Manyara: RC Munyeti apiga marufuku umoja wa watu wa Kilimanjaro mkoani kwake

Manyara: RC Munyeti apiga marufuku umoja wa watu wa Kilimanjaro mkoani kwake

Hakuna maendeleo hapo. Unajenga kigorofa migombani halafu kwa mwaka unalala humo siku mbili tu kama siyo ujinga ni nini huo ? Kwa nini usiwekeze mahala ambapo utaingiza pesa ?

Ujinga wako ufiche usijehuku utachekwa, maendeleo huanzia nyumbani, na gorofa alilojenga linatokana na faida ya biashara zake,ujinga wako unakutuma ukipata faida upeleke wapi?usile,usinywe,usivae,usilale pazuri.
Ndo maana kwenu kuna nyumba za vichuguu maana ubongo wenu umejaa usaha
 
Si ajabu kitachofuata ni kufuta makanisa ya wazungu maana yanafunza utamaduni wa kimagharibi, futa misikiti maana inafunza utamaduni wa mashariki ya kati, futa kila ambacho hakina asili ya Manyara...
Umewaza mbali
 
Nguruvi3,
Nilitegemea Rc angepiga marufuku kuanzishwa kwa hivyo vyama, sio kwa wana Kilimanjaro tu, hadi kwa wazawa wa mkoa wa manyara,ningemuona kweli ana Nia ya dhati ya kupambana na hii saratani inayoshika kasi kwa kukisiri kwa vikundi vya kikabila nchini.Tuishi na jamii zinazotuzunguka vizuri, utasaidiwa na mgogo hali ya kuwa wewe ni mndengereko.
 
Vyama vya kikabila siyo vizuri kwa mustakabali was taifa.
Hata hivyo,katazo la mkuu wa mkoa lina utata kidogo;
1. Pale viwepo vyama vya Wairaq, wamasai,......(makabila).
2. Watu wa Kilimanjaro (mkoa, siyo kabila), wakafanyie kwao.

Tunahitaji busara na hekima kupinga mambo tunayohisi yanaweza kusababisha mgawanyiko katika taifa.
Hatuwezi kupinga ukabila kwa ubaguzi.
 
Huyu jamaa nilimdharau wakati alipokamtwa akiwatongoza madiwani wa chadema.
 
Ukiona mtu anaota ndoto za mchana huna haja ya kushangaa ila ujue karibu anakuwa chizi.
Rubbish ideology, wachaga walikuwepo kabla ya crdb, na wapo hata crdb ispokuwepo,
Wachaga hawategemei mikopo kuendesha shughuli zao, ukitaka kujua uhalisia pitia minada yote ya mabenk kwa wakopaji utajua wakopaji wengi defaulters kina nani.wachaga hawakuja mjini kucheza ndombolo bali kutafuta pesa na wengine elimu, hyo miaka mingine mitano hamtawafanya chochote zaidi ya kuwanyima fursa za ajira, sasa miaka hyo mitano ikiisha itakuweje au mnadhani mtatawala milele
 
Kila mtu ataishi kivyake... ukiona vikundi vya kufa kufaana viko hatua hiyo ujue vyama vya siasa tofauti na kile pendwa vitakuwa mashakani kiasi gani!?
Jina baya humdhuru mwenye nalo... tunachojisahaulisha ni kwamba kila mwanadamu ana kichaa chake na uwezo wake wa kukidhibiti... ole wetu... ole wetu... ole wetu.
Wengine tunasema kwa hali ilivyo "yetu macho"
 
Si ajabu kitachofuata ni kufuta makanisa ya wazungu maana yanafunza utamaduni wa kimagharibi, futa misikiti maana inafunza utamaduni wa mashariki ya kati, futa kila ambacho hakina asili ya Manyara...
Ubepari tuliukataa... ukomunisti hatukuuweza... ujamaa ulitushinda ninachokiona sasa ni kama GARI LIMESHAKATA USUKANI NA MWELEKEO UMEPOTEA!!!
NI MWENYEZI MUNGU PEKEE ATUNUSURU TUENDAKO MAANA....
 
