Manyara: RC Munyeti apiga marufuku umoja wa watu wa Kilimanjaro mkoani kwake

Manyara: RC Munyeti apiga marufuku umoja wa watu wa Kilimanjaro mkoani kwake

johnthebaptist,
Tangu lini mukawakubali wapare kwamba ni wenzenu? Tangu lini mukashabikia biashara ya Mpare kwamba ni mwenzenu? Ubaguzi unawauwa! Hata Arusha inawaponyoka CHADEMA kwa hilo hilo! Arusha kuna mbunge Mchaga, je, Moshi wako tayari kumpa support mtu kutoka Arusha awe Mbunge wao, au hata Mpare tu!

Hakuna umoja wa maana! Kwani kusaidiana lazima awe mchaga tu ndo musaidiane? Yote makundi ya kufanya mambo ya hovyo tu bila kumbukumbu kwamba munaonekana. Ubaguzi hadi hotel, magari ya abiria, shule, vyama vya siasa n.k. kila sehemu eti ni kumuunga mkono mchaga mwenzenu. you are finished.
 
Sijajua kilimanjaro ipi unayoiongelea.. kuiita kilimanjaro makaburin ilihali makabur yenyewe ni machache na yako sehem maalum ni upumbavu.
Tuweke ushabiki pembeni..si wachaga tu haya makabila mengine wanatoka makwao wanakwenda sehem nyingine kutafuta pesa. It doesnt mean kuwa makwao hapajaendelea hapana lakin ili kuendana na gali ya maisha lazima watu watoke wakatafute.
Si wahaya.. wasukuma..wakurya..si wanyakyusa na makabila mengine.. wote wapo kwenye mikoa ya watu wanatafuta.
Na pia kama makaburi kila mkoa kijiji wilaya wanamakaburi.
You see its not about status.. its about life kwa ujumla.
Uchagani pangekuwa pameendelea mngebaki huko huko migombani kwenye umande mwingi na udongo wa mfinyanzi wa kuteleza mkaishi kama nyani lakini mmekimbilia mikoa ya watu na kuuacha mkoa wenu kuwa mahali pa kwenda kuzikwa tu na si pa kuishi. Kwa ufupi Kilimanjaro ni makaburini tu kama ilivyo Kinondoni makaburini hakuna tofauti.
 
Haaa tutafanya mikutano kwa Whatsupp au teleconference.Tunanunua bando kwenye siku moja tunafanya mkutano. tutumie technologia sawasawa
 
Usijidanganye ndugu, Hilo kanisa la mkoloni ndio nini mkuu? Nimefika hadi huku migombani kote ni Ulimwengu wa Tatu tu,
Kwa ufupi, Tanzania yote makabila yote ni Average third world, plus or Minus,
Hapo umeona kanisa tu? Hahaha eti Tanzania yote Ni Sawa? Kwahyo moshi vijin kulivyo jengeka utafananisha na tandahimba? Hebu acha vituko
Hapa ni marangu(moshi vijijin)

FB_IMG_15702098938113855.jpeg
 
Patriot,
Kwanza mimi siyo mchaga hata tindo analielewa hili.

Pili ninachosema katika mada yangu ni kwamba Umoja wa watu wa mkoa fulani siyo Umoja wa kabila......kwani hakuna kabila linalohitaji umoja kwa sababu Kabila tayari ni moja ila Makabila ndio yanaweza kuwa na umoja.

Wewe kuwa mpare hakukufanyi uwachukie wachagga kwa sababu baadae utagundua wewe ni mgweno na hiyo dhambi haitakuacha!
 
