Mamlaka ya Usalama wa Anga Tanzania (TCAA) imewataka wamiliki wa 'drones' kuzisajili ndani ya siku 4

Umeeleweka mkuu
 
Hivi tunaelekea wapi jamani.
Yote hiyo ni udhibiti ili wapinzani wakati wa kampeni wasipate coverage yoyote maana hizi drone ndizo zinaweza kupiga picha za watu wengi kwa usahihi kabisa. Wanataka kudhibiti wapinzani wakose picha za aina hiyo ili ionekane hawana watu.

Wamefanikiwa,redio,TV zote, wamezuia magazeti,sasa ni drones.

Mimi naona bora wakati wa ukoloni kwakua unajua tunafanyiwa hivyo na watu baki!
 
Hiyo sentensi ya mwisho โ€œ.......ask for permission from police and local authority.....โ€ ndio mwisho wa kila kitu. Hao ndio watakaomnyima mtu kibali na wakiona drove wanamkamata anayei-control!!

Huu ndio mwisho wa kutoa ushahidi kwa mambo kadhaa. Wezi wa kura wakiwa na mabox hawataki kuonekana wanafika kituoni. Vurugu kwenye mikutano zisiwe na ushahidi!!

Tumefikia pabaya sana!!
 
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imewataka wamiliki wa ndege zisizo na rubani (drones) kuhakikisha zimesajiliwa ifikapo Agosti 28, 2020, vinginevyo watachukuliwa hatua. Kanuni za TCAA zinataka mtu au kampuni kuomba kibali kabla ya kuingiza, kusajili na kutumia drone.

cloudstvtz

Kwa mbali naanza sasa kuona hata humu 'Vijiweni' tunamokaa tutawekewa Sheria 'Kandamizi' hakuna Kuwazungumzia 'Wapinzani' bali ni Wao tu.
 
hapana mkuu. Serikali inafanya kazi yake. Vinatakiwa viwe monitored otherwise vinaweza vikaleta madhara vikirushwa ovyo ovyo. Anga ni mali ya serikali na lazima waangalie usalama pia. Drones zinafanya kazi nyingi sana siku hizi hata kubeba mabomu.
Au mzigo wa madawa ya kulevya unahamishiwa nyumba nyingine kukwepa mkono wa sheria au kumtafutia mtu kesi ya madawa ya kulevya.
 
Ohoooooo... Kwani hii sheria ni mpya? Na why wamechelewa hivi.
 
7.Drone inaweza kuwabaini wasiojulikana wakiwa wanafanya tukio la uhalifu.
 
๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ
 
Kwaiyo adi za watoto ambazo hazina camera zinaitaji kusajiliwa wasije muingiza mwanangu kwenye kesi ya uhaini bure?
Inabidi uende TCRA wataalam wao wakupe maelekezo limit ya kupaa juu mwisho futi ngapi n.k.
Pia maeneo gani hupaswi kurusha hiyo drone, unapewa kibali hakuna shida yeyote kama ukifuta mashariti hayo na kurusha kwenye eneo la nyumbani kwako tu.
 
Ni kweli mkuu, usajili utasaidia na kupunguza hayo madhara. Lakini pamoja na usajili, bado kuna uwezo wa drone kutumika kufanya yote hayo. Kwa mfano bunduki zinasajiliwa lakini watu wana fyatuliwa kila leo!! Ila kusajili ni Sawa!
 
Si zinasajiliwa? Si kukatazwa kutumika.
Labda wanaohofia kuna watu wataingiza siasa katika kutoa vibali vya kutumia kwenye matukio kama haya.
Maana bongo napo siasa na ukada kila sehemu.

Hapa serikali wawe fair wasijiingize kwenye kupendelea kundi lolote lile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