Mamlaka ya kiroho ndani ya mbingu - je, yalikuwa na pande mbili?

Mamlaka ya kiroho ndani ya mbingu - je, yalikuwa na pande mbili?

Vita ya mbinguni ilikuwa before Adam hajaumbwa. Shetani alishatupwa duniani na malaika zake. Shetani anajua principle za Mungu ndio maana ili aweze kupata kibali cha ku operate duniani ilibidi atumie mwili wa nyoka.
Duu Kumbe shetan Tumemkuta Hapa
 
Kwann bible haijaeleza uumbaji wa Mwanzo kabla Ya uumbaji wa Adam....(haijaeleza hicho kizaz kilichooangamizwa )
 
Kitabu cha mwanzo kina majibu yote

Reason ya ku-quote si kwa ulichoki-comment hapo bt ili niku-notify direct instead ya ku-quote post #1 ambayo ni ndefu.

Kikubwa/kingine kinachotatiza hapa ni kwamba Mungu anajua kabla mambo hayajatokea so ina maana aliyajua yote hayo kuwa Shetani atakuja kuasi pia alijua kuwa atakuja kumuumba Adam, atamuongezea na msaidizi lakini baadae msaidizi atadanganywa and so on... then why akayaruhusu haya yatokee na wakati anajua mwisho wake kwanini asingezuia uumbwaji wa shetani kwanza ? Au pengine malaika hawakuumbwa na Mungu coz sioni sehemu ambapo panazungumzia uumbwaji wa malaika, though tunasema kila kitu kiliumbwa na Mungu.

Nikija katika suala la Ayubu kuna mambo yanafikirisha hapo, Mungu anajua kitu kabla hakijatokea so alijua Ayubu angeshinda lile jaribu na shetani anaujua vyema uwezo wa Mungu kwanini wasingefikia mwafaka wenyewe bila kumtesa huyu kiumbe for nothing wakati conclusion inafahamika?? Proof ya nini sasa wakati unajua conclusion??

Suala lingine pengine boundary iliyopo kati ya Mungu na shetani ni tofauti sana na vile tunavyofikiria maana mpaka shetani anaulizwa na Mungu kuwa "shetani umetoka wapi? Shetani anajibu natoka kuzungukazunguka duniani, katika kutembea huku na huko. Mungu tena anamuuliza Je umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu?" Can you imagine these conversations kwamba uhusiano wao ukoje kiasi cha kuulizana maswali na kujibizana huku sisi wengine tukijenga picha kubwa ya Shetani hawezi hata kumkaribia Mungu kwamba akimwona Mungu anakimbia, maana tunajua Mungu hachangamani na uchafu/uovu na tunajua shetani ni muovu ndio maana maandiko yanaandika "mwovu Shetani" lakini vipi hiyo conversation??

Suala lingine hapo kwa Ayubu, inabidi sasa watu watambue kuwa si kila anaekufa basi ni Mungu tu anaetoa uhai wa mtu huyu kama wengine wanavyoamini bali pia uhai wa wengine unatolewa na Shetani angalia hapa Mungu anamwagiza Shetani juu ya Ayubu "tazama yeye yupo mikononi mwake lakini tunza tu uhai wake" so ina maana shetani ana uwezo wa kugusa uhai wa mtu

Je kwa hapo tunaweza ku-conclude kuwa sio kila kifo kinachotokea ni mpango wa Mungu kama wengine wanavyoamin kuwa kila kifo ni mpango wa Mungu??

Na huku kukiwa na andiko lingine likisema mtu kufa kabla ya siku zake ni chukizo mbele za Mungu sikumbuki ni kitabu gani mwingine anaweza kusaidia hapo.

Kazi kwelikweli.
 
Hapa naona swala la uimbaji likiwa limeanza zamani asili ikiwa mbinguni na Kiongozi wa Kwaya baadae akatoswa, waimbaji wa nyimbo za kidunia unakuta mtu anasauti maridhawa tamu hadi unapagawa. Sijui kuna connection na ule msemo wa "Sauti ya kumtoa nyoka pangoni" Nyoka kama kwaya Master!!!
Wewe umenielewa vizuri, ukweli ndio huo
 
Sorry kama ni lugha ya mfano... Uhalisia wake ninini?

