Dini Inasema Nini Kuhusu Ushoga?
Ushoga ni nini
Ushoga ni ile hali ya mwanaume au mvulana kujihusisha kingono na mwanaume au mvulana mwingine kinyume na maumbile. Yaani, uume kuingizwa ndani ya ****** wa mwanaume au mvulana mwingine, na kujamiiana kingono.
Uhusiano wa jinsia moja katika kipindi cha mababu katika Biblia
Mapenzi ya Mungu kuhusu ngono ya binadamu ni nini hasa? Mapenzi hayo yalidhihirishwa awali katika uumbaji wa binadamu wa kwanza: “Mungu aliwaumba wanaume na wanawake” (Mwanzo 1:27). UAMUZI WA MUNGU WA KUUMBA MWENZAKE WA KIKE KUTOKA KWA MWANAUME HAUKUWA JAMBO LA BAHATI MBAYA.
Mwanamke alikutana na vigezo muhimu vitatu kwa namna ya pekee: (1) “Siyo vyema mtu kuwa peke yake” (Mwanzo 2:18); (2) alihitajika msaidizi, anayefaa kwake (Mwanzo 2:18, 20); na (3) kizazi cha binadamu kingeendelea kupitia ujumbe wa kijinsia (Mwanzo 1:28).
Yesu na Paulo wote walisadikisha uelewa huo huo (Mathayo 19:4-6; 1Wakorintho 7:2).
Kwa hivyo, mwanamke alikuwa: (a) dawa ya kimungu ya upweke wa Adamu; (b) msaidizi kwake, anayefaa; na (c) njia ya kuendeleza kizazi cha binadamu. Hapa, tunaona mpangilio wa kimungu kwa binadamu wa aina yake.
MUNGU ANGEWEZA KUUMBA WANAWAKE WAWILI KWA AJILI YA ADAMU, LAKINI HAKUFANYA HIVYO. BADALA YAKE, ALIMUUMBA MWANAMUME MMOJA KWA MWANAMKE MMOJA, MAISHANI.
Hayo ndiyo mapenzi ya kimungu kwa “Mungu kumuumba mwanamume na mwanamke” (Mwanzo 1:27; Mathayo 19:1-9).
Muda mfupi baada ya Mungu kuanzisha utaratibu wa uumbaji, ambao alitangaza kuwa “mzuri sana” (Mwanzo 1:31), mwanadamu alianza kuingilia kati na kubadilisha mapenzi ya kimungu, na kubadilisha makusudio ya asili ya Mungu, kuhusu ngono ya binadamu.
Ushoga katika kipindi cha Musa
Mbali na kipindi cha kihistoria cha awali kabla ya Musa, kipindi mfumo dume, Mungu alifafanua wazi mapenzi yake katika suala hili alipowapa Sheria ya Musa taifa la Israeli. Katika sura inayoshughulika karibu kabisa na kanuni za ngono, maneno Yake ni wazi na dhahiri.
“Msiendelee na tendo la kulala na mwanaume kama unavyolala na mwanamke. Hilo ni chukizo. Msizitie uchafu nafsi zenu kwa mambo haya yote, nchi isije kuwatapika kama ilivyotapika mataifa yaliyokuwa kabla yenu” (Walawi 18:22-30). “Mtu akilala na mwanaume kama ilivyo kulala na mwanamke, wote wawili wametenda chukizo. Lazima wauawe. Damu yao iwe juu yao wenyewe” (Walawi 20:13).
Ushoga katika kipindi cha Agano Jipya
Ni dhahiri kuwa katika Agano Jipya ni sawa na katika kulaani kwake isiyoweza kusamehewa na isiyo na shaka ya shughuli za kimapenzi zisizo halali.
