubwa kuliko simba wote niliokwisha kuwaona pia kuna Twiga weupe....anyway .......ilikuwa majira ya kama saa kumi na mbili jioni hivi machine inaunguruma mdogo mdogo taa nilikuwa nimewasha ingawa giza lilikuwa sio zito bado kulikuwa na mwanga.....zingatia ni ndani ya msitu(pori ) nene.....mara taa za gari zikawa zinajiwasha na kujizima zenyewe kama vile zimechanganyikiwa...halafu gari likazima ghafla....kwenye gari tulikuwa watu sita..mmoja kwenye kiti kushoto..... wawili kitanda cha chini...... na wawili kitanda cha juu.....wote tukawa kimya tunatafakari....kujaribu kupiga starter hata switch on haionyeshi.....tukawa kimya kama dk. moja hivi.....mara ukapita upepo wa baridiii upepo mkali kiasi halafu kimyaaa......mara tukasikia mlia shwaa shwaaa shwaa shwaaa kama vile kuna kitu kinaji buruza....
Kuangalia mbele tulishuhudia nyoka mweupe kama maziwa hana madoa doa ni mweupe tuu unene wake ni kama sadolin yaani diameter yake.....halafu kakatiza barabara kwa mbele....wote tuko kimya tunamuangalia tu....kichwa kikapotelea chakani lakini kiwiliwili bado kinakatiza barabarani....,,na mlio shwaa shwaa shwaaa.....duuuh...sasa cha ajabu zaidi mkiani alikuwa anawaka taa...taa ya rangi ya blue..na ina mwanga wa kutosha.....yaani mkia wake ulisimama juu kama mkia wa ng'e..halafu kwa juu kuna kama kakikombe ndio kuna kama jiwe hivi ndio linalotoa huo mwanga........bahati mbaya zamani hizo tulikuwa hatutembei na kamera.....
kwa kifupi baada ya joka kupotelea kichakani gari lilikubali kuwaka na tukaendelea na safari...sasa baada ya kufika Mpanda tukawahadithia jambo tulilolishuhudia......wakafurahi sana wakatukaribisha sehemu fulani kuna wazee wanakunywa pombe za kienyeji...walituhoji na kupata uhakika kabisa kwamba huyo nyoka wanamfahamu na kumuona ni bahati kubwa sana na huonekana mara moja baada muda mrefu sana na lile jiwe linalowaka taa ni jamii ya LULU....
.....ITAENDELEA>>>>>>>>
Wanaonimaliza kabisa ni wale wanaokuja na picha za mashamba ya chai na wengine chai kitokota jikoni🤣🤣😅Wajuaji washavamia shughuli 🙌🏻
Stori ikiwa nzuri ndio kabisa huwezi kamwe kuelewa maana.😀Hivi maana ya itaendelea kwenye true story huwa ni nini, kuwa hukupata muda wa kuimalizia au lazma watu tuwe tunabembeleza kuwa rudi umalizie ndio mambo yanakuwa byen
Ila ni sawa.. Ngoja tusubiri muendelezo wa huyo nyoka mwenye mkia kama wa nge