Manyara: RC Munyeti apiga marufuku umoja wa watu wa Kilimanjaro mkoani kwake

Manyara: RC Munyeti apiga marufuku umoja wa watu wa Kilimanjaro mkoani kwake

Miaka ya 90 nilihudhuria msiba wa Nshomile, ilipofika usiku bia zikaletwa, aise mbona mimi walikuwa wananiruka!!
 
Pole sana kwa masumbufu hayo mabaya sana. Je, atatufutia na kile hama cha kufa na kuzikana cha Wasambaa?? Ajaribu aone.
 
Wachaga walikuwa wanajiona supper power kipindi makabila mengine hayajapata exposure.

Sasa hivi kila Kabila lime chamgamka fursa za biashara, ajira za kisomi nk kila Kabila linafanya. Sasa hawa wachaga wanapata tabu kweli wanaona wanaonewa.
 
Huku Dom,wapo wachaga wana vikundi vyao, had kununua bidhaaa kwenye maduka wanaangaliana Wao kwa Wao
 
Hivi wewe ni nani? haswa mpaka umtake Rais amtengue Mnyeti? Kama unapenda ukabila nenda Burundi au Rwanda au Kenya lkn Tanzania hatuna ujinga huo na wala hatutaki kuuruhusu
 
Naunga mkono uamuzi wa RC Nyeti

safi sana ukabila sio wa kuachwa utamalaki
 
Utafuta chama cha kusaidiana sawa. Lakini ikitokea mtu mathalan wa Kilimanjaro amefariki. Ufanikishaji usafiri na mazishi utafanikishwa vipi? Ukweli ni kuwa hata kama watu wote wa eneo aliloishi marehemu watahusishwa, lakini wa atokako marehemu watahusika zaidi. Wenye mamlaka waangalie kama katiba za vyama vya kusaidiana zinagongana na katiba ya nchi. Namna nyingine ni wivu tu kwa wabunifu na wenye mafanikio.
 
Kweli wazungu wataendelea kutawala Dunia...yaani watu kujitamburisha kwa kabila lao na kua na Umoja wao imekua kosa..Watu wako kwenye Taifa lao huru alafu leo Uhuru wa kutumia lugha zao au kuunda Umoja wao imekua jinai...Kwa mtazamo wangu..watu wanao toka kabila flani kuunda Umoja wao ili kusaidiana,kubadirishana mawazo nk sio jinai kabisa. Tatizo hii elimu ya wakoloni ilitufumba macho na kuchukia utamaduni na uafrika wetu nayo ni shida.
Mwisho mwenyeti bila shaka amekosa busara na hekima kabisa au ata kumshauri hamna..mfano huku kwao Misungwi kwa wasukuma kuna kitu kinaitwa Wananzengo..vikundi hivi vinajumuhisha wasukuma wa maeneo ayo..je navyo vitafutwa?
Katika ili Mnyeti amekosa busara kabisa..
 
Wakati flani wanafunzi wa MUHAS waliosoma ILBORU tulitaka kuanzisha umoja wetu, uliokuwa na lengo la kusaidiana kimasomo na pale mwenzetu anapopatwa na matatizo. Aliyekuwa makamu mkuu wa chuo wa wakati ule alikataa kata kata kuwa na vikundi vya mlengo wa kimaeneo au kikabila. Hata hivyo, mpaka nahitimu masomo, wengi wa marafiki zangu wa ndani sikuwa nimetoka nao Ilboru.
So binafsi sioni umuhimu wa vikundi hivyo.
 
Naunga mkono uamuzi wa RC Nyeti

safi sana ukabila sio wa kuachwa utamalaki
Kwahiyo watanzania ni kabila moja ? Elimu ya wakoloni bado inasumbua sana..
Unaposema ukabila tofautisha na Umoja wa Kilimanjaro au Wachagga...
Lakini kwaku ni mwanetu kada basi awezi kukosea
 
Hujaishi bado wewe! Mjaluo kamwe hamsaidii asiye mjaluo!! Mkurya ni ngumu sana kumsaidia asiye mkurya, mchaga,mpare,mmeru,muarusha,mmaasai,msambaa na mmbulu wanaishi kwa umoja kama jamii moja toka enzi na enzi,babati ni eneo linalokaliwa kwa kiasi kikubwa na wambulu,wamaasai,wachaga,waman'gati,kwa kiasi kikubwa,na hapajawahi kuwa na malalamiko ya ukabila au ubaguzi, leo tuko hapa tunajadili uchagga na ukabila usiokuwepo kwa kulazimishwa na wapenda madaraka,hatari hii
Vikundi vya namna hiyo vinawafaa waishio nchi za kigeni, ili kusaidiana pindi wawapo huko. Ila ukiwa nyumbani nchini kwako wote ni watanzania, na sijawahi ona watanzania wanashindwa kumsaidia mtu eti kutokana na kabila. By the way hivi vikundi Mimi huwa sivipendi kwani vinachochea ubaguzi
 
Angefatilia zaidi asili na lengo la hivyo vyama, kwa haraka haraka wachaga wametapakaa sana Tanzania, na katika taratibu za mazishi ni lazima wazikwe makwao hapo kuna gharama ambazo wanachama wanachangia kwenye hivyo vyama kupunguza makali kwa wafiwa.

Kuwezesha kusafirisha miili ya marehemu, sidhani kama vyama vya wachaga vina ajenda nyingine tofauti na kuzikana.
Huku dodoma kuna kimoja kinaitwa UWAKA hichi kililenga kanda ya kaskazini kote ila yeyote anaweza kujiunga, na shuhughuli kubwa ni kuzikana.
Hapendi wachaga kwa kuwa wanaipenda Chadema......hahhaaaa bado hamjamjua tu.
 
Mwaka 2007, Prof. Rwekaza Simpho Mukandala, alifuta vyama kama hivi UDSM. Miongoni mwa vyama hivyo ni KAGERA UNIVERSITY STUDENTS ASSOCIATION (KAUSA) kilikuwa kikubwa mno nami nilikuwa kiongozi.
Mkuu Buberwa, hizo Premises zako na Conclusion mbona zinaleta invalid argument?
Kwamba Prof alifuta chama cha KAUSA kwa vile kilikuwa kikubwa mno?
 
Back
Top Bottom