Manyara: RC Munyeti apiga marufuku umoja wa watu wa Kilimanjaro mkoani kwake

Manyara: RC Munyeti apiga marufuku umoja wa watu wa Kilimanjaro mkoani kwake

Tatizo la mikoani ni ile hali ya watu kujuana kwa ukaribu.

Nilienda kufanya kazi Tanga mwaka 2004 na ndani ya wiki moja mji mzima ukawa umeshanijua.

Huwezi ukamsikia Makonda akiongea kama huyo Mnyeti,

Dar kuna mamia ya makundi ya kikabila ambayo yana mchango katika ukuzaji wa maendeleo ya maeneo ambayo watu wanatoka.
 
Watu wanafurahia Ukabila kwa maslahi yao binafsi ...hata Kama haupo watatengeneza Hali ya kufikirika
watachora Simba au kuchonga kinyago na Kisha kujitisha nacho...watu Kama Hawa huwa hawajui chungu halisia ya wanachokifanyia mchezo...Hadi kiwatokee...tupinge Ukabila
 
Utawala huu unawachukia sana wachaga, sijui kwa nini
Kuwachukia watu wenye akili ni kazi bure, hawa jamaa waliwekeza siku kwenye elimu, badala ya kuwauliza waligikaje hapo tunatamani wawe kama sisi
 
Uchagani pangekuwa pameendelea mngebaki huko huko migombani kwenye umande mwingi na udongo wa mfinyanzi wa kuteleza mkaishi kama nyani lakini mmekimbilia mikoa ya watu na kuuacha mkoa wenu kuwa mahali pa kwenda kuzikwa tu na si pa kuishi. Kwa ufupi Kilimanjaro ni makaburini tu kama ilivyo Kinondoni makaburini hakuna tofauti.

Hahahaaaa, wachaga wasingekuwa huko unakoishi usingepata hata hyo akili iliyojaa usaha unayoringia kuandika utumbo humu. Zunguka tz yote ukikosa mchaga ujue hata mahali pa kula hapafai, wanakusaidieni kuondokana na upumbavu uliowajaa, wamehama kwao kwenda kutafuta maisha na wameweza wanawasokomezea maporini wwao wanaishi mjini, vijijini kwao mijumba ya kutisha.
Kwa ushauri tu dec 20-24 nenda segera na KIA uone mafuriko ya magari yakielekea uchagani utapata jibu
 
Inaelekea serikali ina mkono wake katika hili suala! Kwa nini haikemei jambo hili la Mnyeti? Vyama/Umoja wa kiwilaya, kimkoa, kikanda na hata kieneo na kifamilia umekuwepo tangu muda mrefu enzi za Nyerere. Hata ndani ya taasisi za serikali kuna vyama vya aina hii. Kwa mfano ndani ya wizara kunaweza kuwa na chama cha idara, chama cha ma-ps nk, vyuoni kuna vyama vya wahadhiri nk. Lengo ni kusaidiana.

Chanzo cha vyama hivi ni kukabiliana na hali ngumu ya maisha na majanga mfano misiba, kuuguza, gharama za harusi na hata kukopeshana kwa riba nafuu. Kwa mfano kuna kitu wahudumu wa bar wanaita mchezo, hii huwasaidia kuchangiana fedha ili kujikwamua kimaisha. Kutokana na michezo hii wanaweza kununua furniture, TVs, kulipa kodi za nyumba nk.

Sasa kuvipiga marufuku hivi vyama ni kudidimiza juhudi za wananchi kujikomboa kimaisha. Jambo hili linapaswa kukemewa na kulaaniwa.
 
Mnyeti anaweza akawa amepata some clues za nini mikutano hiyo ililenga. Kumbuka ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Manyara.

Na kwanini iwe kwa wenye asili ya Kilimanjaro pekee wakati wenye asili ya Singida, Mbeya, Tanga, Mwanza , Kigoma na Kagera hawajaguswa.
Japo nao wamepewa onyo kama wakijihusisha na mambo ya ovyo nao watapigwa marufuku.
 
Vikundi vya kusaidiana kupitia umoja mbalimbali vipo nchini siku nyingi. Na vikundi hivi huwa na maslahi ya pamoja huku vikiwa vimejengwa ktk misingi ya kusaidiana ktk mambo ya kijamii na kiuchumi, na kwa kadiri viwezavyo hujiepusha na mambo ya kidini na kisiasa.

