Mkushi Da Gama
JF-Expert Member
- Jun 23, 2015
- 3,692
- 4,991
Duu Kumbe shetan Tumemkuta HapaVita ya mbinguni ilikuwa before Adam hajaumbwa. Shetani alishatupwa duniani na malaika zake. Shetani anajua principle za Mungu ndio maana ili aweze kupata kibali cha ku operate duniani ilibidi atumie mwili wa nyoka.
Kitabu cha mwanzo kina majibu yote
Wewe umenielewa vizuri, ukweli ndio huoHapa naona swala la uimbaji likiwa limeanza zamani asili ikiwa mbinguni na Kiongozi wa Kwaya baadae akatoswa, waimbaji wa nyimbo za kidunia unakuta mtu anasauti maridhawa tamu hadi unapagawa. Sijui kuna connection na ule msemo wa "Sauti ya kumtoa nyoka pangoni" Nyoka kama kwaya Master!!!
Sorry kama ni lugha ya mfano... Uhalisia wake ninini?
Kumbuka hapa hatukosoi (hatuna uwezo huo)
bali tunajenga mjadala wenye kuelimishana....
Kwahiyo ishu ya kutoa povu sidhani kama hapa ni mahali pake sahihi
Wanatheologia wa mtizamo kama huu hawa amini kama kweli kuna kitu kama Neno la Mungu zaidi ya wao kuamini haya yaliyopo kwenye biblia ni masimulizi au tunzi za watu fulani.Uhalisia wa hilo simulizi ni kukufahamisha na kukupa tahadhari Tu juu ya kani mbili kinzani katika mapito yako kama Mwanadamu_hamna la ziada
Wala sina tatizo katika hilo hata mimi naheshimu na nafahamu kuwa ni Kitabu kiliandikwa na watu wenye nia njema
Hapa na ndipo kwenye Tatizo na tatizo lenyewe linakuja juu ya uwelewa kati ya mtu na mtu
Itakuja tu pindi utakapoulazimisha mchicha kuwa msufi na kwale wa porini kuwa kuku wakufuga nyumbani
Ufunuo wa Yohana 12hivi maandiko yanayodai shetani sijui alitupwa toka mbinguni huwa yanatokea wapi?
mwenye andiko atusaidie hapa
Na ni vema kwa mtu yeyote kusoma hicho kitabu kama simulizi ili kuamsha udadisi ndani yake na kupata ukweliWanatheologia wa mtizamo kama huu hawa amini kama kweli kuna kitu kama Neno la Mungu zaidi ya wao kuamini haya yaliyopo kwenye biblia ni masimulizi au tunzi za watu fulani. Mimi ninavyo amini ni kwamba shetani yupo katika mambo mengi maovu kama kiwiliwili chake tu ila kichwa chake kipo katika dini.
.Yakobo 2
19 Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.
Hili linalotajwa hapa ni kundi fulani katika wanadamu linalo amini katika Mungu na kutetemeka hata hivyo bado wanabaki kuwa mashetani kwa jinsi ya kutenda kwao.
Swadakta,naona umenihepa vizuri sana,nilidhani ungeleta ile aya ya isaya ili nikupe somo.Ufunuo wa Yohana 12
7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;
8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
Swadakta,naona umenihepa vizuri sana,nilidhani ungeleta ile aya ya isaya ili nikupe somo.
Sijui kwanini yohana aliamua kutaja kisa cha ibilisi kutupwa toka mbinguni kuna duniani,
Mimi navyohisi,yohana alikopy unabii wa isaya,akafanya mabolesho kidogo,
Kwa sababu MTU unajiuliza kwanini kisa cha shetani kutupwa duniani kimekuja kutajwa mwishoni mwa maandiko,wakati kilitakiwa kuwepo katika kitabu cha mwanzo?