Uhalisia wa hilo simulizi ni kukufahamisha na kukupa tahadhari Tu juu ya kani mbili kinzani katika mapito yako kama Mwanadamu_hamna la ziada

Kumbuka hapa hatukosoi (hatuna uwezo huo)

Wala sina tatizo katika hilo hata mimi naheshimu na nafahamu kuwa ni Kitabu kiliandikwa na watu wenye nia njema

bali tunajenga mjadala wenye kuelimishana....

Hapa na ndipo kwenye Tatizo na tatizo lenyewe linakuja juu ya uwelewa kati ya mtu na mtu

Kwahiyo ishu ya kutoa povu sidhani kama hapa ni mahali pake sahihi

Itakuja tu pindi utakapoulazimisha mchicha kuwa msufi na kwale wa porini kuwa kuku wakufuga nyumbani
 
Uhalisia wa hilo simulizi ni kukufahamisha na kukupa tahadhari Tu juu ya kani mbili kinzani katika mapito yako kama Mwanadamu_hamna la ziada



Wala sina tatizo katika hilo hata mimi naheshimu na nafahamu kuwa ni Kitabu kiliandikwa na watu wenye nia njema



Hapa na ndipo kwenye Tatizo na tatizo lenyewe linakuja juu ya uwelewa kati ya mtu na mtu



Itakuja tu pindi utakapoulazimisha mchicha kuwa msufi na kwale wa porini kuwa kuku wakufuga nyumbani
Wanatheologia wa mtizamo kama huu hawa amini kama kweli kuna kitu kama Neno la Mungu zaidi ya wao kuamini haya yaliyopo kwenye biblia ni masimulizi au tunzi za watu fulani.

Mimi ninavyo amini ni kwamba shetani yupo katika mambo mengi maovu kama kiwiliwili chake tu ila kichwa chake kipo katika dini.
.Yakobo 2

19 Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.

Hili linalotajwa hapa ni kundi fulani katika wanadamu linalo amini katika Mungu na kutetemeka hata hivyo bado wanabaki kuwa mashetani kwa jinsi ya kutenda kwao.
 
Ndiyo maana tunakatazwa kwa nguvu zote kuhoji mambo yaliyopo kwenye vitabu vya dini...

Tunahimizwa kuamini na kuabudu pasipo kuhoji wala kukosoa... vinginevyo ingekua hatari sana... mambo mengi ukiyafikiria hayaleti maantiki...


Cc: mahondaw
 
hivi maandiko yanayodai shetani sijui alitupwa toka mbinguni huwa yanatokea wapi?
mwenye andiko atusaidie hapa
Ufunuo wa Yohana 12
7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;

8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.

9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
 
Wanatheologia wa mtizamo kama huu hawa amini kama kweli kuna kitu kama Neno la Mungu zaidi ya wao kuamini haya yaliyopo kwenye biblia ni masimulizi au tunzi za watu fulani. Mimi ninavyo amini ni kwamba shetani yupo katika mambo mengi maovu kama kiwiliwili chake tu ila kichwa chake kipo katika dini.
.Yakobo 2
19 Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.
Hili linalotajwa hapa ni kundi fulani katika wanadamu linalo amini katika Mungu na kutetemeka hata hivyo bado wanabaki kuwa mashetani kwa jinsi ya kutenda kwao.
Na ni vema kwa mtu yeyote kusoma hicho kitabu kama simulizi ili kuamsha udadisi ndani yake na kupata ukweli

Kuliko mwenye kusoma 'kama neno la Mungu' _huyo atakuwa kajitia pingu ya kutohoji kitu na kufisha udadisi ndani yake kwakua kwake yote ni heri

Na Imani bila kuhoji ni Upumbavu
 
Ufunuo wa Yohana 12
7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;

8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.

9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
Swadakta,naona umenihepa vizuri sana,nilidhani ungeleta ile aya ya isaya ili nikupe somo.

