Manyara: RC Munyeti apiga marufuku umoja wa watu wa Kilimanjaro mkoani kwake

Manyara: RC Munyeti apiga marufuku umoja wa watu wa Kilimanjaro mkoani kwake

Acha uongo amepiga marufuku hata umoja wa wanamara
ilikuwa ni kutafuta njia ya kuanzia tu , tangu lini wakurya wakawa na umoja wa namna hiyo ? chunguza mitaa unayoishi uone kama kuna umoja wa wakurya
 
samurai, Michongo watu wote wanapeana wenyewe kwa wenyewe
Ushawahi ona msomali anampa mswahili mchongo
Mbona wa haya, wajaluo husemi

Ova
 
Wachagga mnaunda vikundi vya kikabila halafu mnaviita vya mkoa wa Kilimanjaro. Mbona hamuwataki Wameru, Wamasai na Wapare kujiunga na hayo makabila yapo pia Kilimanjaro?
Kwani wamasai Hawana vikundi vyao?

Ova
 
Watapigwa na mabomu ya machozi na polisi
 
Mkuu wa mkoa hajakosea

Hivi vikundi vilikuwa vinachochea sana ukabila

Bora vifutiliwe mbali

Lazima watu wawe na vikundi vyao vya kusaidia misiba na shida mbalimbali maana wanatoka sehemu moja!

Kuvizuia ni upunguani wa aina fulani!

Tuseme wakitaka kuchinja na kutambika kikwao watafanyeje na umevunja umoja wao???

Wana shida za kikwao za matambiko yao huko,unavunja mikutano yao,watajisaidia aje?

Au Mnyeti ndio aje awasaidie kutambika mizimu ya kabila asilolijua kwa lolote?

Punguani huyu na wewe included!
 
Kauli ya RC Mnyeti ni kauli ya kibaguzi tena ubaguzi wa kikabila. Mimi nasema asipoguswa mpaka Jumatatu basi yupo mlezi wa ubaguzi huu na tusimfiche tumwambie ukweli wewe ni mbaguzi na sisi ni Watanzania.

Aguswe na nani wakati awamu hii ni ya kuwashughulikia wachaga? Mnanyooshwa, si uliona mwingine aliondoka mbele ya Jaffo na watu wakaendelea na shughuli zao?
 
Kwani wamasai Hawana vikundi vyao?

Ova
Huo ukabila ndio hatuutaki. Vikundi vyote vya kikabila vivunjwe. Changianeni kanisani, mtaani, kijijjni, misikitini au mrudi kwenu mkachangiane lakini kurasimisha na kuanza kutengeneza ubaguzi.
 
Hata mimi sivipendi vikundi hivyo,vifutwe tu,kama kukitokea tatizo wote tusaidiana kama jamii.Ila anaji-contradict kwa kuruhusu uanzishwaji wa vikudi vya makabila ya mkoa wa Manyara,mbona navyo ni vya kikabila?Asiruhusu vyote.Mimi huwa sipendi pia vikundi vya kufa na kuzikana,napenda tatizo likitokea tusaidiene wote kama jamii.
 
Wachagga wanataka kutuletea nchi Kama Wakikuyu wanavyofanya Kenya. Mtu anapata nafasi, badala ya kulinda maslahi ya Taifa, analinda maslahi ya Wachagga. Mliona mmefika mbali na makabila mengine hayafai, hayajasoma, hayajui kutafuta hela etc. Rudini Tanzania. Achaneni na Chagga Empire.
 
Hizo zote ndiyo Sera za utawala wa awamu ya tano, ambao umeamua kufanya ubaguzi ndani ya nchi hii, iliyokuwa haina ubaguzi wa kabila, dini wala itikadi za kisiasa

Hakika Taifa hili linazidi kuporomoka kutoka kileleni mwa mafanikio yake na kurejea kwenye ukabila, udini na kufanya upendeleo wa wazi kabisa wa itikadi za kisiasa
Mnyeti anakataza ukabila. Hajaporomosha taifa anakataza watu wa Mara na Kilimanjaro wanapokuwa mkoani Manyara wasiendekezi ukabila - anataka waungane na watanzania wenzao.
 
Michongo watu wote wanapeana wenyewe kwa wenyewe
Ushawahi ona msomali anampa mswahili mchongo
Mbona wa haya, wajaluo husemi

Ova

Ndio maana nikakwambia Tanzania kuna ukabila wa chini kwa chini Wachaga ni moja ya watu wenye hizo tabia, hao uliowataja pia wahaya na wajaluo ni walewale tu...

