Inahitajika kujadilika na watu kutoa mawazo ya kuona kama kuna ulazima wa kuwa na vyama vya aina hii na kama viwepo basi viongozwe kwa taratibu gani. Kufuta bila kujadiliana au kutoa nafasi kwa mawazo mbadala kutolewa ni kuwa na uhodhi wa fikra.
Mzee Mwenzangu, hivi vyama vimekuwepo mingi si kwamba ni jambo geni.
Tatizo linalojitokeza ni ukosefu wa busara, na hapa kwa namna mbili
1. Kama ulivyosema hapo juu. Kwamba, vyama hivi havijavunja sheria au kuwa tishio
Kama ni hivyo, kuna nafasi ya mawazo mbadala badala ya kuhodhi fikra.
2. Kukosekana kwa busara kunaweza kumkuza sungura akalingana na Tembo.
Kauli ya mkuu wa mkoa inazidi kuchagiza tatizo badala ya kutoa suluhu
a) Kapiga marufuku vyama mkoani kwake akisema '' Waende kufanyia mikutano Kilimanjaro''
b) Katoa idhini ya uwepo wa vyama vya Wairaqi, Washomvi , Wamasai ndani ya Manyara
Kwa kutazama hayo mawili, RC anapinga ukabila na anataka vyama vya Utanzania
Halafu anapinga ukabila na kuhubiri ukabila ukafanyike K'njaro badala ya ''Tanzania''
Halafu tena anataka vyama vya makabila ya washomvi, wamasai na Wairaq si vya Tanzania
Hii ina maana moja,Mkuu wa mkoa aliwalenga wananchi wa Kilimanjaro na si ukabila
Maana yake ni nini?
Anawaunganisha watu wa Kilmanjaro zaidi katika ukabila kwa kuwaonyesha kuwa hawatakiwi kuwa na vyama Manyara, huko ni kwa Wamasai na Wairaq
Kwahiyo anaupiga vita ukabila kwa jicho la Kilimanjaro na anahubiri ukabila kwa jicho hilo hilo
Nadhani akiwa kiongozi wa Serikali, kuna kila sababu ya Serikali kujitenga na kauli zake
Ile dhana ya kwamba kuna watu wa kanda fulani wanapigwa vita, inapata mashiko hapa
Tutajadili vyama na sababu zingine, kubwa ni kauli ya RC dhidi ya watu wa Kilimanjaro.
Kwa maneno mengine, ni halali kwa wa Wamanyara na haramu kwa wa Kilimanjaro
Hii ni sumu, na huko Kilimanjaro wakianza kudai haki yao hao Wamanyara waende wapi?
Kuna tatizo kubwa sana ukimsikiliza, wala si vyama.
RC hakuongozwa na ukabila, alilenga mahali. Kama ni hivyo, alifanya hivyo kama yeye au alifanya hivyo kama sheria, au kama sera au ilani ?