Sijui kwanini yohana aliamua kutaja kisa cha ibilisi kutupwa toka mbinguni kuna duniani,

Mimi navyohisi, yohana alikopy unabii wa isaya,akafanya mabolesho kidogo,
Kwa sababu MTU unajiuliza kwanini kisa cha shetani kutupwa duniani kimekuja kutajwa mwishoni mwa maandiko, wakati kilitakiwa kuwepo katika kitabu cha mwanzo?
 
Swadakta,naona umenihepa vizuri sana,nilidhani ungeleta ile aya ya isaya ili nikupe somo.
Sijui kwanini yohana aliamua kutaja kisa cha ibilisi kutupwa toka mbinguni kuna duniani,
Mimi navyohisi,yohana alikopy unabii wa isaya,akafanya mabolesho kidogo,
Kwa sababu MTU unajiuliza kwanini kisa cha shetani kutupwa duniani kimekuja kutajwa mwishoni mwa maandiko,wakati kilitakiwa kuwepo katika kitabu cha mwanzo?

Ni hivi tu mkuu kwamba baada ya mambo yote kukamilika ndipo Mungu aliwafunulia manabii waliokuwepo wakati huo siri zake. Kuna mambo Mungu aliyoyafanya siri na kuyawekea mhuri yafungwe hadi kwa wakati uliokusudiwa.

Ndipo kwa huo wakati Mungu huvunja huo mhuri na siri kuwa wazi kujulikana. Kristo Yesu katika kisiwa cha Patmo alimfunulia Yohana Mambo yaliyokuwa kabla na yoliyokuwepo kwa wakati wake na yatakayokuja baada yake.
Hivyo ni dhahiri alionyeshwa shetani alivyotupwa, yupo wapi na ni jinsi gani atakavyomalizwa.

Ufunuo wa Yohana 1
19 Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo.
 
WAIDH-QAALA RABBUKA LIL-MALAAIKATI INNII JAAILUN FILL ARDHWI KHALIFAH, QAALUU-ATAJ-ALU FIIHAA MANYUFSIDU FIIHAA WAYASFIKU DDIMAA-A, WAQAALA - LMALAAIKATI INNY AALAMU MAALAA TAALAMUUN(SURATUL- BAQARAH).
TAFSIRI: Na alipowaambia mwenyezi mungu malaika wake kuwa mimi nataka niumbe mwanaadamu ili akawe kiongozi katika ulimwengu, malaika wakamkatalia wakamwambia kuwa huyo atakwenda kufanya ufisadi na kumwaga damu katika ulimwengu, mwenyezi mungu akawaambia mimi najua zaidi ya munayoyajua.

Haya ni majadiliano kati ya Allah na malaika zake wakati Allah anataka kumuumba Adam.

Na kupitia uthibitisho huu ni wazi kuwa Allah kuwaambia malaika halikuwa shauri na mwenyewe alikuwa anataka kutimiza malengo yake juu ya kuumba kiumbe ambacho ni bora kuliko viumbe vyote alivyoviumba, na ili kiwe bora ni lazima akipe hadhi ya juu zaidi kuliko viumbe wengine, na malaika kukataa kwao kuumbwa kwa mwanaadamu ndio mwanzo wa wao kujishusha mbele ya adam kwani aya zinazofuatia zinaonesha mwisho wa siku Allah anawaamuru malaika wamsujudie adam, na Ibilisi alikataa kwa sababu yeye alikuwa ni part of the plan, alikuwa ni kama messenger ambae atafuatana na adam kuja duniani kwa kumpa majaribu adam na kizazi chake, na ukiangalia ni wazi adam hakuumbwa kwa ajili ya kukaa peponi na ibilisi kumshawishi adam ale tunda yote ni part of the plan, kwani mwanzo kabisa Allah alivyowaambia malaika kuwa anataka kuumba adam akawe khalifa ktk ulimwengu ilikuwa hata adam mwenyewe hajaumbwa.

So majibu ya maswali yako yote kayaangalie suratul- baqara hapo nimekupa kwa ufupi tu.