Mtume Paulo alihitimisha kuwa ni tabia “isiyostahili” na “isiyo ya kumcha Mungu” ya mataifa, na kusema: Kwa sababu hii, Mungu aliwaacha wafuate tamaa za uchafu. Kwa maana hata wanawake wao walibadilishana matumizi asili kwa yale yaliyo kinyume cha asili. Vivyo hivyo pia wanaume, wakiacha matumizi asili ya mwanamke, wakaongozwa tamaa zao wao kwa wao, wanaume kwa wanaume wakifanya mambo ya aibu, na kupokea ndani yao malipo ya kosa lao ambalo lilikuwa linalipwa. Na kama hawakutaka kumjua Mungu, Mungu aliwaacha wafuate akili iliyodhoofishwa, kufanya mambo ambayo hayafai, ambayo walijua hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wale wanaotenda mambo kama hayo wanastahili kufa, siyo tu wanafanya mambo kama hayo lakini pia wanawakubali wale wanaotenda (Warumi 1:26-32). Zingatia kuwa “Mungu aliwaacha” kwa “tamaa za uchafu.”
Kitabu cha Warumi kizima ni tangazo kuu la Agano Jipya la njia za kuhesabiwa haki kwa “kila mtu” (Warumi 1:16).
Kwa hivyo, kulaaniwa kwa ushoga katika Warumi wa kwanza ni sawa na kulaaniwa kwa mauaji, udanganyifu, tamaa ya mali, na dhambi nyingine zote zilizoorodheshwa humo na mtume Paulo.
Uchunguzi kuhusu Warumi wa kwanza unastahili kuzingatiwa. SI TU KWAMBA MUNGU ANAKASIRISHWA NA WALE WANAOSHIRIKI KATIKA TABIA YA USHOGA, BALI PAULO ANABAINISHA KWAMBA, ANAKASIRISHWA PIA NA WALE WANAOUNGA MKONO TABIA HIYO, HATA KAMA HAWASHIRIKI KATIKA SHUGHULI HIYO WENYEWE. MANENO NI: “WALE WAFANYAO MAMBO HAYA WANASTAHILI KUFA, SIYO TU WAFANYAO, BALI PIA WALE WANAORIDHIA WALE WAFANYAO” (WARUMI 1:32). KWA KIGEZO HIKI PEKEE, WENGI WAMEPATA KUTOKUBALIKA NA MUNGU.
Hukumu ya ushoga katika biblia
Ushoga ni ushetani asilimia 100. Ushoga ni zaidi ya uchawi. Ushoga ni uchafu wa ajabu. Ushoga ni laana. Ushoga ni nuksi, balaa. Kwa ufupi, ushoga haukubaliki kibiblia na kijamii.
Katika Biblia, kusudi la Mungu kuwaumba wanadamu lilikuwa ni ili wazae na kuongezeka, waijaze dunia, ili waitawale na kuimiliki. Ili kusudi hili litimie, Mungu alimuumba mwanamume na mwanamke. Kwa sababu mwanamume anatoa mbegu na mwanamke ana yai, likirutubishwa na mbegu ya mwanamume, mimba inatokea, na mtoto anazaliwa.
Mwanamume kwa mwanamume ni mbegu kwa mbegu, bila yai. Vivyo hivyo, mwanamke kwa mwanamke ni yai kwa yai, bila mbegu. Hawawezi kuzaa na kuongezeka, na kujaza dunia. Hiyo ni KINYUME kabisa cha kusudi la Mungu. Ndiyo maana ni chukizo kwa Mungu.
Katika kitabu cha Mwanzo 1:
26 Mungu akasema, na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. 28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
Katika Biblia yote, utaona kuwa mahali ambapo Mungu alimtaja mwanamume, alitaja pia mwanamke. Hakuna mahali ambapo Mungu ametaja mwanamume na mwanamume au mwanamke na mwanamke.
Hukumu kwa ushoga
Wengi wetu tunakumbuka historia ya kwenye vitabu vya dini kuhusu Sodoma na Gomora, uovu mkuu uliotawala katika miji hiyo ulikuwa ni uzinzi na ushoga, ambao leo tunatafsiri kama mapenzi ya jinsia moja.
Mfano wa Sodoma na Gomora kuhusu ushoga
Katika biblia, historia ya Sodoma na Gomora inapatikana katika Kitabu cha Mwanzo katika Agano la Kale la Biblia. Hadithi hii inaonesha jinsi Mungu alivyowashughulikia watu wa miji ya Sodoma na Gomora kutokana na uovu wao. Sodoma na Gomora ni miji miwili iliyokuwa katika eneo la Jordan ya leo, karibu na Bahari ya Chumvi. Watu wa miji hii walijulikana kwa uovu wao wa dhambi, na ukosefu wa haki.