Ndani ya vikundi hivi ni mkusanyiko wa watu wenye dini, jinsia, itikadi, umri na hata elimu tofauti. Hitaji kuu la wanachama ni fursa ya mafao yapatikanayo ktk siku zenye changamoto kwa muhusika, mathalani kufiwa, kuuguliwa, majanga ya moto ama mafuriko na vitu kama hivyo.

Vikundi kama hivi vimekuwa ni maarufu kwa yale makabila yenye maendeleo, na ktk hili huwezi kabisa kulikwepa kabila la Wachagga. Kwa kuwa wameishi na utaratibu huu kwa muda mrefu, na wanahimizana kuishi na utanaduni huu kokote kule ulimwenguni. Mimi si Mchagga, lkn mke wangu ni Mchagga, ninona fahari kubwa juu ya ustaarabu wa hali ya juu kutoka ktk kabila hili.

Kutokana na "urbanisation" makabila mengi huguswa nchini huguswa na tamaduni na utaratibu mzuri wa uendeshaji wa maisha kutoka ktk kabila hili, ikiwemo uendeshaji wa shughuli za kijamii mfano kusherehesha hafla mbalimbali, kufanya harambee za maendeleo na kujali elimu na kupenda walikotoka.

Katika hili la Mh. Mnyeti hana chochote kile "substantial" zaidi ya hisia za chuki za kikabila ama kukwepa kuwajibika kutoa michango. Badala ya kuwasisitiza wazawa wa mkoa wa Manyara waige mazuri kutoka kwa watu wa makabila mengine ambayo yanaonyesha mfano jinsi ya kushikamana kwa pamoja ktk shida na raha, yeye pengine ni "anti social" kwa anatumia marufuku hiyo ana nia kuficha madhaifu yake kupitia suala hilo ili kukwepa kuchangia watu wa mkoa wake ama wa kabila lake.
 
Kwanza mimi siyo mchaga hata tindo analielewa hili.

Pili ninachosema katika mada yangu ni kwamba Umoja wa watu wa mkoa fulani siyo Umoja wa kabila......kwani hakuna kabila linalohitaji umoja kwa sababu Kabila tayari ni moja ila Makabila ndio yanaweza kuwa na umoja.

Wewe kuwa mpare hakukufanyi uwachukie wachagga kwa sababu baadae utagundua wewe ni mgweno na hiyo dhambi haitakuacha!
Unatoa maneno ya jumla sana bila kuelewa undani wa umoja wa kikabila. Kuna makabila yameunda umoja huo kwa lengo ovu kwa makabila mengine na moja ya makabila hayo ni Wachaga. Wanaunda umoja wa wachaga Shinyanga wanakoishi na kufanya biashara. Wanapanga mipango ya maendeleo ya Moshi na kuchanga pesa kupeleka moshi, siyo shinyanga wanapoishi na kuchuma mali. Wanaitisha vikao vya kuamua mchaga gani aletwe kuwa kiongozi wa kanisa Manyara au Sumbawanga. Wanapeana anuani za mahoteli ya wachaga ili wakisafiri wasiende hoteli ya kabila jingine. Wanatangaziana makanisani pandeni mabasi ya mchaga mwenzetu tumuunge mkono.

Mambo haya yanaposemwa hadharani ndo afya ya taifa kuonesha tunachukia tabia yao. hakuna haja ya kupamba malengo ya umoja na kujifanya hatujui ubaya wake.
 
Hapo umeona kanisa tu? Hahaha eti Tanzania yote Ni Sawa? Kwahyo moshi vijin kulivyo jengeka utafananisha na tandahimba? Hebu acha vituko
Hapa ni marangu(moshi vijijin) View attachment 1284400

Unapoteza Muda bure, Nipo huku had sasa na nimekaa wiki ya tatu hii, vijana kwa wazee huku wanakunywa tu mbege, Vijana wa mjini mkipata something mnakumbuka walau kuja kuwajengea wazee nyumba, yenye aluminum roof na umeme na koki ya maji nje, mtu ukimwachia elfu 10 anakuona kama mungu mtu.. ni Ulimwengu wa Tatu tu kama sehemu nyingi za Tanzania na Africa kwa Ujumla, mvua ikinyesha hata kwenda kwa jirani huwezi maana ni tope na Landscape ya huku ni Vimilima na miinuko, tofauti kati ya Mtanzania wa Kilimanjaro na wa mbeya au Songea haipo. Nasema nikiwa namaanisha.
Otherwise huku kuna hali ya hewa nzuri na mvua ni nyingi, Kama kungekuwa kumejengeka basi kungependeza sana.
 
Back
Top Bottom