Pia nataka nitoe angalizo kuwa mwenyezi mungu hapangiwi na anajua anachokifanya kuna mambo anayafanya kwa sababu zake na kuonyesha utukufu wake, mungu hapingwi na amri zake lazima zitekelezwe, na anajua mwanzo na mwisho wa kila alichokiumba.

Back to the topic binaadamu lazima atambue thamani na utukufu wake kwa viumbe vyote kuanzia malaika, wanyama na kila kilichomo ktk mbingu na ardhi kimeumbwa kwa ajili ya kumtumikia yeye, kwa hiyo kama unataka urejeshe ufalme wako wewe mwana wa adam lazima utambue nafasi yako kwanza kama kiongozi, na hii ni kwa wanaadam wote bila kujali rangi, dini au kabila kila binaadamu ni kiongozi na anapaswa kuishi kiuongozi, dini ni mifumo tu ya maisha lakini mwisho wa siku hukumu zote ni kwa mungu alietuumba kabla ya kukejeli imani za wenzako jiangalie wewe kwanza imani yako inakupa uhuru wa kuitambua nafsi yako ya kiuongozi na kwa kiasi gani inakupeleka karibu na mola wako bila ya kuwa na khofu ya viumbe wenzako wanaokurudisha nyuma na kukukatisha tamaa kila siku wakiongozwa na muovu mkuu ibilisi.
 
akayaruhusu haya yatokee na wakati anajua mwisho wake kwanini asingezuia uumbwaji wa shetani
Kuna jambo hujalisoma vizur labda kwa mchangiaji mmoja juu hapo kwamba Mungu anajua vema mambo yatakayotokea mbeleni lakin hayazuii kwa sababu amemuumba mwanadam na kampa mamlaka ya kuchagua jema au baya Sasa Mwenyezi Mungu akiingilia mamlaka ya mwanadam au kiumbe chake atakua anavunja sheria na ye ni Mtakatifu hawez fanya hivo sana sana atatoa hukumu tuu juu ya maamuz ya kiumbe wake
 
Ezekiel
Swadakta,naona umenihepa vizuri sana,nilidhani ungeleta ile aya ya isaya ili nikupe somo.
Sijui kwanini yohana aliamua kutaja kisa cha ibilisi kutupwa toka mbinguni kuna duniani,
Mimi navyohisi,yohana alikopy unabii wa isaya,akafanya mabolesho kidogo,
Kwa sababu MTU unajiuliza kwanini kisa cha shetani kutupwa duniani kimekuja kutajwa mwishoni mwa maandiko,wakati kilitakiwa kuwepo katika kitabu cha mwanzo?
Ezekiel
28 :13 - 19

13 Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari.

14 Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto.

15 Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako.

16 Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto.

17 Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama.

18 Kwa wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao.

19 Wote wakujuao kati ya kabila za watu watakustaajabia; umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele

Nadhani umepata picha halisi ya shetan kutupwa kutoka mbinguni
 
Mshana Jr umeandika mambo ya kufikirika sana humu mkuu. Mbaya zaidi your biasness is transparent. Umeandika ukiwa tayari una imani yako - Yesu ni Mungu na Utatu Mtakatifu. Kosa.
 