Katika Kitabu cha Mwanzo sura ya 18, Biblia inaeleza jinsi Mungu alivyotuma wageni wa mbinguni (malaika) kwa Ibrahimu na kumwambia kwamba atakagua mji wa Sodoma kwa sababu ya uovu wa wenyeji wake.
Ibrahimu alijaribu kuwaombea watu wa miji hiyo kwa Mungu, akisema angeacha kuwaangamiza ikiwa atapata watu wa haki katika miji hiyo. Mungu akakubali kutoharibu miji hiyo ikiwa angeweza kupata japo watu kumi waadilifu. Lakini hakupata hata hao kumi.
Malaika wawili walikwenda Sodoma kumwokoa Loti, mpwa wa Ibrahimu, na familia yake kabla ya Mungu kuiharibu miji hiyo, lakini HATA HAO MALAIKA WALITAKA KUINGILIWA KIMWILI NA WATU WA MIJI ILE YA SODOMA NA GOMORA.
Malaika wale walionya familia ya Lutu kutokuangalia nyuma wakati mji ulipoharibiwa na moto kutoka mbinguni.
Lutu na familia yake walitii amri ya Mungu na kuondoka Sodoma. Hata hivyo, mkewe aligeuka na kuangalia nyuma kwa hamu kubwa ya kutaka kuona nini kitatokea na akageuzwa nguzo ya chumvi. Mungu aliangamiza kabisa miji ya Sodoma na Gomora kwa moto, na hakuna kitu kilichobaki isipokuwa magofu.
Biblia imetoa hukumu kwamba kulala na mwanamume mwenzako kama unavyolala na mwanamke ni machukuzo.
Dhambi ikifika mahali ikaitwa machukizo, maana yake ni lazima wanaofanya hivyo wauwawe.
Warumi 6:23: Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana.
Kibiblia, zipo dhambi ambazo Mungu anaweza kusamehe na asikuadhibu. Ila kuna mahali dhambi ikiitwa machukizo lazima uadhibiwe.
Kwa dhambi ambayo ni machukizo, Mungu huwa anaadhibu wanaotenda makosa haya.
Mambo ya Walawi 18: 22 Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. 23 Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko. 27 (kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi😉 29 Kwani mtu awaye yote atakayefanya machukizo hayo mojawapo, nafsi hizo zitakazoyafanya zitakatiliwa mbali na watu wao. Kukatiliwa mbali ni kuuwawa au kunyongwa.
Nini cha kufanya?
Biblia inasisitiza kila mara kwamba ushoga ni dhambi, hata kupitia vitabu vifuatavyo:
Mwanzo 19:1-13; Mambo ya Walawi 18: 22; Warumi 1:26-27; 1Wakorintho 6:9.
Warumi 1:26-27 inatufundisha kuwa, ushoga ni njia mojawapo ya kumkana na kutomtii Mungu.
Mtu anapodumu katika dhambi na kutokuamini Mungu, biblia inatuambia kwamba “Mungu huwaachilia” kutenda maovu zaidi ili wapate kujua ubatili wa maisha bila uwepo wa Mungu.
1Wakorintho 6:9 inasema kuwa mashoga hawataurithi ufalme wa Mungu.
Mungu haumbi mwanadamu mwenye tamaa ya ushoga. Biblia inatuambia mtu huwa shoga kwa sababu ya dhambi (Warumi 1:24-27), na pia kwa sababu ya uamuzi wake mwenyewe.
Mtu anaweza kuzaliwa na msukumo juu ya ushoga kama tu watu pia huzaliwa na msukumo juu ya fujo, ukorofi na dhambi nyinginezo. Hili halihalalishi dhambi yo yote inayofanywa na wanadamu. Je, mtu akizaliwa na msukumo wa hasira mbaya, ni halali aendeleze hasira zake mbaya? La, hasha. Hata kwa ushoga pia, si halali.
Kila dhambi ni chukizo kwa Mungu. Ushoga ni mojawapo ya mambo yaliyoorodheshwa katika 1Wakorintho 6:9-10, yatakayozuia mtu asiingie katika ufalme wa Mungu. Kulingana na Biblia msamaha wa Mungu juu ya shoga upo sawa na wa mzinzi, muabudu sanamu, muuaji, mwizi na kadhalika.
