Kuanzia uchaguzi wa 2010 kizazi kilikuwa kimebadilika, hivyo uhakika wa CCM kuendelea kushinda kihalali cheo cha urais uliondoka rasmi, ikabidi uchaguzi ule mbinu chafu zianze kutumika. Uchaguzi wa 2015 hali ikawa mbaya zaidi kwa CCM kwenye nafasi ya urais. Uchaguzi wa 2020 Magufuli akaamua kuharibu kabisa uchaguzi. Na ushahidi wa hayo upo,na iko siku utakaa wazi peupe.
Unapoanza kuona matokeo ya uchaguzi yanaleta malalamiko ya wazi kila mara, huku wanaofaidika na uchafu huo hawataki ubadilike, hapo ujue chama hicho kinaishi nje ya kizazi chake. Na kwasababu sasa box la kura linatoa matokeo yasiyo sahihi, ni wazi watu watalipuuza, huku wakitafuta njia mbadala, na machafuko ndio itakuwa njia sahihi ya mabadiliko hayo. Tunza hii post.