Uchagani pangekuwa pameendelea mngebaki huko huko migombani kwenye umande mwingi na udongo wa mfinyanzi wa kuteleza mkaishi kama nyani lakini mmekimbilia mikoa ya watu na kuuacha mkoa wenu kuwa mahali pa kwenda kuzikwa tu na si pa kuishi. Kwa ufupi Kilimanjaro ni makaburini tu kama ilivyo Kinondoni makaburini hakuna tofauti.
Acha utoto wewe hapa Tanzania kuna waingereza, wamarekani, wafaransa n.k kwahiyo kisa wamekuja Tanzania inamaana nchi zao ni mbaya kuliko Tanzania? watu wanahama kupata fursa mpya sio kisa kwao kuna njaa sana
 
Mnafanya umoja kimagroup sasa , au kimtaa, mpak inafikia hatua ya chama kinarun mkoa mzima na mnaitisha kikao cha mkoa , si hatar hyo...alaf manyara sio far from Kilimanjaro , ni useles kutengeneza chama cha namna hiyo tena Kwa ukubwa huo , angalau ingekuwa Songea au katavi huko hapo inaweza ikamake sense , japo bado ni very dangerous
Hivi hivyo vyama vinamajeshi yake na vinamamlaka na uwezo wa kibadili ukweli?.
 
We nawe acha upumbavu wako,umezidisha masifa mpaka unakera!! Sijui mchaga gani mpumbavu hivi? Sasa hilo shetani likiona masifa ya kijinga kama haya ya kwako si linaweza ku justify ubaguzi wao dhidi ya wachaga? Au anaweza kupeleka pendekezo kwa mkuu ateketeze wachagga wote maana wanamkwamisha? Na si unajua jinsi yule mtu asivyowapenda? Hebu kaeni kwa adabu jamani,mpo hatarini mjue
Huwezi kuzuia mafuriko kwa mkono mkuu,kwani ni haramu mtu kusifia? Lengo ni kuwaambia wasidhani maendeleo ya kule Ni ya Leo,kule maendeleo Ni jadi yao huwezi kuyazuia kivyovyote
 

Kipindi hichi watu akili hawana...united we stand ...divide we fall
 
Wachaga walikuwa wanajiona supper power kipindi makabila mengine hayajapata exposure.

Sasa hivi kila Kabila lime chamgamka fursa za biashara, ajira za kisomi nk kila Kabila linafanya. Sasa hawa wachaga wanapata tabu kweli wanaona wanaonewa.
Karibu uchagani mkuu uondoe stress aliyetangulia katangulia tu
Mazingira tu haya yanakujulisha kuwa jamii hii iliendelea, imeendelea na itazidi kuendelea
FB_IMG_15707285916351968.jpeg
 
Angefatilia zaidi asili na lengo la hivyo vyama, kwa haraka haraka wachaga wametapakaa sana Tanzania, na katika taratibu za mazishi ni lazima wazikwe makwao hapo kuna gharama ambazo wanachama wanachangia kwenye hivyo vyama kupunguza makali kwa wafiwa.

Kuwezesha kusafirisha miili ya marehemu, sidhani kama vyama vya wachaga vina ajenda nyingine tofauti na kuzikana.
Huku dodoma kuna kimoja kinaitwa UWAKA hichi kililenga kanda ya kaskazini kote ila yeyote anaweza kujiunga, na shuhughuli kubwa ni kuzikana.

Sidhani kama ita - work out...

Hii kitu iko kila mahali wala haiwahusu wachagga au watu wa Kilimanjaro tu....

Hata huku kwetu tunayo hii association ya watu wa eneo fulani. Siyo rasmi kuwa imeandikishwa mahali lakini inafanya kazi na iko miaka na miaka....

Tuna kikao mara moja kwa mwezi na huwa tunaalikana kwa mobile text message tu na watu wanaheshimu mno umoja huu....

Kwa hiyo, nionavyo mimi hiyo ni kauli tu lakini huwezi kufuta kilicho ndani ya mioyo ya watu....

Watakutana tu na wataendelea kufanya shughuli zao kama kawaida...
 
MKUU WA MKOA WA MANYARA ASIGAWE WATU KWA MISINGI YA UKABILA!

Tumeshangazwa sana na taarifa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Mnyeti amefuta kikundi vya watu wa Kilimanjaro waishio Manyara na kwamba ataendelea kuvifuta vikundi vyote vya watu toka mikoa mingine waishio Manyara kwa kisingizio kuwa vinaendekeza ukabila!

