Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,648
Mahakama imeeleza kuwa uamuzi wa kiasi halisi kinacholipwa lazima ufanywe kwa kuzingatia njia na hali ya maisha ya baba. Mawasilisho na viambatanisho vinadhihirisha kuwa kabla ya kifo cha marehemu alikuwa akitoa kiasi kilichoombwa kutokana na uwezo na hadhi yake. Marehemu alikuwa baba mzazi wa watoto walioitwa.
Mahakama pia imesema kuwa Mwombaji ametaja biashara nyingi kuwa ni ushahidi wa mapato yanayotokana na biashara inayohusishwa na mirathi, hata hivyo watu aliyowaomba matunzo mbele ya mahakama ni wasimamizi wa mali za marehemu.
Mapato yanayotokana na mirathi ya marehemu si mali ya walalamikiwa pekee bali ni mali ya mirathi ambayo imeshughulikiwa mbele ya Mahakama ya Mirathi. Waliyohojiwa wangekuwa baba mzazi wa watoto Mahakama ingewashikilia vinginevyo.
Kwa kuwa hakuna ubishi kwamba mhojiwa kwa nafasi yake ya wasimamizi wamewajibika kuwakimu watoto mahitaji ya msingi, wanapaswa kuendelea na malezi ya watoto kulingana na uwezo na nafasi zao.
Pia, suala la pili la uamuzi ni suala la malimbikizo na amri inayowataka walalamikiwa kutoa matunzo kwa watoto waliotajwa hadi watimize umri wa miaka 18. Ni ukweli kwamba Sheria ya Mtoto ilitungwa ili kuhudumia ustawi wa mtoto. Hata hivyo, tangu awali ni lazima ieleweke kwamba usimamizi wa mali ya marehemu sio jukumu la kudumu.
Kutokana na maelezo ya pande zote, hakuna ubishi kuwa katika shauri la mirathi namba 39 la mwaka 2019 walalamikiwa waliotajwa waliteuliwa kuwa wasimamizi wa mirathi ya marehemu Dk. Reginald Abrahaman Mengi.
Kwa mujibu wa kifungu cha 109 cha mirathi na usimamizi wa Sheria ya Mali majukumu ya wasimamizi ni kukusanya na kusambaza mali za marehemu kwa warithi halali. Jukumu hilo linaisha mara baada ya wasimamizi kuwasilisha hesabu. Mapato ambayo mwombaji anaomba kutunza watoto wake hadi watimize umri wa miaka 18 yakitoka katika mirathi ya marehemu ambapo walalamikiwa ni wasimamizi tu na sio wamiliki.
Kesi ya uthibitisho ni mbele ya mahakama kuu kwa hivyo mahakama ya watoto sio mahakama inayofaa kwa mwombaji kuomba maombi haya. Kadhalika, mahakama hii haiwezi kuwaamuru walalamikiwa kama wasimamizi wa mali za marehemu walipe malimbikizo kutokana na jinsi marehemu alivyokuwa akitunza watoto wake enzi za uhai wake.
Marehemu alikuwa akitoa mahitaji ya watoto wake kwa vile alikuwa baba mzazi wa watoto waliotajwa, na njia na namna zake zilifanikisha mipango yake. Waliohojiwa si wazazi wa watoto, wao ni walezi tu na wasimamizi wa mali za marehemu.
Zaidi ya hayo, kwa kuwa kuna kesi zinazoendelea za mirathi ambazo zote zinalenga kuhakikisha mirathi ya marehemu inagawiwa kwa haki kwa warithi halali, ni vyema mwombaji kupeleka maombi yake mbele ya mahakama ya mirathi na siyo mahakama ya watoto.