Manyara: RC Munyeti apiga marufuku umoja wa watu wa Kilimanjaro mkoani kwake

Manyara: RC Munyeti apiga marufuku umoja wa watu wa Kilimanjaro mkoani kwake

Hayo ni matokeo ya viongozi kukosa kazi za msingi zakufanya. Mimi sidhani kama hivyo vikundi vya makabila mbali mbali vina jambo jipya au kubwa kiasi hicho kwasababu vipo kila mahali siku hizi hadi kwenye mitandao na havijaleta athari yoyote.Na katika hali ya kawaida kuna mambo katika jamii hauwezi kuyazungumza kwa usawa kwa watu wenye mienendo, mila na tamaduni tofauti mkaenda sawa kwaiyo kama watu wameona kuna ambayo wanaweza wakasikilizana wao kama wao kuna shida gani.Maana yote nikwaajili yakujenga.
 
Kwani wazungu wao hawana makabila? Mbona sijawai kusikia wana umoja wao mfano, umoja wa watu wanatoka Manchester city?
Unaweza kututajia makabila mawili yanayopatikana Uingereza?
Pili kwanini tuwaige hao mabeberu
 
Ulio wataja, makonda, mabeyo, mnyeti hawapo idara moja, nitofauti na dhamani kipindi cha mkwere ukienda TRA, kamishina, afisa elim ya mlipa kodi mchaga, afisa utawala mchaga,Afisa mipango chaga, mnatakiwa mkila na kipofu msimshike mkono tatizo lawachaga hawajui kula na kipofu
Tofauti ni nini?
 
Tuko na miaka zaidi ya 58 ya Uhuru sijaona madhala ya ivi vyama.
Lengo kuu ni kusaidiana tuu not otherwise.
Kuvipiga marufuku ni WIVU tuu
 
Alafu utasikia ngoma za makabila..urithi wetu.Huu si kuendekeza ukabila?
Utasikia mashindano ya ngoma za makabila..Hivi apo si kuendekeza ukabila?
Mnyeti timu yako na uwanja wako pale Misungwi umeupa jina la kisukuma..hivi huu sio ukabila?
Basi futa ilo jina au timu yako na uwanja wako tuelewe kua nivya wasukuma tu.
 
Hapo Mkuu wa Mkoa wa Manyara, yuko sahihi. Hawa watu wa mkoa huo tajwa wana ubinafsi sana.
Huwezi kuwa tajiri kwa kumchukia tajiri,hao wengine nani amewanyima kuwa na umoja wao?nafikiri makabila mengine yanapaswa kuiga spirit ya wachaga.
 
Kuzikana! Kuzikana kikabila! Ni mtindo wa kuungana kufanya upuuzi tu! Munafikia hatua ya kuamua nani awe m/kiti wa mtaa, nani awe mchungaji wa KKT Manyara, nk.

Nasikia na kuongozana gari la mchaga yupi mpande kuelekea mikoa mingine, hotel ya mchaga gani iko mkoa mwingine. There is a lot of primitive foolishness.
 
Ni mpango wa Mungu mwenyewe kutoa majibu kwa farao wa kichaga na wazaliwa wao kwa kutesa na kuonea Wana Israel wa makabila mengine kwa miaka mingi
We jamaa ndo mchawi humu alafu unajidai kushindilia kabisa na maneno ya kibiblia😂😂
Dunya kweli wew, hata Mungu anasikitika juu ya uwezo wako wa kufikiri. Pole sana ndugu
 
Huwezi kuwa tajiri kwa kumchukia tajiri,hao wengine nani amewanyima kuwa na umoja wao?nafikiri makabila mengine yanapaswa kuiga spirit ya wachaga.
Hawawaon wahindi, waarabu, wanakomaa na wachaga. Uchawi ndio shida yetu kubwa ( kum-pull down alie juu baadala ya kuiga mbinu alizotumia kufika hapo alipo), so sad uchawi unapewa baraka, term hii kweli ya kishamba💩
 
Binafsi RC yupo sahihi, kama ni kushirikiana waaanzishe vyama vya kijamii vitakavyojumuisha makabila yote yaliyopo mazingira hayo, bila kujali dini,rangi,vipato n.k n.k

Tutaondoa dhana ya ukabila
Dhana ya ukabila haijawahi kuwepo Tanzania, ndo inaanzishwa taratibu.
Watch n learn
 
nipo w

hapa mtaani kwetu nyumba zote ni za wachaga kuanzia nyumba ya kwanza mpaka ya mwisho,hakuna hata moja ya kabila lingine! mtaa umetulia hakuna uswahili kwa ufupi ni uzunguni ! my late grandfather alikua anaamini wasio wachaga ni savages alikua anawaita watu wa porini, kwa akili kama zako alikua sahihi kabisa kuwaita hivo
Ndiyo ukabila unaopigwa vita nawa Tanzania huo
 
Jinsi vilivyokuwa vikiendeshwa, mwanachama A ni Jaji/Hakimu, Mwanachama B ni Polisi, Mwanachama C ni Mwendesha Mashtaka, Mwanachama D ni Kiongozi Sehemu Fulani, Mwanachama E yupo TRA,, F NI Mfanyabiashara, G ni Jambazi, H ni na kadhalika.
Sasa hapo Jambazi anapata watu wote wa kuweza kumsaidia jambo lake, na Mfanyabiashara naye anapata watu wote wa kuweza kumsaidis na kumletea wateja, na watarajiwa wanapata watu wote wa kuweza kuwasaidia na kuwaumiza wengine
 
RC yupo sahihi ni kuleta ukabila tu na ubaguzi , futa kabisa huo upuuzi
Wa Iraq na wamasai sio ubaguzi?,Mnamaanisha kila kabila wakae na kuishi kwao?,basi Ngosha nae Arudi kwao......,Kweli ukianza na SHETANI HUWEZI KUMALIZA NA MUNGU....,Mmefikia hatua ya kuogopa vyama vya kufa na kuzikana?
 
Qur'an 49:13
49_13.gif

13. Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.
13
 
Back
Top Bottom