Vitendo hivi visipokemewa sasa vitaathiri sana ustawi, umoja, na ushirikiano katika nchi yetu na hivyo kuchochea chuki na ubaguzi kwa misingi ya kikabila au kikanda! Tunatarajia kuona mamlaka ya uteuzi pamoja na mamlaka nyingine zinazohusika na usimamizi wake zitamkemea Mheshimiwa Mnyeti kwa vitendo hivi! Endapo mamlaka hizo zitashindwa kumkemea basi Mungu mwenyewe atamkemea! Hivi kauli na matamko haya ya Mheshimiwa Mnyeti yataishia wapi? Je, akilikuta Kanisa la AICT huko limejaa Wasukuma atalifuta? Hivi akilikuta Kanisa la Mennonite huko limejaa Wajita atafanyaje? Akilikuta Kanisa la Kisabato limejaa watu wa Mara na Kilimanjaro atafanyaje? Atalifuta Kanisa la Moravian huko kwa kuwa limeanzishwa na watu kutoka mikoa ya Mbeya au Tabora au Songwe? Hivi kweli atakataza kujengwa kwa misikiti ya Sunni kule kwa sababu itakuwa na watu wengi wa Kigoma? Hivi akiwakuta Wakenya huko atafuta jumuiya zao? Kweli atawazuia Wazungu kukusanyika kupitia jumuiya zao? Hivi kweli atazuia na kuzifuta jumuiya za Kihindi katika Mkoa wake?

Inawezekana Mheshimiwa Mnyeti hajui kuwa katika kila nchi kuna jumuiya au vyama vya watu wanaotoka katika nchi zao ikiwemo Tanzania. Viongozi wetu wakuu wa Serikali mara kadhaa walipotembelea nchi hizo wameongea na jumuiya hizo. Vyama hivyo vimekuwa kichocheo cha uchumi na maendeleo katika nchi au maeneo wanayotoka.

Biblia inatueleza kuwa watawala wa Kiajemi waliwahi kutunga sera za kibaguzi kwa lengo la kutaka kuua vyama na mikusanyiko ya Wayahudi wakati wa Danieli! Lakini sera zile hazikufanikiwa. Lengo lao lilikuwa ni kuwanyamazisha viongozi wote wa Kiyahudi akiwemo Danieli lakini walishindwa na matokeo yake walinyamazishwa wao! Kadhalika, wakati wa Esta, mamlaka zilikuja na sera ya kufuta vyama, na vikundi vyote vya Kiyahudi pamoja na mikusanyiko yao. Lakini Hamani, aliyekuwa ndiye mtunga sera mkuu alifutika yeye mwenyewe kutoka katika uso wa dunia wakati Moderkai, kiongozi wa Wayahudi ambaye alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa wakilengwa na sera ile ya kibaguzi, akatangazwa kuwa Waziri Mkuu.

Ni hakika kuwa Mkuu wa Mkoa anayo mamlaka makubwa sana katika Mkoa wake. Lakini asipotumia vizuri na kwa hekima mamlaka hayo anaweza kujikuta anagombana na wananchi lakini pia asishangae kujikuta anapambana na Mungu! Je, ni kiongozi gani aliyewahi kupambana na Mungu akabaki salama? Mheshimiwa Mnyeti na wengine walio nyuma ya mkakati huo wasihangaike kutaka 'kummaliza na kumnyamazisha Mordekai' wanayemdhania haijalishi kama ni mtu au kikundi au jamii fulani.

Wajibu wa Askofu unamtaka asinyamaze na kufumbia macho mambo yote yanayoashiria hatari katika jamii. Atanyamazaje kwa mfano anaposikia kauli na matamko kama ya Mheshimiwa Mnyeti? Ole wake Askofu asiposimama katika zamu yake (Ezekieli 33:1-20).

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani.
 
Back
Top Bottom