Manyara: RC Munyeti apiga marufuku umoja wa watu wa Kilimanjaro mkoani kwake

Manyara: RC Munyeti apiga marufuku umoja wa watu wa Kilimanjaro mkoani kwake

Kauli ya RC Mnyeti ni kauli ya kibaguzi tena ubaguzi wa kikabila. Mimi nasema asipoguswa mpaka Jumatatu basi yupo mlezi wa ubaguzi huu na tusimfiche tumwambie ukweli wewe ni mbaguzi na sisi ni Watanzania.
Kasemaje RC Mnyeti?
 
Nafasi za ma DC na ma RC mheshimiwa rais amezigawa kama peremende kwa makada wa CCM kwa manufaa ya CCM bila kujali maslahi ya nchi, kila aliyelalamika alionekana 'mpinzani'. Sasa ndio muelewe magufuli ni kiongozi wa aina gani.
 
Kwani kasemaje wakuu?sisi wengine ndiyo tumeweka beleshi la zege chini mda huu,hatujui tanzania ilikopitia leo.
 
Safi Sana mnyeti,vikundi vya kusaidiana au vikundi vya kikabila? Huu upuuzi ndio unaochochea ukabila
 
Wachaga Mungu kesha wapa majibu Mitandao yenu mliyojenga miaka ya kuonea makabila mengine kwenye ajira,tenda,vyeo na fursa Mungu kamtumia Magufuli kuwapa majibu yenu.Uovu wenu umepatiwa majawabu
Nikweli kwenye vipindi vya Jk, na Mkapa walipiga hela sana Wizara ya fedha, na TRA, na Bandarini, walijenga kikundi chao nafasi nyeti walijazana wao tu, sasa magufur anafatilia ofis zote kujua kinafanyika nini, tofauti kikwete na mkapa wao walikuwa kazi yao nikusafiri tu marekani awajui mawizarani kunafanyika maovu gani.
 
kasemaji kwani, nipo jirani na mkulu Nimwambie afanye yake.
ka thread kafupi halafu hakaeleweki
sema huyo mnyeti alichokifanya siyo unaongea bila sababu za msinng tutajua unachuki nae binafsi
Kasemaje RC Mnyeti?
Kwani kasemaje wakuu?sisi wengine ndiyo tumeweka beleshi la zege chini mda huu,hatujui tanzania ilikopitia leo.
 
Nafasi za ma DC na ma RC mheshimiwa rais amezigawa kama peremende kwa makada wa CCM kwa manufaa ya CCM bila kujali maslahi ya nchi, kila aliyelalamika alionekana 'mpinzani'. Sasa ndio muelewe magufuli ni kiongozi wa aina gani.
Magufuli ni kiongozi mzuri sana tena na ataacha alama iliyotukuka katika historia ya taifa kwa kujenga nidhamu kwa watumishi wa umma, kujenga miundombini ya kiuchumi, kuwezesha biashara na uwekezaji na kuinua hali ya utaifa na uzalendo.

Rais anapofanya uteuzi hateui roboti la kupewa maelekezo na kutendo ,anateua watu ambao Wana utashi binafsi wa kutenda na utashi huo wengine hupelekea kutenda na kutamka yasiyofaa, hayo yasijumuishwe na uongozi wa Rais Magufuli
 
Ila tukiacha unafiki tukawa wakweli, hata Wachaga huwa niwabaguzi sana tena ule ubaguzi wa kimya kimya ambao kwenye macho ya wengi huwezi kuuona... Mchaga kwenye michongo ya hela hupeana wenyewe na mbaya zaidi ni wepesi sana kuwekana kwenye nafasi hili liko wazi tuache unafiki..

Ukweli uliowazi, Tanzania ukabila upo tena wa siri siri sana na hili linaongozwa sana na makabila makubwa ya Tanzania na ukilichunguza kwenye kila taasisi ambayo haya makabila yapo utaliona...kuna mengine ni mazito hapa kuyasema ila awamu fulani ya tatu kuna taasisi fulani nyeti kiusalama kuna kabila waliwekana sana na hata nafikili failure pale ndipo ilipoanzia..Awamu ya tatu pia mashemeji walijenga himaya kwenye taasisi zote za hela mpaka ikawa too much..

Makabila madogo madogo Tanzania hasa watu kutoka Pwani ndio pekee sijaona kama wana huu upumbavu..
 
Madhani bado kidogo tu itatilewa amri ya kuwacharanga mapanga wachagga popote watatakapoonekana nje ya kilimanjaro!! Wachagga mnapaswa kuwa na umoja wakati huu kuliko wakati mwingine wowote,na Mungu awape ulinzi wa pekee kipindi hiki,na mufanye ibada maalum kwa ajili ya maisha yenu maana dalili na ishara zinatia mashaka mno,Mungu awalinde sana.
Looooooooh, Mungu wangu mbona hali inatisha...kwa hiyo hata kuzika Watu wa Kilimanjaro hawaruhusiwi tena Kuzika Manyara, au siyo?
 
Kauli ya RC Mnyeti ni kauli ya kibaguzi tena ubaguzi wa kikabila. Mimi nasema asipoguswa mpaka Jumatatu basi yupo mlezi wa ubaguzi huu na tusimfiche tumwambie ukweli wewe ni mbaguzi na sisi ni Watanzania.
Baadhi ya Wachagga wanazingua. Baadhi sio wote. Najua Kuna Wachagga hawataki hivyo vikundi vya kichagga. Kukatazwa ni kawaida. Hata chuo kikuu UDSM zamani vilikuwepo lakini vimekatazwa. Kwani Wachagga wamepata madhara gani UDSM. Undeni social unions sio tribal unions.
 
Wachagga mnaunda vikundi vya kikabila halafu mnaviita vya mkoa wa Kilimanjaro. Mbona hamuwataki Wameru, Wamasai na Wapare kujiunga na hayo makabila yapo pia Kilimanjaro?
 
Wame experience huko Manyara mpaka wenyeji wamekalamika kuwa vikundi hivyo vinaleta ubaguzi kwa wenyeji
sasa mbona karuhusu vikundi vya makabila ya mkoa wake ? halafu unapaswa kujua kwamba lengo ni wachaga
 
Anapita wala usisumbuke kujiuliza sana. Wenyeji wa Manyara wamelalamika umoja huo una malengo mabaya ndiyo maana ukapigwa marufuku mbona mikoa mingine hakuna shida. Wanakilimanjaro waache ubaguzi
Usitunge uongo , video iko pale juu , haya yako hayamo
 
Kama ni kufuta, vifutwe vyote vya nchi nzima! Kuanzia cha wana Chato n.k

La sivyo iyakuwa ni upandaji wa mbegu ya ubaguzi wa kikabila waziwazi!! Na mavuno yake kuna siku yataonekana....

Hawa viongozi wasio na akili wametufikisha mahali pabaya sana!
Huenda Mkoa wa Manyara vilikuwapo vyama viwili tu cha Kilimanjaro na Mara basi. Vingekuwepo vya mikoa mingine navyo vingefutwa!
 
Back
Top Bottom