Kuna jambo hujalisoma vizur labda kwa mchangiaji mmoja juu hapo kwamba Mungu anajua vema mambo yatakayotokea mbeleni lakin hayazuii kwa sababu amemuumba mwanadam na kampa mamlaka ya kuchagua jema au baya Sasa Mwenyezi Mungu akiingilia mamlaka ya mwanadam au kiumbe chake atakua anavunja sheria na ye ni Mtakatifu hawez fanya hivo sana sana atatoa hukumu tuu juu ya maamuz ya kiumbe wakeakayaruhusu haya yatokee na wakati anajua mwisho wake kwanini asingezuia uumbwaji wa shetani
EzekielSwadakta,naona umenihepa vizuri sana,nilidhani ungeleta ile aya ya isaya ili nikupe somo.
Sijui kwanini yohana aliamua kutaja kisa cha ibilisi kutupwa toka mbinguni kuna duniani,
Mimi navyohisi,yohana alikopy unabii wa isaya,akafanya mabolesho kidogo,
Kwa sababu MTU unajiuliza kwanini kisa cha shetani kutupwa duniani kimekuja kutajwa mwishoni mwa maandiko,wakati kilitakiwa kuwepo katika kitabu cha mwanzo?
Ukisoma simulizi hilo bila mahaba ya kiitikadiInaandikwa kwamba..... Basi Bwana Mungu akasema... NA TUUMBE MTU kwa mfano wetu.. Hapa Bwana Mungu hakuwa pekeyake... Kulikuwa na mamlaka kamili ya kiroho juu mbinguni yaliyokuwa yanaongozwa na Mungu mwenyewe
Tafsiri nyingine ni kwamba tayari huko mbinguni kulikuwa na maisha mengine ya kiroho mpaka walipojadiliana kuumba mtu mwenyewe mwili wa nyama
Uumbaji mwingine wote wa vitu na wanyama viliumbwa na Mungu mwenyewe... Kwa uweza wake mkuu wa kutamka tu na ikawa.... Ilipofika kwenye kuumba MTU ndio cabinet ya mbingu ikahusishwa!
Kwanini kwenye uumbaji wa MTU Mungu hakufanya maamuzi binafsi Kama kwa wanyama mimea na vingine vyote? Kuna ufunuo wa ajabu hapa... Ni kwa vile alitaka awepo mtu kwa mfano WAO
Shetani anatajwa kama malaika mkuu... K vyeo vya kisasa unaweza kusema katibu mkuu, waziri mkuu ama msaidizi mkuu..... Huyu kwa asilimia 95 hufahamu yote ya mkuu wake wa kazi kwakuwa ndio kama mtendaji mkuu
Kwenye uumbaji Mungu aliumba kila kimoja na kinyume chake... N mpaka wakati huu Hakukuwa na kitu kinaitwa dhambi japo kabla ya uumbaji nchi ilikuwa kiza tena totoro kiwa(ukiwa) na vilindi vya maji vikiwa vimetuama juu ya uso wa dunia...
Ni kwenye uumbaji pekee wa Adam ndio Mungu aliishirikisha Mamlaka yake (shetani?) Vingine vyote alifanya mwenyewe.... Na hata alipoona Adam yu mpweke bustanini... Kwa mamlaka yake binafsi akamtengenenezea Adam msaidizi (Hawa/Eva?)
Kwanini hapa haikushirikisha cabinet yake? Je lilith ndio shetani mwenyewe? Nini kilimuudhi shetani mpaka kuamua kwenda kumdanganya msaidizi wa Adam ale tunda la mti wa kati? Mti wa ujuzi wa mema na mabaya? Je ni kwa vile hakushirikishwa kwenye kumtengeneza? Wivu? Kisasi? Kwanini hakumwendea Adam? Au kwakuwa aliasi mbinguni na kufukuzwa?
Na baada ya hapo dhambi ikaingia ulimwenguni na shetani akapewa ufalme wa giza.... Ndio hapa kinyume cha mbingu kinakamilisha uumbaji wote kiroho....
Je huu ulikuwa unabii au mpango wa Mungu? Kwanini shetani ana role kubwa sana kwenye dhana nzima ya kukengeuka kwa dunia, Adam na upili wa kiumbaji?
Tutafakari kwa pamoja... Inawezekana kabisa shetani tumdhaniaye na nyoka tumwonaye ni vitu vingine kabisa tofauti na uhalisia wa dhana nzima ya Eden, uumbaji, uasi, tunda la mti wa kati nk