Inaonekana kuna dili, tenda nyingi sanachafu, mambo makubwa mengi ya hovyo Ndugu Wicknell Chivayo na kampuni zake wamejihusisha nayo, mambo kama dili / tenda za silaha, utakatishaji pesa, uuzaji rasilimali za nchi, dili za kuchapisha karatasi za uchaguzi, jinsi ya kuiba uchaguzi, jinsi ya ku-inflate tenda, kupiga cha juu, umeme, maji, gas na ufisadi wa aina nyingine.
Hapa wanasema amepewa tenda ya kuchapisha karatasi za uchaguzi na vifaa vingine vyote vya uchaguzi wa wabunge, madiwani na Rais Tanzania 2025.
Tunaomba wahusika wathibitishe kwamba ni kweli au sio kweli kwamba Lebone litho printers ndio watachapisha karatasi (ballot paper) na vifaa vyote kwenye uchaguzi wa 2025.
Kama ni kweli kwanini wamewapa tenda kampuni yenye historia mbaya, very bad track record na tuhuma za ku- inflate price, kutoa rushwa na kuiba chaguzi kwenye nchi za Mozambique, Namibia na Zimbabwe kufanya kazi hii?
Zambia waliamua kuvunja mkataba kutokana na tuhuma zinazowakabili.
Huu mchakato ulifuata due process? Hawajatupiga? Vipi kuhusu integrity of the ballot papers?
Tunaomba wahusika wathibitishe au kukanusha kwamba Wicknell Chivayo ndiye linkman, dalali au hahusiki na uchaguzi Tanzania?
Kama anahusika na hii kampuni amelipwa kiasi gani kwa kazi yake ya udalali na serikali ya Tanzania?
Ni kweli hakuna conflict of interest kutokana na ukaribu wake na Rais wa Tanzania na Wicknell Chivayo
na hii kampuni inayochapisha hizo karatasi za kupiga kura?
Tunaomba ufafanuzi kutoka mamlaka husika ili kuondoa hii sintofahamu.
Soma hapa
gambakwe.com
View: https://www.instagram.com/reel/DOSw22CjTxd/?igsh=MWo2NW96ODYweHRhZA==
View: https://www.youtube.com/live/N8g-TC5U8Rs?si=h7ybzGzes5N9awSM
Leaked documents and voice notes suggest that SA company, Ren-Form and its politically connected partner, Wicknell Chivayo inflated a tender for the Zimbabwean Electoral Commission by 235%.