Inaandikwa kwamba..... Basi Bwana Mungu akasema... NA TUUMBE MTU kwa mfano wetu.. Hapa Bwana Mungu hakuwa pekeyake... Kulikuwa na mamlaka kamili ya kiroho juu mbinguni yaliyokuwa yanaongozwa na Mungu mwenyewe
Tafsiri nyingine ni kwamba tayari huko mbinguni kulikuwa na maisha mengine ya kiroho mpaka walipojadiliana kuumba mtu mwenyewe mwili wa nyama
Uumbaji mwingine wote wa vitu na wanyama viliumbwa na Mungu mwenyewe... Kwa uweza wake mkuu wa kutamka tu na ikawa.... Ilipofika kwenye kuumba MTU ndio cabinet ya mbingu ikahusishwa!
Kwanini kwenye uumbaji wa MTU Mungu hakufanya maamuzi binafsi Kama kwa wanyama mimea na vingine vyote? Kuna ufunuo wa ajabu hapa... Ni kwa vile alitaka awepo mtu kwa mfano WAO
Shetani anatajwa kama malaika mkuu... K vyeo vya kisasa unaweza kusema katibu mkuu, waziri mkuu ama msaidizi mkuu..... Huyu kwa asilimia 95 hufahamu yote ya mkuu wake wa kazi kwakuwa ndio kama mtendaji mkuu
Kwenye uumbaji Mungu aliumba kila kimoja na kinyume chake... N mpaka wakati huu Hakukuwa na kitu kinaitwa dhambi japo kabla ya uumbaji nchi ilikuwa kiza tena totoro kiwa(ukiwa) na vilindi vya maji vikiwa vimetuama juu ya uso wa dunia...
Ni kwenye uumbaji pekee wa Adam ndio Mungu aliishirikisha Mamlaka yake (shetani?) Vingine vyote alifanya mwenyewe.... Na hata alipoona Adam yu mpweke bustanini... Kwa mamlaka yake binafsi akamtengenenezea Adam msaidizi (Hawa/Eva?)
Kwanini hapa haikushirikisha cabinet yake? Je lilith ndio shetani mwenyewe? Nini kilimuudhi shetani mpaka kuamua kwenda kumdanganya msaidizi wa Adam ale tunda la mti wa kati? Mti wa ujuzi wa mema na mabaya? Je ni kwa vile hakushirikishwa kwenye kumtengeneza? Wivu? Kisasi? Kwanini hakumwendea Adam? Au kwakuwa aliasi mbinguni na kufukuzwa?
Na baada ya hapo dhambi ikaingia ulimwenguni na shetani akapewa ufalme wa giza.... Ndio hapa kinyume cha mbingu kinakamilisha uumbaji wote kiroho....
Je huu ulikuwa unabii au mpango wa Mungu? Kwanini shetani ana role kubwa sana kwenye dhana nzima ya kukengeuka kwa dunia, Adam na upili wa kiumbaji?

Tutafakari kwa pamoja... Inawezekana kabisa shetani tumdhaniaye na nyoka tumwonaye ni vitu vingine kabisa tofauti na uhalisia wa dhana nzima ya Eden, uumbaji, uasi, tunda la mti wa kati nk
Ukisoma simulizi hilo bila mahaba ya kiitikadi

Hutoshindwa kutambua kuwa shetani ndiye Mungu mwenye

Kulingana na hilo simulizi_ mwanadamu alikuwa anaishi kama hayawani akiwa bustanini(Eden) nimejuaje.?

Ni baada tu ya kula Tunda akaanza kuhisi Yu uchi..!? Ikiwa na maana akajitambua..!?

Umungu ukawaingia Adamu na hawa kama walivyo ambiwa na anayeitwa shetani..!? Kumbe naye mkweli eenh.[emoji39]

Hivyo kama waliweza kujitambua baada ya kula Tunda inaonesha hapo kabla mwanzoni walikuwa malofa bila ubishi

Kwa mantiki hii ni kwamba shetani huyo kwao alikuwa ni msaada wa kuwatoa kifungoni(uzwazwa)

Na si kama Adui kama wanavyoaminishwa watu wengi wanaolishwa maana kupitia masomo ya mwengine

Maana yake bora ni lipi.!?

Kati ya kuishi milele kama hayawani_ au kwa muda mfupi ila ukijitambua...!?

Mpaka hapa ni kwamba Uyo anayeitwa Adamu hakukosea kufanya maamuzi[emoji818]

Na ukiwa huru katika tafakari hutoshindwa pia kutambua kuwa ilikuwa ni makusudi la aliyeanzisha huo uhai katika pahala hapo

Ni kama igizo jengine la mind evolution (level 1 to 2) kwa huyo kiumbe anayeitwa Adamu

Ila katika hila ya huyo Mungu kujiita shetani....[emoji3][emoji16]

Ngoja niishie hapa nisije nikakera wengi
 
Back
Top Bottom