Vyama vya kikabila siyo vizuri kwa mustakabali was taifa.
Hata hivyo,katazo la mkuu wa mkoa lina utata kidogo;
1. Pale viwepo vyama vya Wairaq, wamasai,......(makabila).
2. Watu wa Kilimanjaro (mkoa, siyo kabila), wakafanyie kwao.

Tunahitaji busara na hekima kupinga mambo tunayohisi yanaweza kusababisha mgawanyiko katika taifa.
Hatuwezi kupinga ukabila kwa ubaguzi.
Akihojiwa huyo RC huenda akajibu huku katanua makwapa "...ni amri kutoka juu!!!?"
 
chezea Wachaga ila mtapata majibu. Tumefika patamu Wachaga waandamane kupinga ubaguz wa wazi wazi dhidi ya uwepo wetu maana tunapoelekea watatutoa roho kama Hitlar kwa Israel

Mbona msiba wa ajali ya Mafuta morogoro ulifanywa ni wa ccm kana kwamba ni wa ccm tuu ndiyo waliokufa? Makundi mengine hata kuchangia damu ilikuwa noooooooooooo.
 
chezea Wachaga ila mtapata majibu. Tumefika patamu Wachaga waandamane kupinga ubaguz wa wazi wazi dhidi ya uwepo wetu maana tunapoelekea watatutoa roho kama Hitlar kwa Israel
Mkuu Tumainel nasoma comment zako humu nabaki tu kumshangaa Mungu kama ni wewe kweli.Kweli Yesu alikuja duniani kwa ajili ya kwenye dhambi ili tupate kuokoka. Amina.
 
Nyakati nyingine yatupasa kufikiri sawasawa ili kupungunza sintofahamu zisizo na ulazima wowote ule.

Kwa mfano mchungaji Msigwa yuko kwenye umoja wa watu wa Iringa lakini yeye ni mwenyeji wa makete mkoani Njombe.

Hizi UMOJA mbali mbali ziko kwa maslahi ya kijamii na kiuchumi zaidi na si maslahi ya kisiasa. Ukitaka siasa nenda kwenye Vicoba huko utawakuta wamejiunga kiitikadi kwa mfano UMAMA ambao ni Umoja wa Madereva Makambako hawa wanafadhiliwa na mbunge wao kwahiyo japo ni Wanaume watupu lakini wapo kisiasa zaidi.

Maendeleo hayana vyama!
 
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa uhuru WA watu kuanzisha ama kujiunga Na vyama ili kufikua madhumuni yalio nayo Vyama vya Watanzania wanaotka eneo moja la nchi wanaoishi nje ya eneo lao la kuzaliwa huwrza kusajiliwa chini ya Sheria ya Societies Act (zamani Societies Ordinances) 2002.
Sasa Kama RC anaona kwamba uwepo wa vyama hivyo unaathiri maendeleo ya Taifa kwa namna yoyote angepeleka pendekezo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ili sheria ifute vyama hivyo au kuwekewa masharti mapua.
Kitendo cha RC kufanya unilateral decision bila hata kuwaita Na kuwajoji wahusika inakiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo yeye aliapa kuilinda Na kuitetea. Kwetu sisi wengine hatua ya RC Manyara inaanzusha a bad precedence ambayo itaathiri maendeleo ya ya baadhi ambazo zimekuwa zikitegemea mchango wa wazaliwa wa eneo lao wanaoishi Na kufanya kazi nje ya eneo hilo Kumbe hata wimbo tunaoendeleza kuwa diaspora wachangia maendeleo ya Taifa inatofauti gani na umoja huo wa Watanzania wa kabila au eneo fulani kuunganosha nguvu ili kujenga kwao?
Tuepuke kuwa chanzo cha vita visibyo na tija.
 
Mtoto wa kwanza katika ufaulu darasa la 7 kitaifa siku hizi lazima atoke chato
 
Back
Top Bottom