Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yatangaza kuifungia JamiiForums

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yatangaza kuifungia JamiiForums

Mkuu maandamano ramani Iko hivi yafanyike usiku saa mbili mpaka saa tatu usiku kwenye Giza hiyo vagalanti hawato kuja sahau


Ask deal of million dollars, kwishaa,
usiku ni hatari mzee waharifu na baadhi ya watu wasojielewa wanaeza fanya uhalifu kuvunja maduka na kuiba mali za watu angalau mchana kweupe
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesitisha Leseni ya Maudhui Mtandaoni ya JamiiForums kwa muda wa siku 90 na kuzuia upatikanaji wa jukwaa hilo, kwa maelezo ya kukiuka Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu maudhui mtandaoni

TCRA imesema uamuzi huu umetokana na JamiiForums kuchapisha taarifa ya Mwanasiasa Humphrey Polepole kuhusu Rostam kumiliki mgodi wa makaa ya mawe kwa asilimia 70 na taarifa za uhusiano kati ya Rais wa Tanzania na "Mfanyabiashara" Wicknell Chivayo bila kuzingatia mizania.

Kwa mujibu wa TCRA, JamiiForums ilishindwa kutafuta maoni ya Mamlaka husika/Msemaji wa Rais/Serikali, kuthibitisha uhalisia wa picha (za Rais na Chivayo) zilizotumika, na hivyo kuuaminisha Umma taarifa za upande mmoja.

Aidha, TCRA imeeleza kuwa jukwaa la JamiiForums halikudhibiti maudhui yenye lugha ya matusi, kashfa na kejeli dhidi ya Rais wa Tanzania, na kuendelea kuhifadhi maudhui hayo ambayo bado yanapatikana kwa umma.

TCRA imeongeza kuwa maudhui hayo yanakinzana na mila, desturi na utamaduni wa Kitanzania, hivyo kuhatarisha mshikamano wa kitaifa, amani na taswira ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

View attachment 3466708
View attachment 3466706
View attachment 3466707
TCRA ni chawa tu kama chawa wengine, baada ya kushindwa kumteka ndiyo wanakuja na vimbwanga uchwara hivi.
 
usiku ni hatari mzee waharifu na baadhi ya watu wasojielewa wanaeza fanya uhalifu kuvunja maduka na kuiba mali za watu angalau mchana kweupe
Mkuu hata mchana ni yaleyale si kama wakenya tu, labda maandamano ya mchana ya amani tumtangulize gwajima member mbele watajuana wao si vitengo wote


Ask deal of million dollars, kwishaaa
 
The internet is the greatest tool democracy ever invented.

You can not keep information under wraps anymore, because technology is impossible to control.


By Tucker Carlson
Cancelled on FOX NEWS, available on YOUTUBE
 
Hahaha mkuu mbona wanasema Isha fungiwa mi bado ipo poa au


Ask deal of million dollars, kwishaaa
 
Tuheshimu sheria
Serikali, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na CCM ndiyo wanapaswa kuwa mfano wa kuheshimu sheria, waache kuteka na kuua watu bali kila mwenye makosa apelekwe mahakami na mahakama ziache kupokea orders kutoka kwa watawala wasiojua sheria badala yake wakumu kwa haki.
 
Bado tu hamja funga mnasubili nini sasa, si mfunge ili mrizike


Ask deal of millions dollars, kwishaaaa
 
Hata Instagram hapaja fungwa bado mpaka muda huu


Ask deal of millions dollars ,kwishaaaa
 
Pamoja na madhaifu yake, Sikumbuki kama Jamii Forums iliwahi kufungiwa enzi za JPM

Huu utawala, naona hautaki kabisa Uhuru wa habari [emoji119]
Uchaguzi wa 2020 kidogo tu kulikua na mvutano mkali kati ya Melo na sirikali, kuna moment tulianza ingia na VPN huku JF na Tweeter huo mwaka mbona, japokua haikutoka official notes kama hii kwa JF kuzimwa...
 
Back
Top Bottom