Baadala Watanzania tulitakiwa tuuishi utanzania kwa vitendo si nadharia... Ndio maana ukazungumzia msomali naongezea Mhindi, Muarabu na wapersia wanaushi ule undugu wao pasipo kuangalia ukabila..
 
Wachagga wanataka kutuletea nchi Kama Wakikuyu wanavyofanya Kenya. Mtu anapata nafasi, badala ya kulinda maslahi ya Taifa, analinda maslahi ya Wachagga. Mliona mmefika mbali na makabila mengine hayafai, hayajasoma, hayajui kutafuta hela etc. Rudini Tanzania. Achaneni na Chagga Empire.

Hili ni tatizo la makabila mengi makubwa hapa Tanzania...
 
Wanabodi, Miaka ya mwanzo wa utawala wa Prof Rwekaza Mkandala pale udsm bila kudhibiti vyama vya makabila angepata taabu Sana, Vyama vikubwa vya kikabila ilikuwa Wahaya na Wanyakyusa na sio kwa bahati mbaya bali ufaulu wao ndio uliwafikisha hapo Udsm na kufanya wao watawale kwa idadi

Wahaya na Wanyakyusa udsm walikuwa wanaitisha mikutano ya kikabila wakati wa weekend kujadili mustakabali wa maisha na kabila Lao, Wakimaliza ukabila mijadala iliyofuatwa ni kuhusu maisha ya shule

Umoja wa Wahaya na Wanyakyusa ulianza kujadili siasa chuoni hata mwenzao akishindwa kuendelea kwa kufeli walipambana arudi mpaka tone la mwisho la damu, Walihamasishana kuunga mkono migomo chuoni

Bila kudhibitiwa wakati huo kukiwa hakuna WhatsApp, Instagram. Leo yangeongeleka mengine hapo udsm

Pongezi kwa Prof Mukandara kuweka msingi na kufuta ujinga wa hayo makabila


Wana JF, kuna makabila hapa Tanzania kwa mawazo yao au fikra zao wanaona lugha zao kila mtu anazifahamu au anajua kuongea, Wanajiona wao ni makabila makubwa kuliko mengine

Nitataja baadhi ya makabila yanayokera na kusumbua watu iwe sokoni, mitaani au barabarani, Haya makabila wao kazi yao ni kuongea tu lugha zao na kutusalimia kwa lugha zao za kikabila bila kuuliza kama mhusika wa kabila hilo

Mosi, Wanyakyusa. Hili kabila na lugha yao ndio kero zaidi, Wao hata maneno ya kiswahili wameyageuza kwa kinyakyusa na kutaka kulazimisha watu wayatamke hivyo, Utasalimiwa kwa kinyakyusa hata kama hupendi

Pili, Wahaya. Hao Nadhani wengi wanawafahamu kwa kelele zao za nshomile, Sasa kama nshomile au umesoma sisi yanatuhusu nini, Ukiwa na marafiki wa kihaya wakikutana wawili basi wewe utaachwa mataa wao ni kuongea kihaya tu, Hawafikiri kuna mtu asiyeelewa

Tatu, Wachaga, Hawa ndio vituko sasa hapa bongo, Lugha zao wanaita kichaga lakini hawaelewani wao kwa wao, Wanalazimisha kuongea lugha inayoitwa kichaga mbele za watu, Lakini kila wilaya ina lugha ya kichaga kinachotofautiana

Alichofanya Mnyeti ni cha kuigwa na kupigiwa mfano, Ukiacha mambo haya yakue mbeleni giza
 
Wachaga Mungu kesha wapa majibu Mitandao yenu mliyojenga miaka ya kuonea makabila mengine kwenye ajira,tenda,vyeo na fursa Mungu kamtumia Magufuli kuwapa majibu yenu.Uovu wenu umepatiwa majawabu
Wazungu pia walidhani wanawakomoa Wayahudi kwa tabia kama za awamu ya tano ya Magufuli. Ila yako wapi? Wayahudi wanadunda tu.
 
Halafu watu walioenda shule ndio Wana ukabila na ubaguzi uliopitiliza. Watu wa vijijini wanaishi kwa ushirikiano mkubwa bila kujali makabila yao. Nafurahigi Sana nikiona bibi na mama yangu wanavyoishi na kushirkiana na wamama na wababa wa makabila mengine bila kujali itikadi ya siasa, ukabila, ujiografia etc.
 
Tunajifanya tumesoma halafu tunaishia kuharibu orientation ya nchi.
 
Back
Top Bottom