Hata hivyo, Mungu anaahidi uwezo juu ya kushinda dhambi, ikiwa ni pamoja na kuushinda ushoga, kwa wale wote watakaomwamini Yesu kwa wokovu wao (1Wakorintho 6:11; 2Wakorintho 5:17).
Tukumbuke kuwa Mungu aliwaumba wanadamu na kuruhusu mwanamume na mwanamke wawe na mahusiano ya kingono katika ndoa yao (Mwanzo 1:27-28; Mambo ya Walawi 18:22; Methali 5:18-19).
Biblia inashutumu ngono kati ya watu wa jinsia moja na kati ya mwanamume na mwanamke ambao hawajafunga ndoa (1Wakorintho 6:18). Tukumbuke kuwa Biblia inashutumu pia kumpiga punyeto mtu mwingine na ngono ya kinywa au ulawiti.
Mtu mwenye tamaa ya kufanya ngono na mtu wa jinsia yake anawezaje kumpendeza Mungu?
Biblia inasema kuwa: “Usiongozwe na mwili wako. Ua kila tamaa isiyofaa ya ngono” (Wakolosai 3:5). Ili kuua tamaa mbaya zinazosababisha matendo yasiyofaa, unahitaji kudhibiti njia yako ya kufikiri. Ikiwa kwa kawaida unajaza akilini mwako mambo yanayofaa, itakuwa rahisi zaidi kuondoa haraka tamaa mbaya (Wafilipi 4:8; Yakobo 1:14-15). Huenda isiwe rahisi mwanzoni lakini baada ya muda utafanikiwa. Mungu anaahidi kukusaidia ‘kufanywa upya katika nguvu zinazoendesha akili yako' (Waefeso 4:22-24).
Katika agano jipya, tofauti ya Agano la Kale, ambapo katika torati watu walikuwa wanauawa, Katika agano jipya, hakuna kuuawa kwa mtu kutokana na ushoga.
Baada ya Yesu kufa msalabani kwa ajili ya dhambi za mwanadamu, dhambi ya ushoga, kama ilivyo kwa dhambi zingine zote, adhabu yake hutolewa na Mungu mwenyewe, na si kuuawa mwanadamu kwa mwanadamu.
Hivyo, bado kuna nafasi ya kuacha kabisa ushoga kabla hasira ya Mungu haijakuwakia.
JAMBO LA KWANZA
Ushoga ulisababisha Mungu akateketeza miji mizima ya Sodoma na Gomora. Miji hiyo ikabaki magofu matupu. Hilo ni jambo kubwa kabisa. Je, tunahitaji ushahidi zaidi ya huo? Kuhitaji ushahidi zaidi ni kushindana na Mungu. Ni kumdhihaki na kuzidi kumchukiza.
Hivyo basi, jambo la kwanza ni KUKIRI KUWA USHOGA NI KINYUME CHA KUSUDI LA MUNGU. NDIYO MAANA NI CHUKIZO KWA MUNGU.
JAMBO LA PILI
Jambo la pili ni kuacha ushoga. Haijalishi unapenda ushoga kiasi gani, ni chukizo kwa Mungu. Dawa ni kuacha. Usiwe shingo ngumu, kama Waisraeli walivyoshupaza shingo hawataki kuacha kutenda dhambi wakiwa njiani kutoka Misri kuelekea nchi ya ahadi, ambapo Mungu aliwaua shingo ngumu wote, kati ya watu 603,550 kasoro 2 tu (Joshua na Kalebu) waliotoka Misri, na hao hawakufika nchi ya ahadi (Hesabu 1:46).
Kubali yaishe. Na ili uache ushoga, yupo Yesu Kristo, anaweza kukusamehe dhambi zako sasa, kabla hujakatiliwa mbali. Ni heri umgeukie Mungu, kwa sababu neema ya Mungu bado ipo.
Usione aibu. Nenda kwa Yesu. Nenda uokoke.
JAMBO LA TATU
Jambo la tatu ni kukimbilia kanisani, ukaeleze shida yako, na utaombewa.